Muislamu wa kwanza,wakati wa Mtume Muhammad(Rehema na Amani ziwe juu Yake)ni Mwanamke Bi Khadija.Bi Khadija(Mwanamke),ndiye aliyemuongoza Mtume Muhammad(Rehema na Amani ziwe juu Yake),Yeye Mtume Muhammad(Rehema na Amani ziwe juu Yake),alipotokewa na Jibril,kumfikishia ujumbe,Mtume hakujuwa lolote ,mpaka alipomuelezea Bi Khadija,na Bi Khadija ndiye aliyemwambia kuwa huyo ni Jibril,na ndiye aliyewatokea Mitume wengi,na kuwaelezea kuhusu mambo ya dini.
Bi Khadija(Mwanamke),ndiye alimuongoza Mtume(Rehema na Amani ziwe juu Yake),Kwenda kwa mwanachuoni,aliyesoma Injili,ili amfafanulie kuhusu sifa za Mtume,atakayekuja baada ya Nabii Issa
(A.S).Na Mtume akakubali kuogozwa na mawazo ya Mwanamke,kwenda kwa huyo mwanachuoni wa Injili,na akaelezewa sifa za Mtume atakayekuja,baada ya Nabii Issa,na Mtume akakubaliana na maneno hayo.
Na kabla ya hapo,Mtume Muhammad(Rehema na Amani ziwe juu Yake),alikuwa akifanyakazi yakuajiriwa na Bi Khadija(Mwanamke),akiwa ndio kiongozi wake wa kazi,na hakulipinga hilo.
Nani aliye Muislamu,atapinga historia,ya Bi Khadija,ya kuwa Mtume,alifanyakazi chini yake,akiwa ni mwajiriwa,kabla ya kumuoa na kuwa mkewe.
Na nani atapinga kuwa Bi Khadija,(Mwanamke),ndio Muislamu wa kwanza,na ndiye vile vile wa kwanza,kumuuelekeza Mtume,kuhusu Jibril,na kumuingoza kuwa yeye ndio Mtume.
Tukija katika,Muislamu wa kwanza,kuuliwa katika uislamu,kutokana uislamu wake,ni Bi Summaya(Mwanamke),huyu aliteswa na kuuliwa,na hakuacha uislamu wake.
Nani kama Bi Khadija(Radhi za Allah,ziwe juu Yake).Mpaka Mtume anafariki,anamtaja Mwanamke huyu,jinsi alivyomuongoza katika uislamu.
Achana na hadithi,zilizoingizwa katika uislamu za israiliat,kupotosha maneno ya Mtume.Soma somo la "Ilimu l khadith",uwelewe hadithi sahihi na zisizosahihii.