Shehe Mwinyi mdogo ameamua kuifanya Zenj emirate au sheikdoom?

Kwani Shida iko wapi? Uislam umefanya Arab Yote imekuwa tajiri ikiwemo super power Iran
 
Eeh kumbe makubwa Sana Sisi hatuna habari?
 
Mwalimu anasema sababu za kuungana ni pamoja na .

"Zanzibar ilikuwa kitovu cha Utumwa na Ukabaila wa kiarabu Africa Mashariki"

Jk Nyerere
 
Sasa papa si ndiyo alianzisha hiyo kalenda,papa ni mkuu wa kanisa
Hiyo kalenda ya kiislam haipo kwenye Quran,kuna watu walianzisha,lakini inaitwa ya kiislam na imekuumiza Zanzibar kuisherehekea
Kama ambavyo namba za Kiarabu, Arab numerals 0, 1, 2, 3 etc (ambazo zilitokea India na kuenezwa na Waarabu) hazimaanishi kwamba kila anayezitumia ni Mwislamu, vivyo hivyo Kalenda ya Gregorian, licha ya kuwa ilianzishwa na kiongozi wa Kanisa Katoliki, haimaanishi kwamba kila anayeitumia ni Mkristo. Asili ya kitu na matumizi yake ya sasa ni mambo mawili tofauti... kalenda na namba hizo zimekuwa mifumo ya kimataifa inayotumiwa na watu wa dini mbalimbali na hata wasiokuwa na dini.
 
Kwani Shida iko wapi? Uislam umefanya Arab Yote imekuwa tajiri ikiwemo super power Iran
Shida ipo kubwa. Kipande hiki cha ardhi kimezaliwa watu wenye dini mbalimbali. Hakuna dini moja inayoweza kuchukua hatimiliki ya hiki kipande cha ardhi. Tunaweza kuishi pamoja kwa upendo kila mtu akiabudu akionacho bora kwake ilimradi asimuudhi mwenzake.
 
Sasa papa si ndiyo alianzisha hiyo kalenda,papa ni mkuu wa kanisa
Hiyo kalenda ya kiislam haipo kwenye Quran,kuna watu walianzisha,lakini inaitwa ya kiislam na imekuumiza Zanzibar kuisherehekea
Papa Hakuianzisha hii calendar ila alifanya marekebisho Kwa ile iliyokuwepo kama scholar mwingine tu, upapa wake haikuifanya calendar kuwa jambo la kiimani na hii iliyopo si kamilifu Ina mapungufu Bado , atatokea scholar mwingine ataidevelop zaidi Anaweza kuwa muislamu( kwasababu inatagemea uchunguzi wa kisayansi na si Imani). Lakini haiuhusiani na Imani Wala hakuna Ibada yoyote ya pekee katika Kanisa eti kusheherekea January mosi hakuna.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…