Sheikh Bombo: Viongozi wa Dini tuingizwe kwenye payroll ya Serikali

Sheikh Bombo: Viongozi wa Dini tuingizwe kwenye payroll ya Serikali

Sheikh Ibrahim Bombo kutoka Mkoani Mbeya amependekeza Serikali ianzishe utaratibu wa kulipa mishahara kwa Viongozi mbalimbali wa Dini kutokana na kazi nzuri wanayoifanya ya kulinda amani na kuhamasisha maendeleo Nchini Tanzania ambapo amependekeza kiwango chao cha chini cha mshahara kisipungue Tsh. laki tisa (900,000/=).

Sheikh Bombo ametoa maoni yake kwenye kongamano la kikanda, Kanda ya Kusini la kukusanya maoni ya Wannanchi kuhusu Dira mpya ya maendeleo ya mwaka 2050.

“Viongozi wa Dini wanafanya kazi nzuri sana kwenye hili Taifa hasa kuliombea amani na jambo lingine, ningependa kuona Viongozi wa Dini waingizwe kwenye pay roll ya Serikali kila mwezi wapate maokoto, ni muhimu sana na kiwango cha chini iwe 974,310, hiyo ianze kulipwa kuanzia mwaka 2025 kwenda 2050”

View attachment 3060936
No way ajira portal ipo si kwa ubaya Mungu ibariki Tanzania
 
Shule muhimu sana
Hakika sheikh mweupe sana kichwani,tena hasa,na hawa ndo tumewapa kulea vijana wetu, Kanisikitisha sana kuongolea mambo ya ndoa eti uwekwe umri kikomo,hajui hata maana ya ndoa ,akishaelewa mana ya ndoa kuwa ni muunganiko wa hiari kati ya mwanamke na mwanamme hataweza kurudiahuu upuuzi kuuongelea hadharani.

Elewa neno Muunganiko wa hiari
 
Hii inaonesha ni jinsi gani hii nchi hata watu mnaoona ni watu wazima nao ni wapumbavu
Mnaalikwa Kuchangia dira ya maendeleo ya nchi 2050 wewe unasema viongozi wa dini walipwe laki tisa na mwisho wa kuoa iwe miaka 35?
Tanzania ujinga bado ni mzigo, na nyie ndugu zangu waislam hawa viongozi wa dini muwawekee kiwango flani cha elimu ili kupunguza mazuzu kama hawa
 
Mashekhe wanapaswa kujivunia na kuonyesha wana wanafunzi wangapi.

Sio kutaka kujihusisha na serikali, kazi yao ni kutoa Elimu ya dini lakini wameacha, wanapishana kwenye korido za viongozi.
 
Sheikh Ibrahim Bombo kutoka Mkoani Mbeya amependekeza Serikali ianzishe utaratibu wa kulipa mishahara kwa Viongozi mbalimbali wa Dini kutokana na kazi nzuri wanayoifanya ya kulinda amani na kuhamasisha maendeleo Nchini Tanzania ambapo amependekeza kiwango chao cha chini cha mshahara kisipungue Tsh. laki tisa (900,000/=).

Sheikh Bombo ametoa maoni yake kwenye kongamano la kikanda, Kanda ya Kusini la kukusanya maoni ya Wannanchi kuhusu Dira mpya ya maendeleo ya mwaka 2050.

“Viongozi wa Dini wanafanya kazi nzuri sana kwenye hili Taifa hasa kuliombea amani na jambo lingine, ningependa kuona Viongozi wa Dini waingizwe kwenye pay roll ya Serikali kila mwezi wapate maokoto, ni muhimu sana na kiwango cha chini iwe 974,310, hiyo ianze kulipwa kuanzia mwaka 2025 kwenda 2050”

View attachment 3060936
Madrasa ni tatizo kubwa duniani
 
Ila viongozi wa kikristo wamewaacha mbali mno viongozi wa Kiislamu kwenye maokoto 😂
 
Bado sana, Dira haijaeleweka ni kitu gani. Wengine wanadhani tunaandika katiba, wengine wanadhani tunatunga sheria au kanuni..!!
 
Sheikh Ibrahim Bombo kutoka Mkoani Mbeya amependekeza Serikali ianzishe utaratibu wa kulipa mishahara kwa Viongozi mbalimbali wa Dini kutokana na kazi nzuri wanayoifanya ya kulinda amani na kuhamasisha maendeleo Nchini Tanzania ambapo amependekeza kiwango chao cha chini cha mshahara kisipungue Tsh. laki tisa (900,000/=).

Sheikh Bombo ametoa maoni yake kwenye kongamano la kikanda, Kanda ya Kusini la kukusanya maoni ya Wannanchi kuhusu Dira mpya ya maendeleo ya mwaka 2050.

“Viongozi wa Dini wanafanya kazi nzuri sana kwenye hili Taifa hasa kuliombea amani na jambo lingine, ningependa kuona Viongozi wa Dini waingizwe kwenye pay roll ya Serikali kila mwezi wapate maokoto, ni muhimu sana na kiwango cha chini iwe 974,310, hiyo ianze kulipwa kuanzia mwaka 2025 kwenda 2050”

View attachment 3060936
HILI JAMBO SIYO BAYA KABISA, LAKINI TATIZO NI VIONGOZI WA MADHEHEBU GANI NA WA NGAZI GANI?, (TAASISI TAMBULIWA) ZILIZO ANDIKISHWA KISHERIA NYUMA YA MIAKA YA 1950. BUT WHY?
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Kuna taarifa zinapenya chini kwa chini kuwa serikali iko mbioni kuanza kuwalipa mishahara viongozi wa dini. Sababu kubwa ya kuwalipa ni kwa kuwa kazi za viongozi wa dini kupitia mahubiri huwafanya wananchi watawalike kwa urahisi.

Hivyo, ukweli huu umeishawishi serikali kuona umuhimu wa dini katika utawala, pamoja na kwamba serikali haina dini na haifungamani na dini yoyote. Viongozi wa dini watakaoingia kwenye mkumbo huu ni wa dini ya kiislamu na kikristo. Viongozi wa dini za asili hawatahusika.

Kiasi cha fedha kinachopendekezwa ni kuanzia Tsh 900,000 lakini kiwango kinaweza kuongezeka kutegemea cheo cha kiongozi husika. Kwa mfano, masheikh na maaskofu watakuwa wanalipwa mishahara minono zaidi.

MAONI YANGU
Ukiangalia katika dhana nyingine utaona viongozi wa dini wanapaswa kulipwa. Dhana ninayoisemea ni kuona dini kama nyenzo inayotumiwa au inayosaidia serikali katika kumanage/kutawala watu wao. Viongozi wa dini wanatumika na serikali katika kutimiza malengo yao. Ikifika wakati wa kampeni za kisiasa, chanjo, milipuko ya magonjwa, psychological healings, etc hapo ndo utaona umuhimu kama mtawala kuwatumia viongozi wa kidini na utaona kama vile wanastahili kulipwa.​

Ukiangalia kwa upande wa imani kuwa dini ni imani then utaona hawastahili kulipwa. Maana sababu ni kuwa Imani zao zitakuwa compromised na kwa sababu hiyo hawatoweza kusimama na kukemea Jamii au serikali.

Lakini kuwalipa mishahara viongozi hawa, huku wakiendelea kupokea sadaka, swadaka na fungu la kumi, ni dhahiri kutawafanya wajikite zaidi kuwafanya wananchi watawalike kuliko kuwafanya waokoke na kuingia mbinguni au firdaus. Hilo ndilo tatizo pekee ninaloliona hapa.

====

Sheikh Ibrahim Bombo kutoka Mkoani Mbeya amependekeza Serikali ianzishe utaratibu wa kulipa mishahara kwa viongozi mbalimbali wa dini kutokana na kazi nzuri wanayoifanya ya kulinda amani na kuhamasisha maendeleo nchini Tanzania ambapo amependekeza kiwango chao cha chini cha mshahara kisipungue Tsh. laki tisa (900,000/=).Sheikh Bombo ametoa maoni yake kwenye kongamano la kikanda, Kanda ya Kusini la kukusanya maoni ya Wannanchi kuhusu Dira mpya ya maendeleo ya mwaka 2050.“Viongozi wa dini wanafanya kazi nzuri sana kwenye hili Taifa hasa kuliombea amani na jambo lingine, ningependa kuona viongozi wa dini waingizwe kwenye pay roll ya serikali kila mwezi wapate maokoto, ni muhimu sana na kiwango cha chini iwe 974,310, hiyo ianze kulipwa kuanzia mwaka 2025 kwenda 2050
 
Moja kati ya viongozi wanaolipwa vizuri ni viongozi wa dini. Na wana allowance nyingi zaidi, kuliko mfanyakazi wa kawaida.
Maoni yangu... Waongezewe zaidi mshahara tena kuanzia 1,000,000/- kwenda juu
 
Moja kati ya viongozi wanaolipwa vizuri ni viongozi wa dini. Na wana allowance nyingi zaidi, kuliko mfanyakazi wa kawaida.
Maoni yangu... Waongezewe zaidi mshahara tena kuanzia 1,000,000/- kwenda juu
Kweli kabisa mkuu. Wachungaji na maimamu wataanza na Tsh 900,000. Kwa maaskofu na masheikh, mshaharunaweza kupaa hadi 1,500,000 au zaidi

Mm naona ni sawa tu ila kinachoniuma ni kuona sisi viongozi wa dini za asili tumewekwa pembeni. Sijui serikali ina mpango gani na sisi.
 
Mimi naomba wawalipe hata million 2, kwa sababu mimi najua miradi muhimu ya serikali itakwama tu halafu hapo ndio tutaanza kuongea lugha moja inayofanana.
 
Back
Top Bottom