Binafsi nitakuwa wa mwisho kuamini Tale anaweza kumuua mke wake... the guy loved his wife for real though hiyo haiwezi kuwa excuse! Ninachoamini, kuua/kupoteza mke si jambo dogo! Mtu anaweza kupata wazimu wa kuua mtoto kuliko mke!
Kuhusu Wabongo na ushirikina, niligundua hili jambo years back... nilipata tatizo ambalo lilinitoa kabisa kwenye reli!
Ajabu, hata Washikaji ambao sikuwahi kabisa kuwadhania, na wenyewe wakawa wananishauri niende kwa Waganga!
Ukirudi kwa ndugu, na sie Waswahili tuishio Uswahilini ndo taabu tupu!!
Mtu ambae aliniweza, alikuwa ni my ex! Kwanza huyu alikuwa very supportive kwenye mitihani niliyokuwa nimekumbana nayo! On top of that, she's dah... very decent and humble to the point nilishindwa kabisa kumkatalia!
Sasa kuna siku akaja home akasema kuna Sheikh keshamlipa, na huyo Sheikh aliwahi kumsaidia kakake; kwahiyo niende tu Sheikh atafanya mambo!!!
Sipendi kuwa mnafiki; ingawaje mimi ni Mwislamu but I don't trust these so-called Sheikhs wakiongeza uganga kwenye CV zao! Sasa nikawa njia panada, huyu my ex- ni very supportive, na mbaya zaidi keshamlipa the so called Sheikh... what should I do!
Nikaamua kwenda kwa sababu kuu 2, mosi the girl ni Mkatoliki Damu, na pili nikaamini inawezekana akawa Sheikh kweli kwa sababu niliamini there's no way huyu mrembo angenipeleka kwa mganga!
Kufika kwa sheikh sasa... advertize ya kwanza kuna madrasa! Nikapata nguvu! Later on akaleta vijana wake pale wakajifanya kusomasoma, walipokuja kuniboa, muda nataka kuondoka nikapewa kidumu cha lita 5, ndani sijui kuna madudu gani sijui... eti nikaoge kwa siku 7!
Nikajua hawa ndo wale wale!!!
Sasa nikikumbuka kile kipindi, kila unayekutana nae, hakuna cha maana anachokuambia "...kule kuna mzee fulani!" "Mkuranga, kuna bibi fulani!" Kuna mshikaji alishawahi kunilipia hadi nauli eti niende Tanga!!!!
Tukirudi kwa Tale, kingine kinachomsumbua ni shule! Kichwa kikiwa cheupe unaropoka chochote bila kujali consquences zake hapo baadae ingawaje uropokaji na wenyewe kwa wengine ni kipaji cha kuzaliwa nacho!!
Matokeo yake, ndo kama ulivyosema, hivi unaepukaje tuhuma za ushirikina wakati amekuwa akiongea hata mwenyewe hadharani!!