Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Sheikh Farid: Tunamshukuru Mwenyezi Mungu, kiufupi tunashukuru sisi tumeachiwa lakini huu ni mwanzo mwema ya busara ya marais wetu, Rais wa Zanzibar na Rais wa Tanzania, Amiri Jeshi mkuu, mama Samia Suluhu. Wamefanya busara kubwa sana kuondoa hii hali ya mtanziko ya muda mrefu sana wa hii Kesi.
Sheikh Mselem: Tumechukuliwa Gerezani jana Usiku, Maghrib na Insha tumeswali palepale gerezani, tumechanganywa na baada ya kuswali Maghribi tumetoka zetu tukaja Airport.
Airport tumeingia kwenye ndege ilikuwa iko faragha, tumefika zetu hapa tumefikia VIP ya zamani, ndege imekaa peke yake, hakuna mtu zaidi ya wenyewe na tulivyotoka pale kila mtu akaingia kwenye gari lake, akaulizwa nikupeleke wapi?
Mzee Mselem nikupeleke kwa mke wa kwanza, wa pili, wa tatu? Nikawaambia kwanza naenda kwetu, muda mrefu sijafika, nikayasome matatizo, ya kutatua nitatue na mengine alafu ndio nitaanza tena kwenda.
Hatukupewa waraka wowote.