Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Zilimpata 16 na zikaja kuondokewa zaidi ya 28 mwilini mwake kule Nairobi kama mnakumbuka mlisema hivyo.

Uongo unahitaji kumbukumbu fasaha sana, haya mwenye akili nyingi hadi kushindwa idadi mbili tofauti hongera kwa kuwa na kichwa ombwe
Weka hapa clip iliyosema 28. Utoto katika majeraha ya binadamu hauvumiliwi hata kidogo.
Weka hapa kudhibitisha vinginevyo tutakuona mpuuzi
 

Kumbe tatizo ni kuona huo ujinga wako wa zamani unadhani wote ni wajinga wa hivyo. ww baki na ujinga wako lakini hili la Lissu wala hatuhitaji mifano yoyote maana hii issue iko wazi tu. Unaweza kukesha hapa na kutoa mifano na utetezi wako upendavyo kwani ni haki yako. Lakini kwa hili la Lissu hatupepesi macho.
 
Hizo hazinisumbui,ukisema walinzi na waliotoa camera wanahusika siwez kataa,lkn ukisema dereva hausiki ntakataa hadi kufa.
Hahusiki kwa sababu mjeruhiwa mwenyewe kama Principal witness anasema hahusiki huyo dereva kwa nini wewe ukatae mpaka kufa kama vile wewe ndio mpangaji Wa njama hizo and you have got evidence to prove what you are saying?
 
Pale unapoamua kubishana na reliable sources kwa sababu ya rangi ya chama, stupid ,jinga kabisa.
 
Nilikuwa nakuheshimu kama GT ila sasa nakupuuza.
 

Ninachopenda kwenu ni Msisitizo wa hii kauli " Uhuru wa maoni na mawazo tofauti"
 
Pole sana Kaka yangu Kitasnia na Kamarada ( Comrade ) Ndugu Pascal Mayalla kwani sijapitia ' pages ' zote ile kwa nilizozipitia niweza Kugundua tatizo Kubwa lililopo katika Kizazi cha Watanzania kwa sasa. Watu wanaongozwa na ' mihemko ' ya Kisiasa pasipo kuangalia Uhalisia wa jambo na hata hao wanaolilazimisha ili liaminike hivyo ukisikiliza tu ' arguments ' zao haraka sana utakubaliana ule Utafiti kuwa Elimu nzima ya Tanzania kwa miaka ya hivi karibuni ipo katika ICU.

Pole pia kwa Kushambuliwa Wewe kama Wewe kimaelezo na baadhi ya Wachangiaji wetu wale wale ambao Mimi siku hizi nawaita ' Wachangiaji Oya Oya ' ambao Wao kufauta mkumbo na kuamini Upuuzi ndiyo jadi yao huku wakiaminishana huko katika Vijiwe vyao.

Nilishasema katika Uzi mmoja ambao niliwahi Kuuandika hapa hapa Jamvini na leo tena narudia lile lile tena nikiwa najiamini kabisa kwani huhitaji kuwa na Elimu kubwa sana kuweza kujua mchezo mzima ulivyo na nini kinaendelea. Nitakataa mpaka siku ya mwisho kama Tundu Lissu alishambuliwa na Watu wa ' System ' wa Serikalini ( Idara Nyeti ) kama ambavyo humu mitaani na uswahil tunavyoaminishana.

Hapa wala tusidanganyane kama kweli ' System ' ingekuwa inamtaka na imemdhamiria Tundu Lissu sidhani hata kama angeweza na kuthubutu kuwakwepa au kushindana nao. System zote au nyingi zilizoko duniani huwa hazitumii na haziwezi kutumia ile mbinu ya Kipumbavu iliyotumika kule Dodoma. Hivi Tundu Lissu ana ' ubavu ' kweli wa kukwepa ' assassination trap ' kama ' Wanamume ' wamemdhamiria kweli?

Yaani kwa jinsi leo hii ' Teknolojia ' za masuala ya Kijasusi zilivyokuwa na mbinu mpya zilizopo ambazo hata hazihitaji nguvu Kubwa kutumika inawezekana kweli ' System ' ikatuma Watu vile halafu Watu ambao ni ' highly trained and qualified ' kabisa wakarusha risasi 38 halafu bado Mtu awe hai? Jamani hebu muda mwingine tuweke hizi Chuki zetu za Kisiasa pembeni na tujikite zaidi katika Uhalisia wa jambo husika.

Sina ufahamu kihivyo wa masuala haya ( nikimaanisha Kitaaluma na Kiutendaji wake ) kama walivyo wengine ila kwa maarifa machache sana niliyonayo ni kwamba sehemu yoyote ile na hasa kwa tukio zima ambalo limemtokea Mtani wangu wa Kinyiramba Mheshimiwa Mbunge Tundu Lissu kamwe hata kama liwe limekuwa ' coordinated ' na ' anonymous Fellas ' ila kwa 99% lazima pia kutakuwa na Watu wa karibu na Mlengwa / Mhusika wametumika katika kulifanikisha. Mifano ya hii iko mingi sana karibia Watu wengi ambao walikuwa ' assassinated ' ilikuja kugundulika baadae kwamba hata Watu wao wa karibu nao walihusika either directly or indirectly sasa nashangaa kwa hili la Tundu Lissu Watu wake wa karibu ama Kifamilia au Kichama wakigusiwa tu katika kutengeneza mtiririko mzima wa Kiushahidi na Kiuhalisia Watu wenye Mahaba na Siasa za ' Oya Oya ' wanaanza Kuhamaki, Kununa na Kukasirika huku wakidhani kwamba kila ama anayewapinga au anayelihoji hili Kiudadisi kabisa basi ni ' Pro Government ' na ni ' Anti Opposition '. Siasa za Kitanzania zimetufikisha pabaya mno ambapo hazitaki kuruhusu ' Fact Finding ' badala yake zimejikita katika ' rumors ' na ' double standards ' pekee.

Nina uhakika kabisa tena wa 100% kwamba hili jambo au Sakata la Tundu Lissu likifuatiliwa Kitaalam kama siyo Kiuweledi kabisa huenda kuna Watu wataficha Nyuso zao kwa aibu na hawatokuja Kuamini kile ambacho Kimejulikana na si ajabu kuna Watu wanaweza hata wakachinjana hasa kwa hasira za Kupotezeana muda na Kufitiana wao kwa wao. Ni suala la muda tu najua kadri siku zinavyoenda mbele ipo siku ukweli wa haki utajulikana na labda nimwombe tu Tundu Lissu kwamba siku ambayo labda atakuja Kuujua ukweli wa Yeye leo hii Kupewa Kilema kile asisite tena kuandika Waraka wake kutuomba radhi Sisi ambao tumefululiza Kutukanwa juu ya hili sakata lake.

Siku zote nasema na nitasema kwamba Wahenga waliposema KIKULACHO KI NGUONI MWAKO wala hawakukosea!

Akhsanteni na nawatakieni pia uchangiaji mwema wa huu Uzi wa Kaka yangu Mpendwa Kitasnia na Amani itawale Kwenu.
 
Brother kwani ukilewa ni lazima uchangie? Au unadhani watu watasema hujui kusoma na kuandika?

 
Pale unapoamua kubishana na reliable sources kwa sababu ya rangi ya chama, stupid ,jinga kabisa.

Kama nakumbuka vizuri waalimu walinifundisha kwenye tafiti Google haiwezi kuwa A reliable source. Huwezi kukaa mbele ya wanazuoni ukawaambia umesoma google badala ya kusoma vitabu. Thus why kwenye dessertation kwenye list ya reference zako Google unaweka chini kabisa ya Reference na unaandika Jina la site, link, tarehe, saa na ikiwezekana na mtu aliyeandika Sababu utakachosoma wewe sasa ndani ya sekunde 5 kinaweza kubadilishwa na mimi nikasoma kitu tofauti.
 
Pasiko bana ili bandiko lako limejaa changamoto binafsi, yaani unajaribu kusema nini kwa mfano? kama dereva anahusika alishirikiana na nani? hao alioshirikiana nao kwa nini wasikamatwe?
 
Padri aliyeuliwa Zanzibar mbona walikuja CIA,FBI na Scotland yard..kwa nini kwa Lissu isiwe hivyo
 
Kumbuka wangekuwa na nia wasingeshindwa kwenda kuwahoji hospitalI ya Nairobi.
Hata kama wangemuhoji huko Nairobi au Ubeligiji angesema hayo hayo ambayo amekuwa akiyasema kwenye social media na vyombo vingine vya habari kila mara ambayo hayana msaada wo wote wa kuwanasa hao assailant wake.

Kwa dalili zo zote dreva wake ni suspect number one.
1. Bunduki iliyotumika waliiona ni AK 47 iliyokuwa na full magazine (risasi 40) ambayo ilimimina risasi zote 40 at close range. Kati ya hizo 17 zilizama kwenye miguu, mikono na kiuno cha Tundu Lissu.

2. Risasi zilimiminwa kutoka upande wa kulia wa gari ambao ni upande wa dreva lakini dreva hakupatwa na risasi hata moja na alipata hata fursa ya kuteremka kwenye gari na kwenda ku take cover kwenye magari yaliyokuwa yamepaki eneo hilo. Assailants walikuwa upande wa kulia wa gari, hivyo risasi zilizama zaidi kwenye mguu wa kulia, paja la kulia, mkono wa kulia, kiuno upande wa kulia na kutokea tumboni na mkono wa kushoto. These are the documented medical forensic clues.

3. Majeshi yetu hayana bunduki za AK 47, yana SMG badala yake ambayzo full magazine zake ni risasi 30. Bunduki za AK47 zinamilikiwa na majambazi yanazozipata kutoka kwa wanajeshi wa Burundi wanaokimbilia Tanzania ambao huwa wanaziuza kwa bei ya shillingi 20,000 tu!! Silaha hizi ndizo zilitikisa huko Mkuranga, Kibiti na Rufiji.

4. Hakuna mwanajeshi ye yote (aliyepata mafunzo ya kijeshi) ambaye ampige mtu (adui) risasi 38 from an AK 47 gun at a close range halafu mtu huyo asalimike!! Never on earth. Kwanza atahitaji risasi moja tu na atafumua kichwa au moyo. Hivyo it is so obvious kwamba assailants wa Tundu Lissu walikuwa ni wahuni tu wa mitaani wasiojua kutumia bunduki. Yaani risasi 38 zote zinakosa target (kichwa au moyo) zinaishia kupiga makalio na hewa!! Hili halihitaji askari wa Scotland yard kulitambua. Swali ni nani aliwakodi hawa wahuni wasiojua shabaha? Kwa nini dreva wa Lissu akawa mkimbizi nchi za nje? Nini kakimbia? Kwani hata polisi wetu wakienda kumhoji huko kwani atasema lo lote la maana? Huko hawawezi kumu arrest. Alipaswa kuwa behind bars ili aeleze vizuri. Tundu Lissu alipaswa kujua hili. Mara nyingi kikulacho unacho nguoni mwako. Eti ninamuamini sana. Mbele ya pesa kunakuamini mtu? Yaani apewe shillingi million 500 aache kukumaliza? Yaani Tundu Lissu hajui kwamba "Money is the source of all evils in this world?"

5. Hospitali ya serikali ya Dodoma na madaktari wa serikali wa Dodoma hospital ndiyo waliookoa maisha yake. Kama serikali ilikuwa na mpango wa kumuua, ingalishindwaje kumumalizia hapo hapo kwenye hospitali yake ya Dodoma humo humo operation theatre? It was so simple eg hiyo damu aliyopewa hangeipata au angalipewa incompatible blood ambayo ingalimumaliza hapo kwa hapo! Lazima aishukuru serikali kwa kuokoa maisha yake badala ya kuilaumu. Upinzani haupaswi kuwa wa aina hii. Tujifunze kwenye nchi zilizotutangulia.

6: Bunduki kama AK 47 au SMG ikiunguruma si mchezo. Kwa askari yo yote trained, hata kama naye ana bunduki ya aina hiyo hiyo lakini kashutikizwa, reaction ya kwanza ni ku take cover. Atalala chini na ku craw hadi mahala salama. Hapo ndipo atatafuta kuona adui/ maadui walipo na kutafakari kama anao uwezo wa kupambana nao au kuomba reinfocement au kutokomea kabisa kwenye eneo hilo. Trained soldier hakurupuki tu kuanza kurusha risasi ovyo ovyo anapositukizwa na milio ya risasi. Hivyo kwa jinsi tukio lilivyotokea hapo usingalitarajia askari waliokuwa karibu na eneo hilo kuwa wangaliweza kuanza kujibu mapigo kwa muda huo mfupi uliotumika kabla ya majambazi hayo kutokomea kusikojulikana. Dreva wa Lissu aliyaona live na alitaja hata aina ya gari yalilotumia na plate namba zake. Polisi walikamata magari kadhaa ya aina hiyo lakini dreva huyo alikataa kwenda kuyatambua na hivyo yakabidi yaachiwe kwani hakuna shahidi aliyejitokeza. Shahidi muhimu alikuwa Nairobi akidaiwa anapata tiba ya kisaikolojia. Sasa hivi Lissu anasema dreva huyo yuko masomoni Ubeligiji. Sijui anasoma digrii gani hapo Leuven University teaching hospital anapotibiwa boss wake. Jamani aacheni kutufanya wajinga. Pascal yuko sahihi kabisa.
 
Kuna mambo mengi baada na kabla ya tukio yaliyopelekea mshukiwa wa kwanza ikiwa system mkuu....

Matukio ya kukamatwa mara kwa mara na yeye mwenyewe kutoa taarifa za kufuatiliwa na hiyo hiyo system

Unakumbuka hii.. huwezi nipinga kila kitu halafu nikakuacha salama

CCTV Camera zote ziliondolewa jirani na eneo la tukio,

Kuzuia kugharamia matibabu yake licha ya kustahili kutokana na nafasi yake

Kuzuia uchunguzi ulio neutral kwa mashirika ya kipelelez ya nje bila sababu za msingi ilihali ya ndani wako kimya.. na hii ndo kwa wenye akili inathibitisha uhusika wa hiyo system otherwise jibu lingeshapatikana nani muhusika

Umeshikilia a very light point ya kuiondoa system lawamani nayo ni ya njia iliyotumika.. Kumbuka hata yy alishajua njama za kuwindwa hivyo hiyo njia endapo ingefanikiwa ingesemwa tu kavamiwa na majambazi na kuuawa this story could over..

Kumbuka na wao wana jua njia hiyo ingekuwa very simple kuwaondoa lawamani kwa watu wasio na fikra pevu kama ambavyo hata ww unaamini system haiiusiki a very BIG NO ni suspect NO1
 
Paskali Mayala, katika hili na kwa mujibu wa yale unayoyaita maswali juu ya dereva wa Lissu huna hoja yoyote kwani maswali yako yote ni irrelevant. Hata hivyo bandiko la MH Lissu limegusia mengi hasa hali ya ulinzi kwenye makazi yao siku ya tukio, ongelea hilo kwani ndo la maana zaidi, Pia, vitake vyombo vya mabavu vifanye uchunguzi na kumhoji mtu yoyote vitakayedhani atasaidia kupata taarifa muhimu kuhusiana na tukio hili baya. Otherwise, umefeli bro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…