Sheikh Farid: Tunashukuru tumeachiwa ni mwanzo mwema wa Rais Mwinyi na Samia

Sheikh Farid: Tunashukuru tumeachiwa ni mwanzo mwema wa Rais Mwinyi na Samia

Sheikh Farid: Tunamshukuru Mwenyezi Mungu, kiufupi tunashukuru sisi tumeachiwa lakini huu ni mwanzo mwema ya busara ya marais wetu, Rais wa Zanzibar na Rais wa Tanzania, Amiri Jeshi mkuu, mama Samia Suluhu. Wamefanya busara kubwa sana kuondoa hii hali ya mtanziko ya muda mrefu sana wa hii Kesi.

Sheikh Mselem: Tumechukuliwa Gerezani jana Usiku, Maghrib na Insha tumeswali palepale gerezani, tumechanganywa na baada ya kuswali Maghribi tumetoka zetu tukaja Airport.

Airport tumeingia kwenye ndege ilikuwa iko faragha, tumefika zetu hapa tumefikia VIP ya zamani, ndege imekaa peke yake, hakuna mtu zaidi ya wenyewe na tulivyotoka pale kila mtu akaingia kwenye gari lake, akaulizwa nikupeleke wapi?

Mzee Mselem nikupeleke kwa mke wa kwanza, wa pili, wa tatu? Nikawaambia kwanza naenda kwetu, muda mrefu sijafika, nikayasome matatizo, ya kutatua nitatue na mengine alafu ndio nitaanza tena kwenda.

Hatukupewa waraka wowote.


Tanzania KWANZA....

HARAKATI ZOZOTE hazina thamani ya kuzidi uwepo wa TANZANIA.....

#KaziInaendelea
#NchiKwanza
 
Hawa magaidi wameachiwa kwa sababu ya dini yao .... Lazima kosa hili liwagharimu watu na serikali..yaani mkawaalika na wamarekani kuwasaidia leo hii mnasema hawana hatia ...
Hawa ni magaidi na magaidi huwa wanawekwa kizuizini milele
 
Hii kesi hii,ni kama mtego kwa mama samia,
Sasa tuambiwe walikuwa na kosa?au uzanzibar na uislam wa Raisi aliyepo umechangia hawa kuachiwa?
Tusipokuwa makini tunaweka "mfano mbaya,huko mbele tutapata tabu sana.
 
Hii kesi hii,ni kama mtego kwa mama samia,
Sasa tuambiwe walikuwa na kosa?au uzanzibar na uislam wa Raisi aliyepo umechangia hawa kuachiwa?
Tusipokuwa makini tunaweka "mfano mbaya,huko mbele tutapata tabu sana.
Haya tumeyataka wenyewe Watanganyika
 
Aende kwanza nyumbani akitoka aende kwa mke wa kwanza kusuuza rungu alafu na kesho kwa nke wa pili na kesho kutwa kwa nke wa tatu dadekii[emoji3][emoji3]
 
DPP afute kesi zote zinazongoja ushahidi kukamilika kama watuhumiwa wamekaa zaidi ya miaka 3 mahabusu kwa kusubiria ushahidi kukamilika.
Naunga mkono Hoja, hebu fikiria familia zao Watoto hawamuoni Baba au Mama kakaa Gerezani kwa kukosa Dhamana,Sheria kandamizi lazima tuzifute wajameni.
 
Yule bwana mdogo wa Mbeya somebody Idude nae ni vizuri akaachiwa akaungane na familia yake wote tunajua jela siyo kuzuri ahurumiwe!!!
 
Back
Top Bottom