Sheikh Bombo: Viongozi wa Dini tuingizwe kwenye payroll ya Serikali

Sheikh Bombo: Viongozi wa Dini tuingizwe kwenye payroll ya Serikali

Wasilipe viongozi, bali serikali inaweza kutoa ruzuku kwa taasisi za kidini kama shule, hospitali, vituo vya malezi, nk.
 
Hii itapendeza, sena serikali ituangalie nasisi jobless pia watulipe ata laki 2 kwa mwezi
 
Kwa sisi wakristo tunaamini uchungaji ni wito. Wanalipwa pesa za kuendesha familia zao tu.
 
Acha kwa sasa hii habari niisome kama chai tu...
 
Kuifungamanisha dola na dini ni kitu hatari sana.

Hakuna kitu kama hicho kinaweza kutokea, uzuri utawala wa ccm mwisho wao umekaribia basi sahau kuhusu hilo.
Mkuu, kuwalipa mishahara viongozi wa dini wewe kinakuuma nini? Wanastahili kulipwa, tena suala hili ni kama limekuja kwa kuchelewa sana.
 
Kwa sisi wakristo tunaamini uchungaji ni wito. Wanalipwa pesa za kuendesha familia zao tu.
Kama mnaamini ni wito kwanini akina GeoDavie, Kiboko ya Wachawi na Suguye wanawalipisha waumini wao mamilioni ya fedha ili kuwahudumia kiroho?
 
Viongozi wa dini wanachangiwa na waumini wao mishahara minono Huku waumini hao kuishia kuwa mafukara wa kutupwa
 
Mkuu, kuwalipa mishahara viongozi wa dini wewe kinakuuma nini? Wanastahili kulipwa, tena suala hili ni kama limekuja kwa kuchelewa sana.
Huna akili, kodi yangu siyo kulipa viongozi wa dini, watafute shughuri za kuwaingizia vipato.

Mwamposa amewezaje kuwa na media zake amejiri watu na hao wengine wanashindwaje?
 
Huna akili, kodi yangu siyo kulipa viongozi wa dini, watafute shughuri za kuwaingizia vipato.

Mwamposa amewezaje kuwa na media zake amejiri watu na hao wengine wanashindwaje?
Mkuu una tatizo sio bure. Kwani viongozi wa dini wakilipwa unapungukiwa nini? Kuliko hizo fedha zifujwe na mafisadi si afadhali zitumuke kuwalipa viongozi wa dini?
 
Tunakoelekea ni kugumu zaidi ya kule tulipotoka. Kwahoyo hakuna tena shughuli ya wito?
Dini sio wito kama unavyodhani. Hii ni kazi kama kazi nyingine. Lazima viongozi wa dini walipwe mishahara.
 
Fedha ni mali yangu , na dhahabu ni mali yangu , asema Bwana wa majeshi . Utukufu wa mwisho wa nyumba yangu utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza , asema Bwana wa majeshi; na katika mahali hapa atanipa amani , asema Bwana wa majeshi .

Cc . Hagai 2:8-9
 
Aa wapi hiyo sidhani kama inawezakana; kama ni hivyo basi taasisi za dini ziruhusu TRA ndio inakusanya sadaka na kila zehebu lipewe goli la kiwango cha makusanyo Kwa mwezi Ili kukidhi.

Maana Kwa mkoa kama wa Mbeya na Songwe kila baada ya nyumba kumi kuna kanisa sasa sijui kama serikali inaweza kuubeba huu mzigo wa misumari, labda Waseeme viongozi wa kuu wa taasisi ambayo NI wawakilishi (head of organisation)Kwa kila kanda
 
Aawapi hiyo sizani kama inawezakana kama ni hivyo basi taasisi za dini ziruhusu TRA ndio inakusanya sadaka na kila zehebu lipewe goli la kiwango cha makusanyo Kwa mwezi Ili kukizi .Maana Kwa mkoa kama wa Mbeya na Songwe kila baada ya nyumba kumi kuna kanisa sasa sijui kama serikali inaweza kuubeba huu mzigo wa misumari,labda Waseeme viongozi wa kuu wa taasisi ambayo NI wawakilishi (head of organisation)Kwa kila kanda
Mkuu, sadaka hazitoshi ndio maana inashauriwa viongozi hawa walipwe. Serikali hawapaswi kukusanya sadaka. Hawaaminiki.
 
Back
Top Bottom