Shaka Hamdu Shaka: Sukuma ndani! "Mkibaini mchwa yeyote popote wa fedha za miradi ya Umma"

Shaka Hamdu Shaka: Sukuma ndani! "Mkibaini mchwa yeyote popote wa fedha za miradi ya Umma"

Kama mambo ndio haya basi Tanzania kama kuna wakati tumepata Rais bora na wa kweli nadhani ni sasa,Tufanye kazi kwa bidii sana,

Hakika huyu Mama ni Mpango wa Mungu,

#WATANZANIA TUFANYE KAZI KWA BIDII
 
" Kwa mwendo huu Tanzania tutafika tunakotaka kwenda tena kwa kuwahi sana, Hongera Mama Samia, Watanzania tuko nyuma yako We chapa kazi achana na Wasio na jema "
 
Huyu bibie anaehamasisha ufisadi mchana kweupe tena kupitia TV ya Taifa atasukumwa ndani lini?👇🤡🤡🤡
 
ubadhilifu wa pesa za miradi yote zikiwemo pesa za mkopo wa TZS 1.3Trilioni toka IMF ambao Rais wetu ameupata kwa sababu tu ya imani ya Wahisani kwake na kila mtanzania atahusika kuulipa mkopo huo hivyo pesa hizo sio Sadaka zilindwe kwa wivu mkubwa,
Hivi hizi fedha alikopeshwa Samia au Serikali ya Tz?
Hivi nani aliwapora hawa watu akili?
 
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka wakati akisoma Azimio la kumpongeza Mwenyekiti wa CCM ambaye ni amiri Jeshi Mkuu na Rais wa JMT Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri zilizotukuka tena zilizofanyika kwa kipindi kifupi Shaka amewataka Viongozi wote wa Kamati za Siasa kuanzia Kata, Wilaya hadi mkoa kuhakikisha hakuna senti moja ya mradi wowote wa umma|Serikali inatafunwa na aliyewaita " Mchwa " yaani majizi,

Mhe Shaka amewakumbusha Viongozi wa kamati za Siasa kuwa Chama Cha Mapinduzi ndio Chama kilichopewa ridhaa na Watanzania na ndio chenye Jukumu la kuhakikisha Wananchi wanafikiwa na huduma zote muhimu kwa wakati kwani Ilani inayotekelezwa ni Ilani ya CCM ya 2020|25,Mhe Shaka amesisitiza miradi yote ya mkopo wa IMF kwa mujibu wa Serikali itamalizika baada ya miezi tisa ( 9 ) hivyo kamati zote za Siasa zifuatilie kwa Ukaribu sana miradi hii,

Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi Taifa amesema kuwa Chama cha Mapinduzi hakitamvumilia yeyote atakayehusishwa na rushwa au Ufisidi wa fedha za miradi ya wananchi huku akiwataka kamati zote za Siasa kuzielekeza dola kuwafikisha michwa hao kwenye vyombo vya kisheria ikiwa ni baada ya kujiridhisha kuwako na ubadhilifu wa pesa za miradi yote zikiwemo pesa za mkopo wa TZS 1.3Trilioni toka IMF ambao Rais wetu ameupata kwa sababu tu ya imani ya Wahisani kwake na kila mtanzania atahusika kuulipa mkopo huo hivyo pesa hizo sio Sadaka zilindwe kwa wivu mkubwa,

Shaka Hamdu Shaka moto Fire, Kazi iendelee
 
Back
Top Bottom