Shamsa Ford asema mahari yake ni Milioni 20

Shamsa Ford asema mahari yake ni Milioni 20

View attachment 1262973
Muigizaji wa Filamu Tanzania Shamsa Ford

Muigizaji wa Filamu Tanzania Shamsa Ford, amesema kutokana na uzuri alionao, anaamini mwanaume anayetaka kumuoa kwa sasa anapaswa kutoa mahari ya shilingi Milioni 20.

Shamsa Ford ametoa kauli hiyo katika kipindi cha KIKAANGONI, kinachorushwa kila siku ya Jumatano katika kurasa za Facebook na YouTube za East Africa TV, ambapo amesema kwa mwanaume anayetaka kumuoa aende na gari lililoandikwa 'Will You Marry Me'.

Shamsa Ford amesema kuwa "mtu akitaka kunioa sasa hivi, naangalia kwanza mfuko wake ukoja ila ninachotaka mimi siku ya kwanza kuja kunipa ombi la kunioa aje na gari lililoandikwa Will You Marry Me,"

"Unajua mimi ni ninastahili mahari zaidi ya Milioni 10 au Milioni 20 kwa sababu mimi ni mzuri, na mtu akinipata mimi maana yake amepata mtu mwenye vigezo vya kuwa mke bora, najua kupika najua kulea familia." amesema Shamsa Ford.

Aidha katika kipindi hicho Shamsa Ford, amesema hakumbuki chochote kwa aliyekuwa mume wake Chid Mapenzi wakati wakiwa kwenye mahusiano, bali anayemkumbuka ni Msanii Ney wa Mitego ambaye alikuwa na tabia ya kununa kwenye mahusiano.

Chanzo: EATV
Kuna magari yanaitwa used. Hili overused. Linafaa kuwa spare tu.
 
Naamini hakuwa serious Tanzania hii utolewe mahari 20 labla mtoto wa Dangote.
Hahahah wa Dangote ili kumu impress mzee lazma uende na 100M kuonesha kwamba upo on de right traki!

Mzee anakwambia toa matumizi ya kiwanda cha Dangote Cement ya siku moja tu kama mahari ya binti. Ukimbwela umemkosa
 
Fanya mpango uniwowe kwa tu million 30 😁😁
 
Ng'onda ndiyo nini jamani mmeniacha njia panda
 
wanaume mbona mnakuwa na Negative mindset kiasi hicho, yaani mtu kusema mahali yake binafsi akili zenu zinaishia kuwaza upuuzi. Ndio maana hilo taifa baadhi ya vijana wana maisha magumu washalaaniwa tayari kwa kufanya vitu vya ajabu.
Naona binti umekuja moto sana huku jf, emu kitulize basis,
Muwasho wa mini?

Umejiunga huku juzi tu Leo unatolea mapovu wanaume, kuwa makini.
 
Huyu demu namkubali hasa Tangu kwenye movie ya bado natafuta
Kama ningekuwa nayo MIL 20 ningemtafuta nijimilikishe na ningemuongeza 10m za juu,
Ananivutia sana.
 
Huyo mbona thamani yake ni laki 2 na blanket moja

Na kwenye hiyo lakimbili nimejumlisha mpaka ela ya kumpa mshenga. Ukiichenjua chenjua hapo bint anatoka na laki na usheenzi . Si pesa ndogo bado
 
Then Ethics za kazi yake hazijui. Hlafu kwa akili yako ya kujiongeza shosti huyo anaweza kuwa dakatri kweli??
hivi kwa akili yako unaweza kumtambua mtu mwenye id fake huku JF, inawezekana ni daktari kweli .
kwa taarifa yako huku kuna madaktari hadi maprofesa wanakuja na id fake
 
Kasoro mimi pekee ndiye niliyesalia kutolaaniwa, ebu wahi haraka pm tuyajenge Mama [emoji87]
wanaume mbona mnakuwa na Negative mindset kiasi hicho, yaani mtu kusema mahali yake binafsi akili zenu zinaishia kuwaza upuuzi. Ndio maana hilo taifa baadhi ya vijana wana maisha magumu washalaaniwa tayari kwa kufanya vitu vya ajabu.
 
Kuna watu hata bure sioi, huo unene nipeleke wapi? napenda wanawake wanaoenda gym wana afya sio big mamas. Sorry watanzania mimi sijui hiyo tabia yenu ya kupenda watu wenye obesity imetoka wapi.

Alafu kitu sitokuja kutoa hadi nakufa ni mahari, kama it means sitooa Tanzania then so be it, mwanamke tumependana tunafunga ndoa alafu natoa hela kumnunua? what the f? traditions za kishenzi bado tunaendelea kuzikumbatia hadi leo, ndiyo sababu hizi watu wa zamani walikua wanapenda kuzaa mabinti alafu wanawauza utotoni, slavery made this sh*t na we still practice it until today.
 
Twenty MILLIONS😳😳!!!!!!
......ina DREAM LINER ndani??????? Au ni SACCOSS!!!??
 
wanaume mbona mnakuwa na Negative mindset kiasi hicho, yaani mtu kusema mahali yake binafsi akili zenu zinaishia kuwaza upuuzi. Ndio maana hilo taifa baadhi ya vijana wana maisha magumu washalaaniwa tayari kwa kufanya vitu vya ajabu.
We mahali yako shingapi nijitose?
 
Back
Top Bottom