Shamba nililonunua kwa Tsh laki 3 mwaka 2009 leo hii thamani yake imevuka Tsh 40m

Shamba nililonunua kwa Tsh laki 3 mwaka 2009 leo hii thamani yake imevuka Tsh 40m

Wakuu wiki hii kwa mara ya kwanza nimepata uhakika wa bila kuhadithiwa na mtu umuhimu wa kumiliki ardhi au nyumba. Ninakumbuka nilikuwa bado niko chuo, mzee wangu akaniambia nimtumie Tsh 50,000/= kuna mchongo wa shamba eka 1 anichukulie. Sehemu yenyewe ilikuwa porini ambapo sikuwahi kuota maendeleo yangefika. Nilimtumia laki 1 baadae nikaongeza ikafika laki 3 nikapata eka 6. Mzee naye akanunua eka nyingi zingine akawagawia watoto wake wengine.

Nakumbuka kama familia tulijitahidi kuendeleza japo kidogo ili kuweka ulinzi kuzuia uvamizi au kunyang'anywa na mamlaka. Chini ya serikali tukufu ya CCM hadi kufika mwaka jana lile eneo tayari lina umeme na maji. Hata barabara ya kufika kule iko vizuri. Watu kibao wameshajenga nyumba za kutosha. Pori litapotea.

Sasa wiki hii aliyekuwa jirani yangu kauza shamba lake eka 7 kwa 60m cash. Kiukweli sikudhania kabisa inaweza fika thamani hiyo. Binafsi nimehakikishiwa nikitaka kuuza langu haiwezi pungua 40m.

MORAL LESSON: Vijana wadogo chini ya 30 years msijiumize kununua viwanja vya 20 × 20 mijini kwa bei mbaya. Nendeni vijijini mkashike maeneo kwa bei rahisi. Baadae yatawasaidia. Miaka 15 ijayo sio mingi endapo utajaliwa kuishi. Kingine heshimuni wazazi, walezi na wakubwa wengine wanapowashauri jambo. Awe maskini au tajiri wewe msikilize. Awe CCM au upinzani msikilize. Wakubwa wameshafanya makosa mengi na huwa hawapendi sisi tukosee tena.
Sijajua shamba langu la ekari 30 litafika bei gani 2040 maana lipo km 3 kutoka Barabara Juu ila ni Kijiji Cha ndani ya Manispaa (Town Outskirt ) ambako Kwa Sasa Bado ni Mashamba.
 
Wapi namimi natapata heka za bei iliopoa ninunue pori langu najua one day tuu
Labda Vijijini ila jirani na Miji andaa pesa ya kuzidi.

Kwa maeneo ya Vijijini kupata eneo la pamoja ni nadra ila yanapatikana mpaka upate mwenyeji.

Kuna mtu alikuwa anauza pori la eka 50 ila anataka walau mnunuzi wa eka 20 Kwa pamoja sijajua kama amepata mteja au laa.

Hapa nilipo Kuna mtu nimebhatusha kaniuzia eka 35 km 5 tuu kutoka lami sawa na km 20 kutoka mjini lakini ni Kwa vile ni wananifahamu ila vinginevyo kupata ni ngumu.
 
Labda Vijijini ila jirani na Miji andaa pesa ya kuzidi.

Kwa maeneo ya Vijijini kupata eneo la pamoja ni nadra ila yanapatikana mpaka upate mwenyeji.

Kuna mtu alikuwa anauza pori la eka 50 ila anataka walau mnunuzi wa eka 20 Kwa pamoja sijajua kama amepata mteja au laa.

Hapa nilipo Kuna mtu nimebhatusha kaniuzia eka 35 km 5 tuu kutoka lami sawa na km 20 kutoka mjini lakini ni Kwa vile ni wananifahamu ila vinginevyo kupata ni ngumu.
Umepata sehem nzur sana
 
Pole sana mkuu.. wazazi wengi wa kiafrika wazinguzi mno ndo maana wengi wao uzeeni hulalamika kutelekezwa na watoto. Mimi pia haikuwa rahisi kwenda sawa na baba yangu... nakumbuka mara ya mwisho kuchukua ada kwake ni term ya kwanza form 5. Nilikuwa ikifika likizo napiga vibarua kama sina akili. Nilifahamu vichochoro vyote vya Arusha. Hata chuo alikuja kujua nipo baada ya kuanza kusoma. Kuna mjomba wangu alinikalisha chini na kunielewesha kuwa nifanye nifanyavyo niwe sawa na mzazi. Nilichukua ushauri wake na kuanza kuyajenga. Tukaanza kuwa marafiki ingawa wa mashaka kimtindo.
Ongera mkuu Kwa kuelewana na wazee wako, lakini kwangu Bado ngumu kidogo sina mahusiano mkuu tatizo ni uchawi niliamua kujiweka mbali nao Kwa sababu za kiusalama zaidi kiukweli uchawi wa ndani ya familia ni mbaya sana ndio chanzo cha matatizo mengi ninayopitia mpk sasa.
 
Back
Top Bottom