GE2025 Sheikh Alhad Mussa: Maandamano hayatakuwepo na hakuna kijana wa kiislam atakayeshiriki katika maandamano

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kwamba una maanisha wale waislamu wenzenu ambao wanaandamana kule Morocco kwa ajili tu ya kuishinikiza serikali yao iache kufuja pesa kwenye kujenga viwanja vya michezo na badala yake watumie pesa hizo kuboresha huduma za afya na elimu ni wajinga na wanafanya jambo ambalo ni haramu?

Kwa hiyo wewe hapo ndio unajiona unaujua sana uislamu kuliko hata waarabu waliokuletea hiyo dini?

Nyie waislamu wa Tanzagiza ni vilaza sana na mna udumavu wa akili.
 
Viongozi wa Dini waache kutugawa sisi Watanzania ni wamoja 🇹🇿
 
Ni wa kupuuzwa.
 
U sheikh alirudishiwa lini?

Alipumzishwa tangu alipomchakata mke wa Dr.Mwaka, nashangaa kusikia ni sheikh tena?

Huyu kiboko yake ni Dk.Mwaka tu.
 
Vijana wooote waTanzania, ambao ni waumini wa dini ya kiislamu; ni mali ya huyu bwanah!
Utawaamuliaje watu wenye akili zao vichwani wafanye unachokitaka wewe?

Wewe uTanzania wako na uislamu wako ni muhimu zaidi ya wao?
 
Pumbavu zake.

Mimi ni kijana wa kiislamu na nimeshajiandaa kwa maandamano.
M Muislamu ukifa kwenye maandamano unakuwa umekufa katika kifo Cha Kijahiliya .

Kuandamana si njia ya Uislamu , sisi Waislamu tunefunzwa kila kitu tuifuate miongozo ya dini yetu .Tukiacha fact kuwa maandamano si njia ya kudai haki katika Uislamu kwenye maandamano Kuna mambo mengi si ya sawa yanafanyika ambayo Muislamu kama vile uharibifu wa Mali za Umma , Fujo , Amani kutoweka , mchanganyiko usio na lazima kati ya Wanaume na Wanawake nk.

Naisihi nafsi yangu na ndugu wengine wa Kiislamu kumcha Allaah katika Hilo na kuachana na njia potofu.
 
Uislamu umesema watu waswali je kila mtu ataswali kwa namna anavyotaka , muda anataka na idadi ya rakaa anataka kisa ameambiwa aswali tu ?

Kuamrisha mema na kukataza maovu kupo ila kana njia zake , Uislamu kila kitu kimwekwa namna , taaratibu na misingi ya kuendea na sio kufanya tu ilimradi.

Ndugu , maandamano sio njia ya Waislamu Mimi Zamani nilikuwa mstari wa mbele kwenye uharakati ila baada ya kusoma dini kupata mwangaza na kufikiri kisawasawa nimeacha na maswala hayo naangalia maelekezo ya dini yanasemaje na yanataka tufanye Nini katika kila hali.

Ukisema ufanye tu hata Al shabab, Al Qaeda warasema Uislamu umeaamrisha tupigane tutee dini , swali linakuja je hao Magaidi wanaodai kutetea Uislamu wanapambana kama dini jinsi ilivyoelekeza ?
 
Kwamba watu wavulie kutekwa?
 


Kwanza, usinifokee.


Pili, nakuambia hili ukakae nalo na ujue kuwa; Uislam sio Dini kwa ajili ya watu fulani tu au kabila fulani tu. Hii ni Dini ya Allah iliyoletwa kwa ajili ya watu wote bila kujali rangi zao wala makabila yao. Kinachotazamwa ni Dini inasemaje, sio watu fulani wanasemaje? Na fahamu kuwa miji haitakasi watu.

Tatu, wanachokifanya ndugu zetu wa Morocco sio sahihi kwa mujibu wa Uislam na ni kwenda kinyume na mafunzo ya Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake), na kwenda kinyume na mafunzo ya Mtume kuna madhara makubwa. Matatizo makubwa tunayoyapata Waislam leo miongoni mwa sababu zake kubwa kabisa ni kwenda kinyume na maelekezo ya Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake).

Maandamano ni katika mila za makafiri za kidemokrasia zilizoanzia Ulaya huko, hayana Asili katika Uislam. Sio njia ya kutafuta haki wala suluhu katika Uislam na wala sio njia ya Kishari'ah ya kuamrisha mema na kukataza mabaya. Na ni kinyume na mafundisho ya Mtume. Na ndio maana hakuna sehemu katika miji ya Waislam hayo maandamano yalileta kheri yoyote, bali shari na uharibifu na udhalili juu ya udhalili kwa Waislam. Kwa mfano tu tazama, Libya, Yemen, Syria, Misri, Tunisia na Sudan na Algeria miaka ya 90 kulifuata nini baada ya maandamano dhidi ya watawala.

Na Mtume wetu alitukataza kuwakosoa watawala wetu hadharani na kuwapiga vita na tumekatazwa kuondoa mkono wa utiifu kwao na kuwafanyia uasi.

Hivyo mimi Muislam mweusi mbantu ninawaonea huruma ndugu zangu katika Iymaan walioko Morocco wanaofanya maandamano kwa sababu njia waliyoiendea sio ya sawa iko kinyume na mafundisho ya Uislam na inapelekea katika fitna ambayo ikija inamchukulia anayehusika na asiyehusika. Tunamuomba Allah Afya na Salama.

Na mwisho kwa kutilia mkazo zaidi; ndio, maandamano ni haramu.
 
Hii inaitwa divide and rule
Hii inaitwa divide and rule
 
Hata hawa waarabu wanavyo tudharau Sisi weusi sio uislamu. Kwa hivyo waislamu wa kweli ni Sisi tulio weusi na wa haki ya chini. Wengine wanautumia uislamu Kwa Neema zao.
 
Kwamba watu wavulie kutekwa?


Mtume wetu katuusia kuwa na subra kunako dhulma ya mtawala, tuchukie dhulma yake ila tuwe na subra na tusijitoe katika utiifu kwake na tusimseme hadharani. Tukitaka kumnasihi tumnasihi kwa siri tukipata hiyo fursa.

Na humu mwetu katika nchi hii hatuna uhakika kuwa ni mtawala ndiye anayeteka hao watu. Hivyo kwanza sisi Waislam hatupaswi kutoa hukumu na kuwasibu watawala wala mtu mwengine yoyote kwa kutumia tetesi na uvumi dhidi yao. Hatutakiwi kumsibu yoyote kwa sababu ya habari isiyo na uthibitisho dhidi yake.

Hapo hapo bado Dini yetu inatutaka tuwe na subra na mtawala hata kama atakuwa ni muovu na dhalimu na tusijitoe mkono wa utiifu kwake na kama tuna jambo la kusema au kushauri au nasaha kwake basi tumnasihi kwa siri, ukikutana naye ana kwa ana umnasihi kwa siri au umuandikie kwa siri kwa hikma na busara, kinyume na hapo tuwe na subra na kuepuka mzozo na mvutano na mtawala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…