Shaka: Wanaotaka Urais 2025 wasahau, ni Rais Samia bara ni Rais Mwinyi visiwani mpaka 2030

Shaka: Wanaotaka Urais 2025 wasahau, ni Rais Samia bara ni Rais Mwinyi visiwani mpaka 2030

View attachment 2322973
Katibu wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema hakuna shaka Rais Samia Suluhu Hassan ataendelea kuwavusha watanzania hadi 2030 kutoka na uwezo mkubwa uliounesha katika uongozi na utendaji uliotukuka. Akizungumza katika kongamano maalum la kumpongeza Rais Samia huko Unguja leo hii, Shaka amesema Rais Samia pamoja na Rais Dkt. Hussein Mwinyi ni viongozi shupavu walioonesha ari kubwa ya kuwatumikia watanzania.

Shaka amesisitiza kutokana na kazi nzuri ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025, inatoa uhalali kwao kuendelea kuiongoza nchi yetu panapo kudra za mwenyezi Mungu mpaka 2030. Ikiwa pia ni utii wa katiba ya CCM, kanuni na utamaduni tuliojiwekea.

Aidha, Shaka amesema wale wenye ndoto ya Urais 2025 kwa bara na visiwani wasahau kwakuwa CCM inamila, katiba, desturi, utaratibu na miongozo mbalimbali zinazotawala muda wa Rais kudhaminiwa na Chama cha Mapinduzi.

===
Tutammis sana huyu mwamba
 
2025 fomu ya Uchaguzi iprintiwe moja tu, Kila Rais wa CCM alihudumu miaka 10, tunataka amani na utulivu kwenye Taifa,
Acha uchawa wa kipuuzi wewe. Tunataka wanamapinduzi kutuongoza. Lazima mama kama anataka kuendelea kuingoza nchi apitie kwenye mchakato kugombea nafasi ya uteuzi kua mgombea urais. Kwenye nafasi ya urais hatutaki viti maalum. Tunataka mtu mwenye uwezo muadilifu na muomini wa itikadi ya chama chake.
 
Back
Top Bottom