Sheikh Alhad Musa Salum: Rangi ya Kijani inayotumiwa na CCM ndio rangi pekee iliyobarikiwa na Mwenyezi Mungu

Sheikh Alhad Musa Salum: Rangi ya Kijani inayotumiwa na CCM ndio rangi pekee iliyobarikiwa na Mwenyezi Mungu

johnthebaptist,
Mungu alilaani Rangi zingine zote. Huo ni uwaza waza wa hali ya juu.

Kwa staili hiyo mnataka wafuazi wa dini yenu wawe wanaccm tu? Na hivi Uchaguzi Mkuu bado sana. Itakuwaje wakati wa kampeni?
 
Uzuri Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema si mnafiki na huwa hakai karibu na wanafiki.
 
Kiukweli Rangi ya kijani ndio Rangi no 1 ya peponi na ndio iliyobarikiwa na ndo Rangi ya ushindi kwa mujibu wa uislam...wazee wengi waanzilishi wa iliyokuwa TAA na baadae TANU walikuwa waislam...hivyo kutokana na kuwa walikuwa wanasoma maandiko kama hadith za mtume muhamad nk ambazo zilieleza ubora wa Rangi ya kijani ikapelekea kuipa TAA,TANU na baadae CCM Rangi ya kijani... johnthebaptist,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio, alinukuu aya husika!

Alinukuu aya husika kutoka katika Qur-an ikisema kuwa CCM inapendelewa na Mola kwa sababu ya rangi ya kijani? Sisemi kuwa mimi ni msomi lakini nimesoma Qur-an yote madrassa na sikuona mahali popote neno CCM wachilia mbali kuwa mola anawapendelea CCM. Kama ipo naomba unijuze tafadhali.

Kama shekhe amesema yu kuwa rangi ya kijani ni ndio inayopendelewa na Mola basi ni kwa nini Yanga haikuwa ikichukuwa ubingwa kila mwaka toka ilipoanzishwa?

Naomba unielewe majibu yangu sikusudii kukuelekezea wewe ila nasema in general tu kwa alichokisema huyu shehe, nimejibu kwa kutumia quote yako kwa sababu tu umesema alinukuu aya jambo ambalo linanisumbua kweli.
 
Back
Top Bottom