Uchaguzi 2020 Sheikh Alhad Mussa Salum asema Sheikh Mohamed Idd ni mshamba anayesumbuliwa na njaa, adai ana laana

Nilijua angejibu hoja za huyo shehe Muhamad zaidi sana naona personal attacks tu. Kweli Bakwata haitoshi
 
Huyu Shekh anafurahisha sana utasema taarab ya mipasho, swali umeulizwa uchaguzi ulifanyika lini? wapi? ulichaguliwa na nani? haya ndio ya kujibu. Eti mkoa wangu wa Dar es salaam. Hapa ndio tumefika waislamu huyu mtu awekwe sehemu yake kapoteza hata heshima kama alikuwa nayo ya Shekh wa mkoa.
 
Wewe umeona the way wanavodeal na kutofautiana kwao ni professional hiyo???!

Mtu akishikwa na kosa la kuua njia za mahakama zikitumika akanyongwa akafa. Then mtu mwingine kafanya same mistake lkn on the spot wananchi wakamkamata kipigo mpaka akafa.

Wote hao wamekufa, sawa, je njia ipi ya kuhukumu imeenda ki professional.
Jibu unalo. Asante.

Ndio maana nikasema imetokea ku hitilafiana masheikh hawa. Huyo muimba taarab kajiimbisha taarabu. Is that profesiónal way ya ku deal na issues mtu mkubwa km huyo??!!!!! Jibu pia unalo.
Asante.
 
Ukipata wasaa fuatilia darsa za sheikh Muhammad Eid, hata kupitia YouTube, utapata faida kubwa inshallah. Ni kweli unapokuwa kiongozi kuna baadhi ya mambo haifai kuyajibu (au walau kuyajibu hadharani).
 
Ukipata wasaa fuatilia darsa za sheikh Muhammad Eid, hata kupitia YouTube, utapata faida kubwa inshallah. Ni kweli unapokuwa kiongozi kuna baadhi ya mambo haifai kuyajibu (au walau kuyajibu hadharani).
Nitafanya hivyo mkuu insha'Allah.
Channel tena mara chache sana ikinikuta namsikiliza.
 
Nimemkumbuka Sheikh Ilunga,Mwenyezi Mungu amrehemu.Alisema Sana kuhusu hawa masheikh wa bakwata,bahati mbaya Sana hatujui vile jinsi tunaweza kuwatoa.
Katika uwakilishi wa sekta yoyote inabidi uwepo uaminifu,watu wakuamini ndo uwaongoze.bakwata haiaminiki na waislam walio wengi na bahati mbaya zaidi bakwata haiwezi kuondoka mpaka iondoke CCM.na Hilo ndo linaleta ugumu.
 
Okay
Shehe Mohammed yupo sahihi, shehe wa kwa jina la yesu na Mohamed amejaa kibri

Hakuna sheik serious anaweza changanya Yesu na Mohamed katika muktaza wa masihara kiasi kile......

Sheik Ponda knows what he does, he is very disciplined, kweli amejitoa kabisa kwa ajili ya wengine!
 
kama Uislam ndio huu basi sidhani kama kweli ni dini ya Amani.


Wewe umekosa hoja; Inakuaje uuhusishe UISLAMU na matendo ya Masheikh???, Uisilamu unaangaliwa kwanza kupitia Qur'an, Sunna na Hadithi za Mtukufu mtume (saw), hivyo ndivyo vigezo muhimu vya kuuangalia Uisilamu.

Ikibidi kuuangalia Ukristo kwa njia hiyo yako, utasemaje kipindi kile mchungaji Gwajima alipomshambulia kwa maneno ya mtaani Askofu Pengo kwamba kala maharage ya wapi???🤣, je hapo na sisi tukisema Ukristo sio dini ya amani itakuwa sawa???.

Jichunge sana unapotoa hoja zako.
 
Nakuheshimu lakini kwa hili naona mwenzangu sijui umechelewa wapi kumfahamu huyu Kanjanja wa dini. Alhad Musa Salum ni mjasiriadini. Ni mtu aliye tayari kutumiwa na yeyote ilimradi anamfadhili. Enzi za Makonda Dar alikuwa kama mke mdogo, Leo haongei lolote kuhusu Makonda kwa sababu tu Makonda hawezi kumwinua kama zamani.
 
Kama kuna kupumbazwa fulani, hawa wanachaguliwa na nani, au kuteuliwa na nani, katika mfumo upi??
Au mapandikizi!?
Swali fikirishi SANA!

Wakae kimya kujibizana kupitia media ni kosa kubwa!

Everyday is Saturday...............................😎
 
Msamehe kwa hilo. Tunawaambia kila siku matendo machafu ya viongozi wa dini wanaosapoti CCM yanakwenda kinyume na dini zao hivyo wasihusishe dini na upuuzi wao. Gwajima alipokengeuka hatukuhusisha dini yake bali yeye mwenyewe na ujinga wake, Pengo alipoongea upotovu tulimsema yeye kama Pengo, Alhadi Mussa alipoacha njia na kuanzisha dini Mseto (IslamKristo) tulimsema yeye kama yeye.
 
Huyo Sheikh huwa ananichekesha sana, akiongea anaongea kiswahili chenye lafudhi ya kiarabu. Basi ccm wakisikia hiyo lafudhi, wanamuona ndio kasoma dini vibaya sana. Nilipomwona tu huyo Sheikh wanafuatana na Makonda, nilijia fika hamna Sheikh bali muhuni.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] kwamba hakuna kitu pale
 
Hivi alhadi haoni aibu kufanya siasa za kijinga
 
Huwa nachukia kweli kuona wajinga wakichanganya Kiingereza na Kiswahili
Mjinga ni mtu gani?!
Anyways, wengine tumekaa sana nchi za nje kuna des mots ya kiswahili tunayatafuta tunakosa ndio maana we mix the two langes (oops hapa nime mélanger na ki français)
Hivo monsieur tuna ku demander utu forgive tu maana sio kwamba we like it.
Ne hésitez pas kutu critisize lakini parceque that's how tunajifunza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…