Naona shehe lenu munaloliabudu limekufa kibudu,mkaungane nalo Jahanam linawasubiri
View attachment 3402021
Mshika Bendera Ya Jarhu Na Ta’adil...
Ash-Shaykh Al-ʿAllāmah Abuu Muhammad Rabīʿ Bin Haadī Bin ʿUmayr Al-Madkhaliy..
Katika Zama Ambazo Nuru Ya Haki Imefichwa Na Vumbi La Batili, Na Sauti Za Wasio Na Maarifa Zimezidi Kuwa Juu Kuliko Sauti Za Maulamaa, Alisimama Mtu Mmoja...
Mpole Kwa Tabia, Mkali Kwa Hoja, Mnyenyekevu Kwa Muumba Wake, Lakini Jasiri Katika Kusema Kweli Mbele Ya Wengi Wanaopinga
Na Huyu Sio Mwingine Bali Ni Shaykh Rabii’ Bin Haadi Al-Madkhali... Bendera Ya Sunnah Na Nguzo Ya Manhaj Salafiyyah Katika Karne Hii Ya Fitnah
Mwanzo Wa Safari...
Alizaliwa Mwaka 1351H (1933M) Katika Kijiji Cha Jizan, Kusini Mwa Saudi Arabia, Sehemu Ambayo Haikuwa Maarufu Kitaaluma, Lakini Allaah Aliichagua Iwe Chimbuko La Mlinzi Wa Dini
Alianza Kusoma Qur-Aan Kijijini Kwao, Akaendelea Hadi Makkah, Kisha Akahamia Madinah, Mji Wa Mtume, Ambako Alipata Elimu Ya Juu, Kisha Akawa Mhadhiri Katika Chuo Kikuu Cha Madinah
Lakini Elimu Yake Haikubaki Vitabuni Tuu Bali Iliingia Kwenye Moyo, Ikakua Kwenye Msimamo, Na Ikatiririka Kwa Kalamu Na Maneno Ya Haki
Da’wah Ya Salafiyyah: Bega Kwa Bega Na Mitume...
Shaykh Rabii’ Hakujitokeza Kama Mwanaharakati Wa Kisiasa Wala Kama Msemaji Wa Hisia Za Watu Bali Alijitokeza Kama Mfuasi Wa Njia Ya Mitume
Alikuwa Ni Mtu Wa Dalili, Sio Jazba, Mtu Wa Sunnah, Sio Siasa Na Mtu Wa Tawhid, Sio Shirki
Alisimama Wazi Dhidi Ya...
1. Ikhwaan Al-Muslimiin, Waliotanguliza Siasa Mbele Ya Tawhid
2. Qutubiyyah, Waliotukuza Watu Kuliko Qur-Aan
3. Suufiyyah, Waliopamba Bid’ah Kwa Rangi Ya Dhahabu Ing'ae
Kwa Kalamu Yake Kali, Lakini Yenye Adabu, Kwa Sauti Yake Ya Upole, Lakini Yenye Uzito Basi Aliwabainishia Ummah Makundi Haya Kwa Dalili Zilizojaa Uadilifu Na Ucha Mungu.
Jarhu Wa Ta’adil: Fani Iliyo Hai Kwa Shaykh Rabii..
Katika Zama Ambazo Watu Walitaka Kulinda Sifa Za Wenye Bid’ah Kwa Jina La “Hikmah,” Shaykh Rabii’ Alibeba Jukumu La Kuchuja Haki Na Batili Kwa Mizani Ya Salaf.
Shaykh Al-Albani Alisema...
"Shaykh Rabii’ Ndiye Aliyebeba Bendera Ya Jarhu Na Ta’adil Katika Enzi Hizi. Anaitetea Sunnah Na Hupambana Na Watu Wa Bid’ah."
[Silsilatu Al-Huda Wa Al-Nur, 850]
Katika Kalamu Yake Kulikuwa Na Ulinzi Wa Dini; Katika Sauti Yake Kulikuwa Na Mizani Ya Haki
Alikuwa Ni Kizuizi Cha Upotovu, Ngome Ya Manhaj, Na Kioo Cha Salafiyyah Iliyo Safi.
Changamoto: Alivyodhalilishwa Kwa Kusema Haki
Watu Wa Batili Walipopigwa Na Hoja, Walitafuta Hila...
Wakaanza Kusema...
"Shaykh Rabii’ Ni Mkali..."
"Anagawa Ummah..."
"Ameanzisha Kundi La 'Madaakhilah'..."
Lakini Kweli Hujitangaza Yenyewe
Shaykh Rabii’ Alisema:
"Sijaanzisha Kundi... Mimi Ninatetea Sunnah, Ninapinga Bid’ah, Kwa Msingi Wa Njia Ya Salaf. Mtu Akiogopa Hilo, Basi Anapaswa Kumuogopa Allaah Kwanza"
Na Aliyekuwa Karibu Naye, Shaykh Muqbil, Akasema:
"Shaykh Rabii’ Akikwambia Fulani Ni Hizbi, Basi Hakika Utadhihirikiwa Uhizb Wake, Hata Ikiwa Baada Ya Muda."
[Thanaa’ Al-‘Ulamaa’ ‘Alayhi]
Vitabu Vyake: Silaha Za Kifikra
Kalamu Yake Haikuwa Ya Kujikinga, Bali Ya Kushambulia Ujinga Kwa Elimu
Aliandika Zaidi Ya Vitabu 30, Miongoni Mwavyo:
1. Manhaj Al-Anbiyaa Fi Da’wah Ila Allaah
2. Naqdu Kitaab Harakat Al-Ikhwaan Al-Muslimiin
3. Fadha’ih Sayyid Qutb
Kila Kitabu Chake Kilikuwa Kama Mshale Wa Nuru Ukielekeza Moja Kwa Moja Kwenye Qur-Aan Na Sunnah, Ukivunja Minara Ya Bid’ah Na Ujinga Kwa Hoja Zenye Msingi Wa Elimu
Ushuhuda Wa Maulamaa: Mzani Wa Uadilifu
1. Shaykh Ibn Baaz
"Shaykh Rabii’ Ni Miongoni Mwa Maulamaa Wa Ahlus-Sunnah. Hatuna Shaka Juu Ya Elimu Na Msimamo Wake Wa Haki."
2. Shaykh Al-Albani
"Msikilizeni Shaykh Rabii’. Ana Hoja, Ana Elimu, Na Ndiye Aliyebeba Bendera Ya Jarhu Wa Ta’adil."
3. Shaykh Muqbil
"Sijui Katika Zama Hizi Mtu Anayewajua Watu Wa Bid’ah Na Makundi Kuliko Shaykh Rabii’."
4. Shaykh Ibn Uthaymin
"Vitabu Vyake Vina Faida Kubwa Kwa Vijana Wa Ahlus-Sunnah. Nawashauri Wavipitie Kwa Makini."
5. Shaykh Saalih Al-Fawzaan
"Hatukuona Kutoka Kwake Ila Msimamo Wa Haki. Ni Miongoni Mwa Maulamaa Wa Kweli Wa Ahlus-Sunnah."