Shehe mkuu wa Mkoa wa Mtwara ndani ya tamasha la ‘Muziki Mnene’

Shehe mkuu wa Mkoa wa Mtwara ndani ya tamasha la ‘Muziki Mnene’

Boss la DP World

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
2,318
Reaction score
8,464
Naona shehe mkuu wa mkoa wa Mtwara ameenda kwenye tamasha la Muziki Mnene lililo waleta wasanii wa muziki wa kizazi kipya mkoani Mtwara.

Hongera ndugu zangu waislamu kwa kukubali kushiriki kwenye tamasha hili la Muziki wa Bongo fleva na Singeli.

Pia niwapongeze waumini wenu kama Naseeb Abdul (Diamond), Ali Kiba, Dula Makabila, Konde Boy, Zuchu, Mwana FA, MWIJAKU, Babu Tale na wengine wengi kwa kuendeleza gemu.
IMG_20220723_143352.jpg

IMG_20220723_144153.jpg

Aliyekaa kulia kabisa
IMG_20220723_144148.jpg
IMG_20220723_143655.jpg
 
Aiseeee.......

Kwa kuwa muislam mmoja kiongozi kahudhuria basi hongera tunapewa waislamu wote? Unadhani ni sawa ulichoandika, hebu tumia tu akili yako ya kuvukia barabara kuwaza kama upo sahihi?

Nadhani Muslims wajifunze kuchagua viongozi walioshika dini kweli na sio waliojificha kwenye kivuli cha dini. Muislam aliyeshika dini anafahamu kuwa muziki kwake ni Haram na atajitenga nao.

Mwisho kabisa mleta Uzi, usichanganye Dini iwe uislam au ukristo na tabia binafsi za mtu.

Ingefaa kama ungeshangaa kiongozi kama huyu imekuwaje ahudhurie hapo.

Hata hivyo viongozi wengi wa Bakwata sio wote huwekwa kwa maslahi ya kiserikali zaidi sio ya Dini ndio maana kuna baadhi ya Muslim hawaamini hiki chombo cha bakwata.
 
Nchi hii ndicho kilichobakia
Watu kwenda kwenye matamasha
Tu...kila leo matamasha tu
Sijui mara msanii huyu mara yule
Nendeni tu lakini mkapoteze mawazo

Ova
 
Kongole Shehe , wahafidhina wasio jua tafsiri ya maandiko na hekma watakushangaa, lakini wasomi na watu waliojaliwa busara ya kumjua Mungu wa kweli watakuelewa kuwa, kuwasubiri vijana misikitini pekee ili uwe karibu nao uwahubirie wa adilike sio rahisi kwa karne ya sasa hivyo, unahitaji kujishusha na kuwafuata huko huko ili wakuzoee na wakuone ni mmoja kati yao ndipo utaweza kuongea nao maneno ya Mungu na kuwabadilisha

Hata hivyo, unapokuwa kwenye nafasi kubwa kama hiyo ya kimkoa SHEHE MKUU unakuwa sii kiongozi wa lile kundi unaloongoza tu bali umeingia kwenye URIKA WA VIONGOZI WA KIJAMII na kwenye matukio ambayo yanakusanya watu wengi na viongozi wengine wa kiserikali na kijamii wapo na wewe unatakiwa kuwepo kwa lile lengo la kuleta umoja wa nchi👏👏👏👏
 
Aiseeee.......

Kwa kuwa muislam mmoja kiongozi kahudhuria basi hongera tunapewa waislamu wote? Unadhani ni sawa ulichoandika, hebu tumia tu akili yako ya kuvukia barabara kuwaza kama upo sahihi?

Nadhani Muslims wajifunze kuchagua viongozi walioshika dini kweli na sio waliojificha kwenye kivuli cha dini. Muislam aliyeshika dini anafahamu kuwa muziki kwake ni Haram na atajitenga nao.

Mwisho kabisa mleta Uzi, usichanganye Dini iwe uislam au ukristo na tabia binafsi za mtu.

Ingefaa kama ungeshangaa kiongozi kama huyu imekuwaje ahudhurie hapo.

Hata hivyo viongozi wengi wa Bakwata sio wote huwekwa kwa maslahi ya kiserikali zaidi sio ya Dini ndio maana kuna baadhi ya Muslim hawaamini hiki chombo cha bakwata.
Yeye ni kiongozi wenu, pia tamasha limejaa waumini huoni vibaragashia na hijabu vimetawala shehe?
 
Back
Top Bottom