Shaka: Rais Samia ametoa fursa za mikopo kwa Vijana, wanawake na walemavu wote hata kwa wale wa kambi za Upinzani

Mwanahabari wa Taifa

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2020
Posts
1,588
Reaction score
956
Your browser is not able to display this video.

Katibu wa Nec Itikadi & Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka akiwa katika mwendelezo wa ziara zake kanda ya Magharibi amenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari akisema " Chama cha Mapinduzi hakitatazama Itikadi katika kuwanufaisha vijana, wanawake na wenye ulemavu kutoka katika fursa mbalimbali zikiwemo mikopo.



Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kinafuatilia kwa karibu utekelezaji wa mikakati ya kuwakwamua vijana dhidi ya umasikini, huku kikiwataka watumishi wa umma kutafsiri kwa vitendo juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kuwatengenezea vijana fursa za kujikwamua kiuchumi na kijamii.



Hayo yamesemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, alipokuwa akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Ifuta, Kata ya Ukondamoyo wilayani Urambo alipokagua ujenzi wa kituo cha Afya Ifuta.



Rais ameonyesha njia, njia ya kwanza ni kushusha fedha nyingi katika Halmashauri zetu za Wilaya kwa ajili ya kujenga au kuanzishwa kwa miradi ya maendeleo. Tuliahidi ajira milioni nane katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa vijana na wanawake mpaka ifikapo mwaka 2025.

"Kazi kubwa anayoifanya Rais Samia ni kutumia fedha za ndani kutengeneza fursa za ajira ili wananchi wajikwamue kiuchumi. Ni jukumu la watendaji wa serikali kutafsi kwa vitendo ili lengo hilo litimie na wananchi hususan vijana, wanawake na walemavu wakwamuliwe kiuchumi.



Shaka amesema CCM itaendelea kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mkakati wa serikali ili ahadi ya Chama kupitia Ilani ya Uchaguzi itekelezwe na kufikia malengo.

Aidha, amesema katika kuwakwamua vijana CCM haitatazama Itikadi yoyote bali inataka kuona fursa zinapatikana na wote wananufaika.

=== ===
 
Hawa kenge Hawa, kwani pesa ni ya CCM? Kwani hao "Kambi za upinzani"hawalipi Kodi,hawakstwi tozo?
Kwanza pesa hajatoa yeye,pesa ni wananchi yeye anasimamia tu(bahati mbaya kijambazi)
 
Hawa kenge Hawa,kwani pesa ni ya ccm? Kwani hao "Kambi za upinzani"hawalipi Kodi, hawakstwi tozo?
Kwanza pesa hajatoa yeye,pesa ni wananchi yeye anasimamia tu(bahati mbaya kijambazi)
Ndio maana amesema hadi nyie CHADEMA mkachukue manoti Ila mkumbuke kurudisha Ili na wengine wapewe,

#SAMIA JEMBE SANA
 
Chadema fursa hiyo kachukueni hela achaneni na ukamanda uchwara mjenge familia
 
Hawa kenge Hawa, kwani pesa ni ya CCM? Kwani hao "Kambi za upinzani"hawalipi Kodi,hawakstwi tozo?
Kwanza pesa hajatoa yeye,pesa ni wananchi yeye anasimamia tu(bahati mbaya kijambazi)
Daaah kenge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…