Acha kunifokea
MAANDAMANO NI HARAMU NA SIO KATIKA UISLAM.
Hujui Uislam na acha kujifanya mjuaji.
View: https://youtu.be/inhkOPcQewI?si=yRQGfx2tjFbvbEms
Katika hali ya ukhiyari, atatangulizwa mwanaume katika mambo ya uongozi. Lakini hatuna khiyari na mtawala ni mwanamke, amepata nguvu au kawekwa na wenye nguvu na mamlaka, sisi tutamsikiliza na kumtii kama mtawala wetu hata kama ni mwanamke.
Mimi sipigi kura na sijawahi kupiga kura na sio kwasababu ya hii kampeni yenu uchwara ya uasi ya "no reform no election" mimi binafsi sijawahi kupiga kura kabisa. Na hiyo kura hata watu katika nyinyi watampigia Rais usitake kuwamalizia hasira zako Waislam kwa sababu unawaona ni easy target.
Ninachozungumza sio kwamba ninaipigania CCM au chama chochote kile au mimi ni chawa. Mimi sio chawa, mimi nasimama na Dini yangu na ninalipigania hili kwa ajili ya Allah na kutafuta radhi zake na kumfuata Mtume Muhammad (Swala na Salamu ziwe juu yake).
Haya masuala ya kutozozana na mtawala, na kumsikiliza, na kumtii (kumtii katika yasiyo maasi), na kutomsema hadharani, na kutomtukana na jambo la kuwa na subra juu yake mtawala na kumuombea Dua ya kheri mtawala wetu hivyo ndio Dini yetu inavyotutaka na kutufundisha na hili ni kwa maslahi ya Amani na utulivu na hata ustawi wa Nchi yetu.
Mitume (Amani Iwe juu yao) walikuja kulingania watu wao katika Tawheed (Kumuabudu Allah Peke yake bila ya kumshirikisha na chochote) na kuwakataza shirki. Waliwafundisha watu wao kumuabudu Allah kwa namna alivyotaka Allah Mwenyewe bila ya kumshirikisha na chochote na kupitia wao Allah aliwaletea waja wake yale yaliyo na maslahi kwao na kuwaonesha yale yenye madhara kwao. Mitume mpaka Mtume wa mwisho Muhammad (Swala na Salamu ziwe juu yake) alikuja na Shari'ah ya mwisho kwa ajili ya watu wote mpaka Kiyama na akawafundisha watu Tawheed na kuwakataza Shirki.
Mitume wote (Amani Iwe juu yao) walikuja kuwafundisha watu Haki itokayo kwa Mola wao na Haki ni kile walichokuja nacho Mitume na waliwafundisha watu . Mtume wa mwisho Muhammad (Swala na Salamu ziwe juu yake) amewafundisha watu utaratibu katika kila jambo la maisha yao ya kila siku ikiwemo namna ya kuamiliana na watawala;
Hudhayfah ibn al-Yaman reported: I asked, “O Messenger of Allah, we were living in an evil time and Allah brought us good in which we live now. Will there be evil after this good?” The Messenger of Allah, peace and blessings be upon him, said, “Yes.” I said, “And any good after this evil?” The Prophet said, “Yes.” I said, “And any evil after this good?” The Prophet said, “Yes.” I said, “How will it be?”
The Prophet said, “After me, leaders will come who do not follow my guidance or my Sunnah. Some of their men will have the hearts of devils in a human body.” I said, “O Messenger of Allah, what should I do if I live to see that time?” The Prophet said, “You should listen and obey the ruler, even if he strikes your back and takes your wealth, even still listen and obey.”
Source: Ṣaḥīḥ Muslim 1847
Ndugu zetu Waislam wa Palestina (Allah Awape Nusra) wanakosea katika baadhi ya namna wanayoenda nayo dhidi ya mazayuni. Hii ni mada pana. Jihad ina vidhibiti na masharti yake.
Ndugu zangu waMorocco ninawaombea kwa Allah Awaongezee ustawi na utajiri na maendeleo juu ya ustawi na utajiri na maendeleo waliyonayo. Allah Humpa Amtakaye katika waja wake. Na ndio maana sisi hatuhangaiki na watawala. Mama Samia (Allah Amuongoze na Alitengeneze jambo lake liwe zuri) sio wa kwanza yeye hapa kuwa mtawala wa Nchi hii na umaskini hajaleta yeye. Allah Ndio Humkunjulia Rizki Amtakaye katika waja wake na Humpimia Rizki Amtakaye katika waja wake, Sifa zote Njema zinamstahiki Allah Mola Mlezi wa Walimwengu wote na Viumbe Vyote.
Watawala hawapandishi wala kushusha bei na gharama za maisha;
Narrated Anas bin Malik (RA):
When prices were high in al-Madinah in the time of Allah's Messenger (ﷺ), the people said,
"O Allah's Messenger, prices have become high, so fix them for us." Allah's Messenger (ﷺ) replied,
Allah is the One Who fixes prices, Who withholds, gives lavishly and provides. And I hope that when I meet Allah, the Most High, none of you will have any claim on me for an injustice regarding blood or property." [Reported by al-Khamsah excluding an-Nasa'i; Ibn Hibban graded it Sahih (authentic)].
وَعَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ - رضى الله عنه - قَالَ: { غَلَا اَلسِّعْرُ بِالْمَدِينَةِ عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اَللَّهِ - صلى الله عليه وسلم -فَقَالَ اَلنَّاسُ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ ! غَلَا اَلسِّعْرُ, فَسَعِّرْ لَنَا, فَقَالَ رَسُولُ اَللَّهِ - صلى الله عليه وسلم -إِنَّ اَللَّهَ هُوَ اَلْمُسَعِّرُ, اَلْقَابِضُ, اَلْبَاسِطُ, الرَّازِقُ, وَإِنِّي لَأَرْجُو أَنْ أَلْقَى اَللَّهَ -تَعَالَى-, وَلَيْسَ أَحَدٌ مِنْكُمْ يَطْلُبُنِي بِمَظْلِمَةٍ فِي 1 دَمٍ وَلَا مَالٍ " } رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ إِلَّا النَّسَائِيَّ, وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ 2 .
1 - في هامش " أ " أشار إلى أن في نسخة: " من ".
2 - صحيح. رواه أحمد ( 3 / 156 )، وأبو داود ( 3451 )، والترمذي ( 1314 )، وابن ماجه ( 2200 )، وابن حبان ( 4914 ). وقال الترمذي: " حسن صحيح ". وقال الحافظ في " التلخيص " ( 3 / 14 ): " إسناده على شرط مسلم ". وهو كما قال.
Sunnah.com reference : Book 7, Hadith 38
English translation : Book 7, Hadith 815
Arabic reference : Book 7, Hadith 812
Narrated Anas bin Malik (RA): When prices were high in al-Madinah in the time of Allah's Messenger (ﷺ), the people said, "O Allah's Messenger, prices have become high, so fix them for us." Allah's Messenger (ﷺ) replied, Allah is the One Who fixes prices, Who withholds, gives lavishly and provide
sunnah.com
Ndugu zangu wa Morocco kama wakisikiliza watu kama wewe
Muhimbu wataharibu.
Mimi ningepata fursa ningewakumbusha ndugu zangu wa Morocco maneno haya ya Swahaba Mtukufu na Khalifa Muongofu aliyeongozwa, 'Umar Ibn Khattab (Allah Amridhie);
'Umar Ibn al-Khattāb said:
“Verily, we were a disgraceful people and Allah honored us with Islam. If we seek honor from anything besides that with which Allah honored us, Allah will disgrace us.”
[al-Mustadrak 214]
Wasiendekeze watu kama wewe ili wasije kuwa kama Sudan, Libya, Syria, Yemen na Algeria (miaka ya 90) na ndugu zao na ndugu zetu wengine.
Maandamano ni katika mila za makafiri na hayana nafasi katika Uislam na wala sio njia ya watu kudai haki katika Uislam na wala sio njia ya kuamrisha Mema wala kukataza maovu iliyowekwa na Shari'ah.
Mtume wetu (Swala na Salamu ziwe juu yake) katufundisha kuwa na Subra tunapohusiana na kuamiliana na watawala.
Na ndio, Maandamano ni Haramu katika Uislam
Messenger of Allah (ﷺ) said: "It is obligatory for you to listen to the ruler and obey him in adversity and prosperity, in pleasure and displeasure, and even when another person is given preference over you.” - Sahih Muslim 1836
Tuna Subra juu ya mtawala. Hatuandamani. Maandamano ni Haramu.
Na Waislam tuna uhuru wa kuabudu kwenye Nchi yetu. Alhamdulillah. Kumuabudu Allah ndio lengo la kuumbwa kwetu. Sisi tunaifuata na kuilingania Dini yetu.
Halafu kama unasema Nchi hii haiongozwi kwa Sheria za Kiislam, why ulikuwa unanipigia kelele kuhusu mtawala mwanamke kule juu? Sisi Waislam tumefundishwa namna ya kuishi katika hali zote. Tunapokuwa na nguvu na tunapokuwa dhaifu, tunapokuwa tuna hiari na pale tunapokuwa hatuna hiari. Na hali nyengine zote. Dini yetu haiji contradict wala kujigonga. Alhamdulillah kwa Neema ya Uislam na Sunnah.
Maandamano ni Haramu katika Uislam na hatukubali muendelee kuchochea uvunjifu wa Amani kwa kisingizio chochote kile, tutatumia kalamu zetu na ndimi zetu kwa kadri ya uwezo wetu, In Shaa Allah, kulipinga hili. Nchi hii ni yetu sote na hatokaa kimya nyinyi wachache mtuzamishe baharini wote na tuko kwenye meli moja.
Ninamuomba Allah kwa Sifa zake na Majina yake Matukufu Aiilnde na kuidumisha Amani yetu na Awaongoze watawala wetu katika njia iliyonyooka na Awajaalie wafanye maamuzi sahihi, Allahumma Aamiin.
Kazakh destroyer adriz Kisai Chifu mkuu