Sheikh Alhad Musa Salum: Rangi ya Kijani inayotumiwa na CCM ndio rangi pekee iliyobarikiwa na Mwenyezi Mungu

Sheikh Alhad Musa Salum: Rangi ya Kijani inayotumiwa na CCM ndio rangi pekee iliyobarikiwa na Mwenyezi Mungu

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Sheikh wa mkoa wa Dsm Alhad Musa Salum amesema CCM imepewa upendeleo na mwenyezi Mungu kwa sababu wanatumia rangi ya kijani ambayo ndio rangi pekee iliyobarikiwa na Mungu.

Alhad Musa amesema hayo wakati akiiombea dua CCM katika katika sherehe za miaka 43 ya chama hicho inayofanyika kitaifa jijini Dsm leo.

Mgeni wa heshima ni mama Samia Suluhu, makamu wa Rais wa JMT

Source: Channel ten

Maendeleo hayana vyama!
 
Dah inasikitisha sana siku hizi kuona "VIONGOZI WA DINI (Masheikh na Mapadri) wakijisahau kumtumikia mungu na kujiingiza kwenye siasa, ila cha kushanga "WAZIRI" hawaambii waanzishe chama cha siasa kama "ROMA MKATOLIKI". Viongozi wa dini wanajivalisha ngozi ya unafiki.

Wanajifanya kujinyamazisha na kujisahaulisha ukweli kuwa mungu amekataza na hapendi kwa kutilia mkazo "MAUWAJI/UTEKWAJI/UKANDAMIZWAJI/UONEVU" wa raia.

Vyeo vyote ni dhamana mbele ya mungu, na kila mwenye cheo atahojiwa siku ya kiama kuhusu utawala aliokua nao na aliowatawala (Wataulizwa kama walitenda "UADILIFU" mpaka kwa wanyama kama mbwa waliokua chini ya utawala wao).

DUNIA ni "PEPO" kwa wasiomuogopa mungu, na ni "GEREZA" kwa wanaomuogopa mungu.
 
Back
Top Bottom