Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?

Maneno meengiii lakini majibu yake yapo kwenye security camera zilizokuwa kwenye nyumba za umma ambazo obviously ni mali ya umma ziliondolewa na nani?
Au na hili unataka dereva wa lisu ajibu?
Je yule aliyesema siku chache baada ya tukio kuwa akiwa shambani akiona nyoka anampiga akifa shauri yake akipona potelea mbali alitumwa na dereva wa lisu?
Kigugumizi cha bunge na polisi kufungua jalada ilikuwa wanamuogopa dereva wa lisu?
Pascal mayalla mnasoma ili muwe wajinga au muwe waelewa?
 
Tindo, Nimekukubali, binafsi sichoki kusema, sijui hawa wenzetu wanafiri mtutu wa bunduki ndio mwarobaini wa kila kitu hapa nchini, Kikwete alinukuliwa akiwaambia wafuasi wake kwamba tukizoea kukingiwa kifua na Polisi kuna siku Polisi nao watatuchoka, tujifunze kusimama wenyewe,
hivi huyu dereva angetaka kumuua Lissu alishindwa nini kumpiga risasi ya kichwa ambayo ingetosha sana kummaliza, tumeambiwa cCTV cameras ziliondolewa kwa maelekezo kutoka JUU.
 
Kismati, usiseme kwamba police walifake hilo tukio, na kwamba hawakutaka kumuua, washambiliaji walitumwa kwenda kummaliza apotelee mbali, sisi tunachoamini ni nje ya ufahamu wa binadamu na hii ni nguvu ya Mungu pekee, yaani mtu atoe onyo kwa kufyatua risasi tena sio moja ?, mtu akikushikia bunduki hata iwe bastora ujue ameamua kukuua
 
Eti anadiriki kusema kabisa "Lissu ashukuru serikali kuokoa maisha yake pale Dodoma hosptl maana serikali ingeamua ingemmalizia palepale"
Serikali haikuokoa maisha ya Lissu, walijaribu bila mafanikio kutaka kuagiza ndege kutoka Dar ije Dodoma ndio eti impeleke Nairobi ambapo ingechukua masaa mawili, wapenzi wa Lissu wakakataa na wakaamua kuchukua ndege nyingine maalumu ambayo ilitumia dakika 45 kufika Nairobi, yale masaa mawili yalilengwa kutumika kukamilisha uuaji
 
Sidhani kama ni uzee, inawezekana anautafuta U-Jerry muro wa Manyara, Mbona tunae Jenerali Ulimwengu ambaye hadi leo anaendelea kuusimamia ukweli ?.
 
Camera za kwa lisu zinasemaje kuhusu hili tukio?Au nazo zilitolewa au ziliwekwa chumban?
 
Kwanza haya madai yako unauthibitisho wowote au ndio nawe ulisikia?
 
Sioni hata mmoja wenu akijenga hoja zenye mashiko kwanini dereva asiwe suspected. Wengi mnaishia kuhitimisha serikali haiwezi kwepa ktk hili.Mimi sikatai,hoja yangu kwanini dereva asiwe pamoja na serikali ktk kufanya huu unyama?Hoja za camera wala walinzi sio kigezo cha dereva kutohusika au serikali kuhusika hakumaanishi dereva hawez husika.Tuwe rational tu ktk kufikir,
 
Kwanza haya madai yako unauthibitisho wowote au ndio nawe ulisikia?
Ndiyo kazi ya tume sasa kuchunguza yote sasa wenyewe hawataki. Jambo kubwa likitokea kila mmoja atasema yake mpaka taarifa rasmi itolewe sasa kama hakuna uchunguzi na haitolewi binadamu ataendelea kuunganisha dots na huwezi kuzuia speculations kwani ndizo huwa source ya taarifa
 
Lkn hizo speculations zako umezitoa kama information.
 

"Tusitegemee lolote jipya hapa.
Tundu Lissu, just get well soon, na sasa inakubidi uchangue kati ya kuendelea na uanaharakati na kuishi kwa mashaka, au uamue kupunguza makali na kuishi kwa amani".


Paskal hapa unatumika kabisa brother! Just think and get back to your mind
 
Misuli, naomba usitutusi kwa sababu tu tunaamini tofauti na unavyotaka tuamini, binafsi mimi huwa situkanwi, Kimsingi hata iweje dereva hawezi kuhusika, vizuri umesema anaweza kuhusika na serikali, tukubaliane tu kwa upole kwamba serikali ina mkono wake hapo, kama walimtumia dereva wewe ndie unaesema, ila serikali inahusika kwa 95%, na ndio maana hata majibu yao yamekuwa wazi kwamba they don't care about what happened to Lissu's attack. jaribu kuelewa basi.
 
Niungane na wewe msnajo.
 
Lkn hizo speculations zako umezitoa kama information.
Muache watu waseme kadri wanavyoweza mpaka pale walio na funguo za mamlaka ya nchi watakapoamka na kutoa majibu sahihi ili kuondoa hii sintofahamu, tukikaa kimya wataona tumekubali yaishe. Alisema Baba Askofu Munga.
 
Inawezekana kwenye mpango wa kutaka kumuua Tundu Lissu kuna mambo ambayo unayajua au unahusika .Hiki unachofanya kuna siku utakuja kujutia. Jana Tundu Lissu aliwajibu wajinga kama wewe kama hukupata muda wa kusoma.
Watu wetu waligundua hatari kubwa aliyokuwamo dereva kutokana na minong'ono hiyo. Wakaamua kumtoa Tanzania na kumleta Nairobi nilikokuwa nimelazwa mimi. Hakutoroshwa. Aliondoka na Mh. Godbless Lema na alipitia mpaka wa Namanga. Alipatiwa hati ya muda ya kusafiria na maafisa wa uhamiaji Namanga. Na wala hakufichwa Nairobi. Alikaa na mimi Nairobi Hospital kwa miezi minne.

Jeshi la Polisi la Tanzania lilimjulisha kaka yangu, wakili Alute Mughwai, kwamba litatuma wapelelezi wake kuja Nairobi kutuhoji mimi na dereva wangu. Tuliwasubiri mapolisi hao. Hawakuonekana mpaka wakati tunaondoka Kenya kuja Ubelgiji tarehe 6 Januari ya mwaka huu.

Dereva wangu hakutoroka Kenya kuja Ubelgiji. Ili aweze kusafiri kutoka Kenya kuja Ubelgiji, alihitaji passport ya Tanzania na visa ya Ubelgiji. Hakuwa navyo.

Hivyo, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Serikali ya Ubelgiji ilimpatia hati maalum ya kusafiria na kuingia Ubelgiji. Wakati mimi na mke wangu tulisafiri kwa passport za Tanzania; dereva wangu alisafiri kwa passport maalum ya Serikali ya Ubelgiji.

Hapa Ubelgiji anaishi mji mmoja na mimi. Amekodishiwa nyumba na anaishi kwa gharama za Serikali ya Ubelgiji, sio za CHADEMA au Mwenyekiti Mbowe au za kwangu mwenyewe. Anasomeshwa na Serikali ya Ubelgiji.

Bado anaweza kuhojiwa na wapelelezi kuhusiana na jaribio la mauaji dhidi yangu. Utaratibu wa kufanya hivyo upo kisheria, kwa mujibu wa Sheria ya Kusaidiana Katika Masuala ya Jinai iliyotungwa na Bunge la Tanzania. Lakini Jeshi la Polisi la Tanzania halitaki kufanya hivyo. Linafahamu mpango mzima wa 'watu wasiojulikana.'

Huu ujinga unaosambazwa na vijigazeti vya Jamvi la Habari na Tanzanite ni kazi ya 'watu wasiojulikana' wanaofamika vyema. Ni aibu kubwa kwa nchi yetu, kwa Jeshi la Polisi na kwa Serikali ya Magufuli.
 
Kila mtu anaeuliza au kuhoji kuhusu kufikiwa kwa Uchunguzi wa tukio la kushambuliwa mbunge wa JMT mheTundu lissu,
Au kuna mtu yeyote aliyetiwa kizuizini mpaka sasa kutokana na tukio hilo.

Huwa wanakuja na jibu jepesi tu eti kwa nini dereva wake amefichwa.

inachekesha hivi ata kama mkipewa dereva ndio mtajua wahusika wa lile tukio?

Kama tu hamjui ata majina ya walinzi ambao walitakiwa kuwa zamu siku ile hivi mkipewa huyo dereva ndio mtajua.?

Kama tu mmeshindwa kung'amua ata kwa kuhisi mtu aliyejitolea kutoa camera za cctv eneo lilipofanyika tukio ndio mna imani kwamba mkipewa dereva wa lissu basi na hizo CCTV zitaonekana .


Even mimi Zero Iq nimefikiria na kuona hiyo ni kama kuruka mkojo wako na kutaka kukanyaga mavi ya Rashidi je nyie wenye kutoa hilo jibu mtakuwa na Iq ya Aina gani?
 
Ila hawa jamaa wakati mwingine utafikiri intelijensia yao ni kama imexpai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…