Shareholder mkubwa wa NMB ameondoka – Rabobank Nederland

Shareholder mkubwa wa NMB ameondoka – Rabobank Nederland

Good! Bring the feedback.

Nimecheka kwa nguvu, feedback ya nini tena wakati kila mtu unataka aingie mwenyewe kwenye hiyo website? Mimi nilimuomba yule mdau updates, ww ukasema nangoja nini nisiingie kwenye web yao? Au unajichanganya?
 
Rabobank wamehamisha hisa zao kwenda Arise B.V (Hisa 174,500,000).

Hawa Arise ni ushirika wa uwekezaji ambao wapo Norfund ( mfuko wa maendeleo wa Norway,benki ya maendeleo ya uholanzi pamoja na Rabobank.

Kimsingi Rabobank bado yumo,sema staili aliyoitumia hii nadhani ameona something wrong somewhere..

Ngoja tuichimbe hii taarifa tujue motive behind.
 
Bahati nzuri mimi ni mtu mzima. Nimekuelewa.

Na kwakuwa mimi ni mtu nusu ndio maana nilikujibu nimeshaingia, nilijua 100% lazima uniulize nimeona nini. Na kweli ndio ulichouliza, na jibu lako nilikuwa nalo. Umeuza cheni fake, umelipwa hela fake. Shubamiit.
 
Yalikuwa mafisadi....... Ndio maana yamekimbia, kwani UONGO ndugu zangu?
 
Wewe ni kilaza sawa na vilaza wengine. Dodd Frank haikuja kutokana na Global Financial Crisis ya 2008. Hebu annika vizuri mpaka mwaka wa hiyo Act. Usitudanganye.

Ni sahihi Dodd Frank ilikuja kwasababu ya finacial Crisis ya 2008-- TOO BIG TO FAIL!!
 
Umesahau kuwa jinsi dunia ilivyokuwa ina run 1980 ni tofauti na 2020 , dunia ya Leo tunategemeana mno. Ndio maana hamna nchi iliyoendelea kwa kutegemea wawekezaji wa ndani pekee.

By the way nje ya mada ivi ni nchi gani iliyotuletea mahindi ya njano kipindi like tuna njaa Kali miaka ya '80'?
"Dunia ya leo tunategemeana mno. Ndio maana hamna nchi iliyoendelea kwa kutegemea wawekezaji wa ndani pekee."

Kwa hiyo zamani wakati nchi hazitegemeani hakuna nchi ilyoendelea?
 

Rabobank has lodged a share transfer request for its stake in NMB Bank Plc​

NMB Bank’s largest shareholder, Rabobank of the Netherlands, has partnered with the Dutch Development Bank (FMO) and the Norwegian State owned development fund (Norfund) to form a Sub-Saharan Africa-focused investment company, Arise .

The partnership was officially launched in Cape Town, South Africa in February 2017.
The ambition of the partnership is to build strong, locally owned financial institutions that serve small and medium enterprises (SMEs), the rural sector, and clients who have not previously had access to financial services.

Rabobank, FMO and Norfund have each in their individual capacities been successful in the development of the financial sector in Africa. Through Arise, the partners aim to continue to adequately support the growth and advancement of financial institutions by proactively providing among other things, technical assistance and management services in the fields of governance, management, marketing, innovation, compliance and risk management.

To achieve their goal, members of the partnership agreed to pool together their networks, expertise and assets, including the stakes they individually held in several financial institutions in Sub-Saharan Africa (SSA). For Rabobank, this represents its shareholding in a number of financial institutions in SSA including NMB Bank Plc (NMB).

The transfer of Rabobank’s shares in NMB to Arise is subject to regulatory approvals both at shareholder level as well as at the various national levels. Rabobank has lodged its share transfer request at the Ministry of Finance (MOF), the Bank of Tanzania (BOT) and the Capital Markets and Securities Authority (CMSA).

NMB will provide an update of the proceedings upon the receipt of responses from the regulatory bodies.

For enquiries contact:

Joseline Kamuhanda,
Senior Manager Corporate Affairs and Public Relations
Email: Joseline.kamuhanda@nmbtz.com

Anna Mwasha,
Strategy & Investor Relations Manager
Ahsante kwa Taarifa
 
An economy dictated by a Ukase must nosedive!
 
Hili ni tatizo la siku nyingi sana.

Kuna Mzee wangu mmoja alikuwa mkubwa Bima. Siku moja tumekaa akawa ananipa stories za enzi zake kazini.

Anasema kuna mwaka Katibu Mkuu wa CCM alimfuata kuomba mkopo. Mkopo mkubwa tu.

Basi yule Mzee akamwambia sawa, fomu hizi hapa utajaza, tutataka kujua mnaweka collateral nini, mnataka mkopo wa muda gani na detail zote.

Kawawa akamwambia habari za collateral usijali, sisi tunakopa kwa integrity ya jina la Chama Cha Mapinduzi na Serikali ya Tanzania.

Yule Mzee akawa anaona hapa mbona mambo mapya haya? Akamwambia Kawawa hilo halitawezekana.

Kawawa akamwambia, "kijana, hivi unajua sisi ndio tuliofanya hii kampuni ikawepo hapa?"

Basi yule Mzee akaona kama katishwa, akampelekea issue bosi wake.Bosi akapitisha mkopo.

Siku kibao zikapita, yule Mzee ikabidi afuatilie malipo ya mkopo, maana Kawawa/CCM walikuwa hawalipi.

Ikawa kazi sana kumpata Kawawa. Kila akimtafuta hampati. Kila akimtafuta hampati.

Mwishowe akampata. Akamsalimia, akamwambia Muheshimiwa nafuatilia ule mkopo, naona malipo hayafanywi.

Kawawa akamjibu akamwambia "Kijana, hivi hapo Bima mna "bad loans ledger"?

Akajibiwa lipo.

Kawawa akamwambia basi huu mkopo uweke katika hiyo "bad loand ledger" tuumalize hivyo.

Na hapo ndipo mkopo ulipoishia.

Vitu kama hivi vinaendelea mpaka leo, hata kama si blatantly hivyo.

Mimi nikiwa mfanyakazi wa NBC enzi hizo nilikuwa shahidi kabisa wa vitendo vya chama tawala kuifilisi benki ya biashara ya Taifa yaani NBC!!

Ilikuwa Hivi; ccm walivyotaka kuchukua fecha toka NBC walishinikiza serikali kumteua mweka hazina wao enzi hizo Marehemu Paul Bomani kuwa mwenyekiti wa bodi wa benki. Sukita ambalo ndio lilikuwa shirika la schumi la chama tawala ,walileta maombi ya mkopo wa mabilioni ya shilingi kutekeleza miradi yao ya kufuga nguruwe kule bonde la Msimbazi. Katika majadiliano ya wajumbe kuhusu maombi yale ;mjumbe mmoja msomi aliuliza kuhusu dhamana iliyokuwa inawekwa kuhusiana na ule mkopo ambayo, haikuwepo!! Mjumbe msomi hakuafiki kutolewa kwa ule mkopo na kilichotokea baada ya yule mjumbe kupinga ni kuondolewa kama Mjumbe wa bodi ya NBC , baada ya hapo mkopo ukaidhinishwa!!!! Hivyo ndivyo wanavyotaka control ya benki ili wachote mapesa watakavyo.
 
Mimi nikawa mfanyakazi wa NBC enzi hizo nilikuwa shahidi kabisa wa vitendo vya chama tawala kuifilisi benki ya biashara ya Taifa yaani NBC!!

Ilikuwa Hivi; ccm walivyotaka kuchukua fecha toka NBC walishinikiza serikali kumteua mweka hazina wao enzi hizo Marehemu Paul Bomani kuwa mwenyekiti wa bodi wa benki. Sukita ambalo ndio lilikuwa shirika la schumi la chama tawala ,walileta maombi ya mkopo wa mabilioni ya shilingi kutekeleza miradi yao ya kufuga nguruwe kule bonde la Msimbazi. Katika majadiliano ya wajumbe kuhusu maombi yale ;mjumbe mmoja msomi aliuliza kuhusu dhamana iliyokuwa inawekwa kuhusiana na ule mkopo ambayo, haikuwepo!! Mjumbe msomi hakuafiki kutolewa kwa ule mkopo na kilichotokea baada ya yule mjumbe kupinga ni kuondolewa kama Mjumbe wa bodi ya NBC!!!! Hivyo ndivyo wanavyotaka control ya benki ili wachote mapesa watakavyo.
Nashukuru ume corroborate mfano wangu.

Inaoneana haya mambo yamefanyika sana, na bado yanafanyika mpaka sasa.

Ila yanayofanyika sasa kuja kuyasikia vizuri itakuwa baadaye sana kama sasa hivi tunavyoongelea ya kina Bomani na Kawawa.
 
"Dunia ya leo tunategemeana mno. Ndio maana hamna nchi iliyoendelea kwa kutegemea wawekezaji wa ndani pekee."

Kwa hiyo zamani wakati nchi hazitegemeani hakuna nchi ilyoendelea?
Tatizo lako bado Una mawazo ya kijima ya mwaka 80, hauwezi kunielewa.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Anataka kuleta ujamaa kwenye ulimwengu wa Sasa wa economic integration huwezi endelea bila kuliwa
Integration my foot.

UK imejitoa kwenye ma integration hasara ya EU.

Kujiondoa hao wageni kutoka kwenye umiliki wa the biggest banking conglomerate is welcome news.
 
Ifike mahali tuwe wakweli, hali inazidi kuwa mbaya Sana mtaani.

Vitu vinapanda bei vibaya mno.

Mo poa 9,000-9,500
Mo extra 5,000-5,500
B 29 25,000-27,000
Mafuta ya kula 18 lts 56,000-74,000
Ngano 29000- 30,000
Kreti la soda 9,800 - 10,000

Hiyo Ni kwa mjibu wa eneo nilipo
 
Back
Top Bottom