Shamim Mwasha, mumewe mbaroni Dar kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya

Shamim Mwasha, mumewe mbaroni Dar kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya

Hii habari ya Shamin inashtua na inasikitisha; lakini tukumbuke haitoshi tu kutoa tuhuma ni lazima serikali iweze kuthibitisha pasipo chembe ya shaka. Ni rahisi zaidi kutuhumu kuliko kuthibitisha. Hata kusema "tumekuta" siyo ushahidi tosha. Tuache process itende kazi; ni matumaini yangu wana mawakili wazuri ambao watawapigania kwa haki. Siyo jukumu lao kuthibitisha hawakufanya; ni jukumu la serikali kuthibitisha kuwa walifanya.
mzee mwanakijiji kumbe wakati mwingine unahisihisi tu mambo ?? nilidhani kuna utofauti .nilikua nakosea sana.
 
Kuna uchawi wa Pete au wa kichupa (hapa mtu anaongelea kwenye Pete au chupa "nataka nisionekane kwa macho ya kibinadamu" hapo hawezi onekana mpaka atakapo iambia hiyo Pete au chupa "nataka kurudi kwenye hali ya ubinadamu") lkn,hiyo Pete au chupa mtu anapaswa kuilipia kila baada ya muda fulani (unamtoa mtu kafara)

God have mercy on us
 
Huyu dada aliolewa ndoa ya kwanza na mwanaume mmoja mstaarabu sana. Walibahatika kupata mtoto wa kike. Yeye ndiye chanzo cha ndoa kuvunjika.

Sasa mwana kulitafuta mwana kulipata.
Wale waliopeleka funguo za vibubu kwa shamimu kama nawaona walivyoishiwa pozi[emoji3][emoji3][emoji3] watavunja vibubu na shoka.
yaani hivyo vibubu mchakato ulikuaje
 
Mamlaka ya Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA) imemkamata mfanyabiashara, Abdul Nsebo maarufu Abdukandida na mkewe, Shamim Mwasha kwa tuhuma ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin.

Wanandoa hao wanadaiwa kukutwa na dawa hizo zenye uzito wa zaidi ya gramu 400 nyumbani kwao Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa operesheni wa DCEA, Luteni Kanali Fredrick Milanzi amelieleza Mwananchi kuwa, watuhumiwa hao walikamatwa Mei Mosi mwaka huu.

Amesema kukamatwa kwa Nsebo na mkewe kumekuja baada ya kukamatwa kwa mtandao mkubwa wa dawa hizo hivi karibuni.

Amesema maofisa wa DCEA baada ya kupata taarifa walienda nyumbani kwa watuhumiwa hao na kufanya upekuzi na kubaini mfuko ukiwa na dawa hizo za kulevya na nyingine zilikutwa katika siti ya nyuma ya gari.

"Tulifanya upekuzi kuanzia saa 8:00 usiku hadi saa 1:00 asubuhi na tulizibaini dawa hizo zikiwa zimefichwa na matokeo ya awali kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali yameonyesha ni dawa za kulevya aina ya heroin.”

“Vitu vingine tulivyomkuta navyo ni simu tano, kadi za benki, hati ya kusafiria pamoja na nyaraka mbalimbali ambavyo vyote tumevichukua,” amesema Luteni Kanali Milanzi

Amesema watuhumiwa hao wana mtandao mkubwa wa kimataifa na kwamba wana majina ya watu wanaoshirikiana nao kutoka nchi mbalimbali ikiwamo Brazil.

Amesema wawili hao bado wanashikiliwa na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.
Wangewakatia fungu nene mngewashika?
 
Mange anasema Shamim aliingia mjini na lorry la mkaa akitokea Morogoro 😂
Aende uko uyo Mange kimavi,Shamim mwasha siyo kinyonge kwao toka miaka hiyo,Mzee mwasha ana bucha kadhaa za nyama miaka ya 90
 
Back
Top Bottom