Shareholder mkubwa wa NMB ameondoka – Rabobank Nederland

Hio bank inabebwa na mishahara ya watumishi kupitia kule bila hivyo ingeshafilisika
Du. Hivi mtumishi wa serikali hawezi kutaka mshahara wake upitishwe benki nyingine? eg Kama anaona CRDB au benki nyingine yoyote ndiyo inakidhi viwango vyake na akaamua kufungua account huko ina maana mshahara hauwezi kupitia huko?
 
pamoja na taarifa kuwa ya hisia tuu bila kuwa na hakika lakini ukweli ni kwamba serikali haiwezi kuendesha bank hii na ikasurvive kabisa uko ni kujidanganya kabisa bali hii bank itakufa.
serikali haiwezi kuendesha hii bank kuna mambo mengi imeshindwa kwa hiyo isipambane kuendesha hii bank itakufa
 
Sirikali ina watalaamu wa kutosha kuendesha benki yeyote, acha mabeberu waondoke zao au nasema uongo ndugu zangu.
 
Mkuu- kwenye mada umesema mwenye hisa mkubwa ameondoka- katika ulimwengu wa mahisiano ya kihisa mbona hujaeleweka na haileti maana yoyote zaidi ya kuleta taharuki isiyo na maana.
 
kwa nini benki zetu za ndani hazijaweza kujitanua nje kama benki za kigeni zilvyoweza, benki ya wakenya equity benki imejitanua sana tanzania, lakini cha ajabu kenya hakuna benki ya tanzania iliyoweza kujitanua.
 
Zimbabwe ya Mugabe hiyooo inakuja Tanzania.
 
Utekaji

Uuaji

Wizi wa kura

Ukabila

NDIO KUMTEGEMEA MUNGU???
 
Redemption of shares sidhani kama itakuwa na positive result hasa kwenye hii bank ambayo serikali ina hold Major shares
 
we need to get more serious linapokuja suala la financial services industry. Hatuwezi kuwa wajinga na kukubali upuuzi wa MATAGA kutaka kila njia ya uchumi imilikiwe na serikali.
Umeandika vizuri sana mkuu. Blessings

Hawa mataga wanafikiri tumesahau jinsi walivyoiua NBC enzi hizo kwa chuchota fedha kwa miradi yao ya pwagu na pwaguzi kule Msimbazi ikiendeshwa na watu wao waliokuwa mambumbumbu pale SUKITA!!

Serikali si inamiliki Tanzania Postal Bank, tuone kama safari hihi wataweza!!!

Naamini kabisa kuwa serikali hawana ujuzi wa biashara kwani biashara ina miiko yake ambayo sio rahisi wao kuifuata!! Mfano ni jinsi ya kuthibiti matumizi, serikali mara nyingi wanajua kutumia fedha bila kuwa makini kwasababu ya political considerations.
 
Hili ni tatizo la siku nyingi sana.

Kuna Mzee wangu mmoja alikuwa mkubwa Bima. Siku moja tumekaa akawa ananipa stories za enzi zake kazini.

Anasema kuna mwaka Katibu Mkuu wa CCM alimfuata kuomba mkopo. Mkopo mkubwa tu.

Basi yule Mzee akamwambia sawa, fomu hizi hapa utajaza, tutataka kujua mnaweka collateral nini, mnataka mkopo wa muda gani na detail zote.

Kawawa akamwambia habari za collateral usijali, sisi tunakopa kwa integrity ya jina la Chama Cha Mapinduzi na Serikali ya Tanzania.

Yule Mzee akawa anaona hapa mbona mambo mapya haya? Akamwambia Kawawa hilo halitawezekana.

Kawawa akamwambia, "kijana, hivi unajua sisi ndio tuliofanya hii kampuni ikawepo hapa?"

Basi yule Mzee akaona kama katishwa, akampelekea issue bosi wake.Bosi akapitisha mkopo.

Siku kibao zikapita, yule Mzee ikabidi afuatilie malipo ya mkopo, maana Kawawa/CCM walikuwa hawalipi.

Ikawa kazi sana kumpata Kawawa. Kila akimtafuta hampati. Kila akimtafuta hampati.

Mwishowe akampata. Akamsalimia, akamwambia Muheshimiwa nafuatilia ule mkopo, naona malipo hayafanywi.

Kawawa akamjibu akamwambia "Kijana, hivi hapo Bima mna "bad loans ledger"?

Akajibiwa lipo.

Kawawa akamwambia basi huu mkopo uweke katika hiyo "bad loand ledger" tuumalize hivyo.

Na hapo ndipo mkopo ulipoishia.

Vitu kama hivi vinaendelea mpaka leo, hata kama si blatantly hivyo.
 

Rabobank has lodged a share transfer request for its stake in NMB Bank Plc​

NMB Bank’s largest shareholder, Rabobank of the Netherlands, has partnered with the Dutch Development Bank (FMO) and the Norwegian State owned development fund (Norfund) to form a Sub-Saharan Africa-focused investment company, Arise. The partnership was officially launched in Cape Town, South Africa in February 2017.
The ambition of the partnership is to build strong, locally owned financial institutions that serve small and medium enterprises (SMEs), the rural sector, and clients who have not previously had access to financial services.
Rabobank, FMO and Norfund have each in their individual capacities been successful in the development of the financial sector in Africa. Through Arise, the partners aim to continue to adequately support the growth and advancement of financial institutions by proactively providing among other things, technical assistance and management services in the fields of governance, management, marketing, innovation, compliance and risk management.
To achieve their goal, members of the partnership agreed to pool together their networks, expertise and assets, including the stakes they individually held in several financial institutions in Sub-Saharan Africa (SSA). For Rabobank, this represents its shareholding in a number of financial institutions in SSA including NMB Bank Plc (NMB).
The transfer of Rabobank’s shares in NMB to Arise is subject to regulatory approvals both at shareholder level as well as at the various national levels. Rabobank has lodged its share transfer request at the Ministry of Finance (MOF), the Bank of Tanzania (BOT) and the Capital Markets and Securities Authority (CMSA).
NMB will provide an update of the proceedings upon the receipt of responses from the regulatory bodies.

SIJUI TATIZO NI UGUMU WA KUTAFSIRI AMA VIPI, LAKINI HIYO JUU NDIO TAARIFA RASMI YA RABOBANK KWENYE WEBSITE YAO RASMI.​

 
hahahahahaha ukifwata post bila kuwa na info utaumia....... fuatilieni arise bv ninani na inamiliki nini

VIVA MAGUFULI
Kwa hiyo post za tetesi hazitakiwi kujadiliwa JF?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…