Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Kuna taarifa zinapenya chini kwa chini kuwa serikali iko mbioni kuanza kuwalipa mishahara viongozi wa dini. Sababu kubwa ya kuwalipa ni kwa kuwa kazi za viongozi wa dini kupitia mahubiri huwafanya wananchi watawalike kwa urahisi.
Hivyo, ukweli huu umeishawishi serikali kuona umuhimu wa dini katika utawala, pamoja na kwamba serikali haina dini na haifungamani na dini yoyote. Viongozi wa dini watakaoingia kwenye mkumbo huu ni wa dini ya kiislamu na kikristo. Viongozi wa dini za asili hawatahusika.
Kiasi cha fedha kinachopendekezwa ni kuanzia Tsh 900,000 lakini kiwango kinaweza kuongezeka kutegemea cheo cha kiongozi husika. Kwa mfano, masheikh na maaskofu watakuwa wanalipwa mishahara minono zaidi.
MAONI YANGU
Ukiangalia katika dhana nyingine utaona viongozi wa dini wanapaswa kulipwa. Dhana ninayoisemea ni kuona dini kama nyenzo inayotumiwa au inayosaidia serikali katika kumanage/kutawala watu wao. Viongozi wa dini wanatumika na serikali katika kutimiza malengo yao. Ikifika wakati wa kampeni za kisiasa, chanjo, milipuko ya magonjwa, psychological healings, etc hapo ndo utaona umuhimu kama mtawala kuwatumia viongozi wa kidini na utaona kama vile wanastahili kulipwa.
Ukiangalia kwa upande wa imani kuwa dini ni imani then utaona hawastahili kulipwa. Maana sababu ni kuwa Imani zao zitakuwa compromised na kwa sababu hiyo hawatoweza kusimama na kukemea Jamii au serikali.
Lakini kuwalipa mishahara viongozi hawa, huku wakiendelea kupokea sadaka, swadaka na fungu la kumi, ni dhahiri kutawafanya wajikite zaidi kuwafanya wananchi watawalike kuliko kuwafanya waokoke na kuingia mbinguni au firdaus. Hilo ndilo tatizo pekee ninaloliona hapa.
====
Sheikh Ibrahim Bombo kutoka Mkoani Mbeya amependekeza Serikali ianzishe utaratibu wa kulipa mishahara kwa viongozi mbalimbali wa dini kutokana na kazi nzuri wanayoifanya ya kulinda amani na kuhamasisha maendeleo nchini Tanzania ambapo amependekeza kiwango chao cha chini cha mshahara kisipungue Tsh. laki tisa (900,000/=).Sheikh Bombo ametoa maoni yake kwenye kongamano la kikanda, Kanda ya Kusini la kukusanya maoni ya Wannanchi kuhusu Dira mpya ya maendeleo ya mwaka 2050.“Viongozi wa dini wanafanya kazi nzuri sana kwenye hili Taifa hasa kuliombea amani na jambo lingine, ningependa kuona viongozi wa dini waingizwe kwenye pay roll ya serikali kila mwezi wapate maokoto, ni muhimu sana na kiwango cha chini iwe 974,310, hiyo ianze kulipwa kuanzia mwaka 2025 kwenda 2050