Shaka: Wanaotaka Urais 2025 wasahau, ni Rais Samia bara ni Rais Mwinyi visiwani mpaka 2030

Unaoushahidi au Vuvuzela as usually
Unahitaji ushahidi gani?.
Mpaka utakajinyea bila kujua ndio utahitaji kupewa ushahidi
Mwana waziri wa ardhi - Wamasai wanafukuzwa ili Mwarabu apate ardhi!
Na bado
 
Unahangaika Sana wewe jamaa,
 
2025 hatutaki mtu zaidi ya Rais Samia Suluhu Hassan,

Kazi anazofanya huyu Mama hapa Upinzani kuweka mtu ni kujipotezea gharama bure kabisa,

Acha dhihaka. Ndio mlisema hivi 2020. Mwisho wa siku mkaengua wagombea wa upinzani na kuzima internet nchi nzima. Waoga wakubwa. Mpo madarakani kwa sababu ya dola. Siku dola ikiwa neutral bila kuegemea popote hamta pata kitu.
 
Urais ni uwezo na Si Zawadi mtu azawadiwe!!!

Kwamba wakiruhusiwa wengine kuchukua fomu watavuruga amani kivp?

What if mgombea wa CCM akionekana hatoshi dhidi ya upinzani?

Nisikuchoshe maana 2025 hapatakuwa na uchaguzi pia mwaka huo ni mbali Sana Bado.
Rubbish
 
Kwakuwa maamuzi ni ya mkutano mkuu kumpitisha mgombea, basi kiongozi shaka asubili muda na wakati utakapotimia na afahamu hakuna mkutano mkuu uliowahi kumpitisha Rais Samia kugombea nafasi hiyo bali ameupata kwa kudra za Mungu kama alivyowahi kunena mwenyewe.

Binafsi naona kuna haja ya nafasi hiyo ya urais, chama kuruhusu wanachama wake kugombea kama ilivyokuwa kwa marais waliopita na wala hakujawahi kuwa na utamaduni, mila, desturi, taratibu, kanuni, sheria au katiba yenyewe ndani ya CCM inayoeleza juu ya taratibu za kugombea nafasi hiyo nyeti ndani ya nchi endapo tu Rais aliyeko madarakani atarithi nafasi hiyo kutoka nafasi aliyepo tofauti na hivyo Shaka aeleze ni wapi pameandikwa utaratibu huo alioutaja.

Naamini muda ukiwadia,wapo wanachama watajitokeza kumpokea Rais Samia kijiti vinginevyo itolewe fomu moja kama ilivyowahi kutokea nyakati za nyuma jambo ambalo si demokrasia wala afya kwa chama.
Halafu kwa akili kama hizo za viongozi wa CCM mnadhani wapo tayari kuanzisha mchakato wa katiba mpya ikiwa tu katiba ya chama Chao hawaiheshimu kiasi hicho? Mungu tu asimame mahali pake kwenye jambo hili.
 
Hakika mchakato wa katiba mpya bado ni kitendawili kisichoteguliwa kwakuwa viongozi wanazani ni katiba ni mali yao binafsi wakati ni mstakabali wa nchi kwa ujumla.walamba asali na wanywa maziwa,wanazani watapunguziwa nguvu ya unywaji maziwa kwa mirija, hivyo katiba mpya kuonekana mwiba kwao lakini kila jambo na wakati wake, muda utafika na watanzania tutapata katiba mpya na kuachana na viraka visivyotimilka.
 
Asali gani?. Mafuta ya petroli 3500 Lita. Acheni ushabiki wa kijinga wakati mfumuko wa Bei umewashinda.
Mfumko hakuna anayeweza kuuzuia hata Nyerere ktk utawala wake vitu vilipanda bei so ktk uchumi hicho ni kitu cha kawaida tu
 
Shaka

ACHA hizi ndugu yangu

Inna lah maaswabirina

"Rasimu ya WARIOBA irudi mezani Sasa iwe KATIBA Mpya"!
Huyu bwana mdogo ww muache aendelee kutapika anadhani watanzania wanachekelea sana maisha haya ya kijinga na kipumbavu.Samia anatudanganya eti halali,yaani uongozi wa kijinga wa namna hii ndio unashindwa kulala,hv hata ulitazama sababu za Samia kukosa usingizi huzioni,afadhali aendelee kulala.
 
Nakubaliana na wewe comredi, Iwepo fomu moja tu ya Urais,

Kazi anazofanya Rais Samia hatuhitaji aletewe bugudha kabisa,

Wamwache Mama achape kazi,
Kwahiyo nchi yetu sote mnajipangia kibabe ? Namna ya kututawala?
 
View attachment 2322973
Katibu wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema hakuna shaka Rais Samia Suluhu Hassan ataendelea kuwavusha watanzania hadi 2030 kutoka na uwezo mkubwa uliounesha katika uongozi na utendaji uliotukuka. Akizungumza katika kongamano maalum la kumpongeza Rais Samia huko Unguja leo hii, Shaka amesema Rais Samia pamoja na Rais Dkt. Hussein Mwinyi ni viongozi shupavu walioonesha ari kubwa ya kuwatumikia watanzania.

Shaka amesisitiza kutokana na kazi nzuri ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025, inatoa uhalali kwao kuendelea kuiongoza nchi yetu panapo kudra za mwenyezi Mungu mpaka 2030. Ikiwa pia ni utii wa katiba ya CCM, kanuni na utamaduni tuliojiwekea.

Aidha, Shaka amesema wale wenye ndoto ya Urais 2025 kwa bara na visiwani wasahau kwakuwa CCM inamila, katiba, desturi, utaratibu na miongozo mbalimbali zinazotawala muda wa Rais kudhaminiwa na Chama cha Mapinduzi.

===
Akili ndogo huondoa maarifa!!
 
Hata mwendakwao.mlimsemea sana acheni uchuro!
 
Kazi inaendelea kufanyika
 
Back
Top Bottom