Shamba eka 4 Kimbiji Kigamboni linauzwa

Shamba eka 4 Kimbiji Kigamboni linauzwa

Daaa hii fursa nzuri sana. Bei kitonga kabisa hiyo.
Karibu sana mkuu. Bei kitonga mno. Kwa eka moja hiyo bei iko kitonga hasa maana ukiwa na mtaji wa ziada ukaamua ufanye kilimo misimu miwili tu hela yako inarudi unabakia na ardhi yako
 
Pia kama unapenda kufanya ufugaji unaweza kufuga kuku, mbuzi, ng'ombe au hata kondoo. Panafaa sana kwa shughuli hizo pamoja na kilimo
 
Wakuu nazidi kuwakaribisha mjipatie eneo Kimbiji ambalo mtalitumia kwa matumizi mbalimbali kuanzia kilimo, ufugaji hadi makazi. Bei ni chee kabisa.
 
Uzuri wa eneo lenyewe hata kama unatumia usafiri wa umma kwenda kule hautahitaji kutumia bodaboda kwenda shamba maana kutoka barabara kuu mpaka shambani ukiamua kutembea ni dakika 10 au 15 tu na hapo ni kwa mwendo wa kujivutavuta yaani mwendo wa kawaida. Kwa pikipiki ni dakika 3 uko shambani
 
Wataalam karibuni mjitwalie shamba kwa bei sawa na bure. Unaweza kuweka hata makazi maana huduma za msingi kama barabara, maji na umeme ziko karibu sana
Vipi barabara za kuelekea shambani zina hali gani? Zinapitika muda wote wa mwaka? Kama umbali kutoka barabara kuu ni mfupi kiasi hicho nitakutafuta tuyajenge nipate japo eneo dogo mkuu
 
Vipi barabara za kuelekea shambani zina hali gani? Zinapitika muda wote wa mwaka? Kama umbali kutoka barabara kuu ni mfupi kiasi hicho nitakutafuta tuyajenge nipate japo eneo dogo mkuu
Karibu sana mkuu. Barabara ya kutoka barabara kuu kwenda shambani imechongwa vizuri na kushindiliwa na kifusi cha mawemawe hivyo inapitika muda wote hata mvua ikinyesha namna gani. Pia barabara inapita pembeni kabisa ya shamba. Karibu tufanye biashara ndugu yangu.
 
Daaa hii fursa nzuri sana. Bei kitonga kabisa hiyo.
Ni kweli kabisa kiongozi. Bei hii ni kitonga mno. Nauza kwa kuwa kuna mambo nataka kuyaweka sawa. Bei ninayouza ni bei ambayo mtu akinunua na akatulia akaamua akate viwanja vya mita 20 kwa mita 20 anapata viwanja kama 9 na kiwanja kimoja akiuza milioni moja na nusu atapata faida nono mno. Karibu kiongozi tufanye biashara
 
Shamba lenye ukubwa wa ekari 4 linauzwa. Shamba liko Kimbiji wilaya ya Kigamboni, Dsm. Shamba liko mita 800 kutoka barabara kubwa ya Kigamboni Pembamnazi. Bei ni mil 5 kwa kila eka. Umeme upo karibu sana na shamba. Tuwasiliane kwa anayehitaji.View attachment 1657764
Panavutia sana. Naona tambarare nzuri sana.
 
Kweli vyuma vimekaza...yaani mwezi mzima nauza shamba kwa bei ya chini kabisa lakini hakuna wateja...imagine upate eka moja kwa Dar tena Kigamboni Kimbiji yaani mita 70 kwa 70 kwa milioni 5 tu si sawa na bure? Unajipatia upepo wa baharini bure kabisa maana shamba liko umbali wa kilomita 1.8 kutoka ufukwe wa bahari. Ukitaka kwenda ufukweni na familia kubarizi hata kwa miguu unaenda tu.
 
Na kwa Kimbiji kwa sasa zinaendelea kujengwa hoteli matata sana pembezoni mwa barabara ya kutoka Kigamboni kuelekea Pembamnazi hivyo ni maeneo ambayo hapo baadae kidogo yatakuwa na thamani ya juu mno. Hebu njooni mjipatie eneo la kuwekeza kwa kilimo na makazi kwa bei sawa na bure
 
Shamba lenye ukubwa wa ekari 4 linauzwa. Shamba liko Kimbiji wilaya ya Kigamboni, Dsm. Shamba liko mita 800 kutoka barabara kubwa ya Kigamboni Pembamnazi. Bei ni mil 5 kwa kila eka. Umeme upo karibu sana na shamba. Tuwasiliane kwa anayehitaji.View attachment 1657764
Mkuu hili Shamba bado lipo? Hebu njoo PM tuyajenge maana naona ni eneo Zuri sana
 
Shamba lenye ukubwa wa ekari 4 linauzwa. Shamba liko Kimbiji wilaya ya Kigamboni, Dsm. Shamba liko mita 800 kutoka barabara kubwa ya Kigamboni Pembamnazi. Bei ni mil 5 kwa kila eka. Umeme upo karibu sana na shamba. Tuwasiliane kwa anayehitaji.View attachment 1657764
Kwa anayehitaji mali bado iko sokoni. Tuwasiliane
 
Back
Top Bottom