Kwani uchungu una upimaje?
Ulitaka muda wote atoe machozi?
Alie huku anagala gala?
Au ulitaka azimie ndio useme kaguswa na msiba?
Mbona mnakuwa waswahili nyinyi,nyinyi ndio wale baada ya msiba nmnaanza kwenda kwa mganga kwenda kupiga bao kujua kama ndugu yako kafa kweli au msukule,ndio kwa akili zenu watu kama nyinyi Gwajima aliwageuza mtaji wa kupiga hela na kutengeneza brand la kanisa lake.
Hivi hushaudhuriaga misiba ambayo wafiwa wanapiga bia muda wote,hawa nao mtasemaje?
Kama hujui kuna wengine uchungu wa Msiba unaanza baada ya kuzika na kuna wengine wapo cool,ila ndani ya vifua vyao kuna maumivu ya uchungu husio pimika.
Yaani mtu kushika simu ndio mnashangaa,mimi jana jamaa yangu kazika baba yake Kigamboni muda alikuwa na simu anachat na sisi na yy ndiye aliye tuelekeza msibani na michango tumemtumia kwenye simu.
Huu uhuru tuliopewa na JF tusiutumie kuwadhalilisha au kuwaumiza wengine kihisia,kisa sababu ya hisia zako za kijinga.
Nyie mlitaka Babutale aomboleze vipi?