TANZIA Sharo Millionea afariki dunia

TANZIA Sharo Millionea afariki dunia

R.I.P Shalo Millionea, yale matangazo ya Airtel na Mzee Majuto wameyatendea mema, watoto wanayapenda sana, hata mwanangu km analia akisikia moja kati ya yale matangazo basi anaahirisha kulia, anyway njia toka Segera hadi Tanga nyakati za usiku ni mbaya sana, ina kona nyingi na malori ukikutana nayo huwa yanawasha full light so yawezekana kilichowakuta timu ya prisons ndicho kilichmkuta Shalo na kwa Harrier na mwendo wake basi ikawa hivyo. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI.
Ni kweli mkuu, Alikuwa ni kipenz cha watoto... kaacha pengo kwao! RIP Sharo!
 
Ridhiwani hakawii kuunda kamati ya maandalizi ya msiba,
Chonde chonde hiyo kamati isiingilie maamuzi ya famila yao
pia JK inabidi awahi msibani kama kwa Kanumba
 
Nikifika nitapata,
Uzima kwa Yesu,
Ninamtolea Moyo wangu,
Nife kwa furaha!

Aaaaaammmmmeeeeennnniiiii!

Bwana ametoa, na Bwana ametwaa, jina la Bwana libarikiwe.
 
Raha ya milele umpe eeh bwana, apumzike kwa amani. Amina.
 
Mungu ailaze roho yake pema. I hope atapokelewa vema na St. Peter katika Pearly Gates.
 
Tumwombee ni kijana mzuri alikuja tofauti mm na familia yangu tunampenda sana nasikitika kaitwa mapema, swaga zake kafanazo majuto kabaki pekeyake tuzidi kumwombea.
 
Maisha ni kutafuta na sio kutafutana meeen! - Sharo Millionea.

R.I.P Broda. Umetangulia sie tupo njiani.
 
Mungu wa ajabu,kweli kila mtu ana siku yake

kamchukua young boy,king majuto aliekula chumvi kias chake bado anadunda tuh

maisha ndivo yalivo
 
R.I.P Sharo. Poleni Wasanii hasa Mzee Majuto kuwa msatahamilivu katika kipindi hiki kigumu. Ukweli jamaa alianza kupanda chati kwa vichekesho vyake,misemo yake na miondoko yake. Alivutia sana watoto.
 
R.I.P Sharo

Duh aisee sina cha kusema kiukweli imetuumiza wengi amefanyika msaada wakati wa majonzi kwangu kupitia kanda zake za vichekesho,Mungu aitunze familia yake na zaidi mapenz yake ya timie wanadam hatuna jinsi...Rest In Peace sharo millionair!we stil lov u
 
There are currently 742 users browsing this thread. (73 members and 669 guests)

Hoya Nyie Guests Mnatuyeyusha Jiungeni Bwana!!!!!
 
Back
Top Bottom