Shangaa Serikali inavyoangaika sana na wachuuzi kuwatafutia mikopo wabaki mjini huku mamia ya vijana wakisota na ukame na hawana fidia

Shangaa Serikali inavyoangaika sana na wachuuzi kuwatafutia mikopo wabaki mjini huku mamia ya vijana wakisota na ukame na hawana fidia

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145
Wana Jf,

Serikali kama kawaida ya kupendelea mafundi kama haijui, wale walio kijijini ndio wapiga kura aswa kuliko hawa wachuuzi wa mjini. Serikali ipo radhi kuona nchi inakabiliwa na ukame mkubwa na wakulima vijana hawapati fidia ya vitu walivyovipoteza wakati wanapambania maisha yao na ya wale wanaoishi mjini. Serikali imetoa mabilion ya pesa kuwapoza machinga, lakini haijui matunda kama maembe, nyanya, vitunguu, na miwa inayouuzwa na wachuuzi hawa inatoka kwa wakulima ambao hawana mikopo na wanakabiliwa na ukame.

Ni wakati sasa kuwaondoa wauza soksi na vitambaa kuwapa mbinu bora ya kupambana na kilimo cha umwagiliaji au cha misimu huko ndiko kuna ajira kubwa. Kwa sasa mambo yote yaliyokuwa yanakosekana kijijini sasa yapo. Hakuna haja ya kuja mjini kuchagua miji kama hakuna malengo na biashara dhabiti.

Nashauri fedha hizi isiwape wazikopeshe wakulima kwani wakulima wengi wanaangaishwa na mabenk eti hawatimii vigezo na mashart.
 
maisha ndivyo yalivyo komaa tu ndugu
 
mkuu km unataka fidia ya mazao yako basi ukayakatie bima, au km unaona machinga wanapendelewa acha kulima ukawe machinga
 
Back
Top Bottom