Dah inasikitisha sana siku hizi kuona "VIONGOZI WA DINI (Masheikh na Mapadri) wakijisahau kumtumikia mungu na kujiingiza kwenye siasa, ila cha kushanga "WAZIRI" hawaambii waanzishe chama cha siasa kama "ROMA MKATOLIKI". Viongozi wa dini wanajivalisha ngozi ya unafiki.
Wanajifanya kujinyamazisha na kujisahaulisha ukweli kuwa mungu amekataza na hapendi kwa kutilia mkazo "MAUWAJI/UTEKWAJI/UKANDAMIZWAJI/UONEVU" wa raia.
Vyeo vyote ni dhamana mbele ya mungu, na kila mwenye cheo atahojiwa siku ya kiama kuhusu utawala aliokua nao na aliowatawala (Wataulizwa kama walitenda "UADILIFU" mpaka kwa wanyama kama mbwa waliokua chini ya utawala wao).
DUNIA ni "PEPO" kwa wasiomuogopa mungu, na ni "GEREZA" kwa wanaomuogopa mungu.