Sheikh Kassim Mafuta awaasa Waislamu kuilinda amani ya Nchi

Sheikh Kassim Mafuta awaasa Waislamu kuilinda amani ya Nchi

Una uhakika kuwa Sheikh anapindisha Aya kwa maslahi ya watawala? Katika anayofundisha kuna ambayo liko kinyume na Qur'an na Sunnah? Kwa mujibu wa Uislamu Mtawala hakosolewi hadharani wala haombewi Dua mbaya. Na miongoni mwa dalili za watu wa Sunnah ni kuwaombea Dua nzuri watawala. Watawala ni binadamu kama binadamu wengine. Wanakosea na wanapatia.
Naam kuhusu kupindisha aya ni kama hii
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا﴾
[ النساء: 59]

Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.​


Ambapo yeye huitumia kwa viongozi hata wasio waislam(Matwaghuti) kinyume na usahihi wake
 
Ingekuwa vizuri ungeambatanisha na dalili,na sio maneno matupu tu..
Labda unisaidie kuhusu hii hadith

«أَفْضَلُ الْجِهَادِ كَلِمَةُ حَقٍّ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائِرٍ» “Jihad iliyo bora kabisa ni kusema neno la kweli mbele ya mtawala jeuri.”
Hii inakusudiwa ana kwa ana wewe na yeye na si kumsema mbele za watu.
 
Tatizo lako ni kuwa umeweka msimamo kisha unatafuta dalili kuupa nguvu msimamo wako, Usahihi ni kutafuta dalili kisha unaweka msimamo juu ya dalili.
 
Hii inakusudiwa ana kwa ana wewe na yeye na si kumsema mbele za watu.
Wewe naona tayari hizo fikra "zimekulevya" kichwani,yaani badala ya kuleta hoja na dalili wewe unazungumza maneno matupu,na huo ndio "upunda" wenyewe tunaousema,kubebeshwa mizigo mizito kichwani pasi na ufahamu. Ilimradi kutumikia maslahi ya kundi fulani
 
Tatizo lako ni kuwa umeweka msimamo kisha unatafuta dalili kuupa nguvu msimamo wako, Usahihi ni kutafuta dalili kisha unaweka msimamo juu ya dalili.
Sasa hapo ni wewe au mimi? Mwanzoni nilidhani unakusudia mjadala wa kielimu kama ulivyosema,lakini sasa naona umegeuka "comedian" kutoa maneno matupu ilimradi kuleta vituko kwa hadhira,
na hilo ndilo tatizo la huyo bwana mafuta na wafuasi wake kubebeshwa fikra potofu pasi na ufahamu na mkiambiwa "mapunda" mnasema matusi hali ya kuwa hata Allah kalitumia hilo neno,kwa watu mfanowenu,
kubebeshwa mizigo msiyo na ufahamu nayo..
Mm nimejibu hoja kwa kadri ya uwezo alonipa Allah(Azza wajal) lakini wewe naona unatoa maneno matupu tu mradi kujaza server,naona mjadala sasa umekushinda.
 
Kenge wengi ni keyboard warriors...
Waingie rodini tuone ?

1751756837834.png
 
Wewe naona tayari hizo fikra "zimekulevya" kichwani,yaani badala ya kuleta hoja na dalili wewe unazungumza maneno matupu,na huo ndio "upunda" wenyewe tunaousema,kubebeshwa mizigo mizito kichwani pasi na ufahamu. Ilimradi kutumikia maslahi ya kundi fulani
Msimamo sahihi wa Kiislamu juu ya watawala (yaani viongozi wa dola au serikali) ni jambo muhimu sana katika dini ya Uislamu, na limeelezewa kwa kina katika Qur’an, Sunnah, na maelezo ya Maswahaba na Maulamaa wa Salaf (waliotangulia).

Hapa chini ni muhtasari wa msimamo wa Kiislamu kuhusu watawala kwa mujibu wa mafundisho ya Salafus-Swalih:


---

1. Wajibu wa Kuwatii Watawala wa Kiislamu

Mtume (ﷺ) amesema:

"Msikilizeni na kumtii kiongozi wenu, hata kama ni mtumwa wa Kihabashi..."
(Imepokewa na Bukhari na Muslim)



Utiifu kwa viongozi wa Kiislamu ni wajibu kwa mambo ambayo hayapingani na sheria ya Allah. Ikiwa wataamrisha maasi, basi hapana utiifu:

"Hapana utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba."
(Ahmad, Bukhari)




---

2. Haramu Kuasi Watawala, Hata Wakiwa Wenye Dhalimu

Mtume (ﷺ) amesema:

"Yeyote atakayeona jambo ambalo halimpendezi kutoka kwa kiongozi wake, basi na awe na subira, kwani yeyote atakayejitenga na uongozi kiasi cha shibri (kidogo) na akafa katika hali hiyo, amekufa kifo cha kijahili."
(Bukhari na Muslim)



Maulamaa wa Salaf walikubaliana kuwa kuasi watawala na kuchochea uasi ni jambo linaloleta fitna kubwa zaidi kuliko uovu wa kiongozi.


---

3. Kuwanasihi Watawala kwa Siri, Si kwa Kuwafedhehesha Hadharani

Mtume (ﷺ) amesema:

"Mwenye kutaka kumnasihi kiongozi, basi asifanye hadharani, bali amchukue faraghani na amwambie..."
(Ahmad, Ibn Abi ‘Asim)



Hii inaonyesha kuwa njia sahihi ni kushauri kwa hikmah na siri, si kwa maasi au maandamano ya uasi.


---

4. Kuwaombea Dua Watawala

Salaf walikuwa wakiwaombea dua watawala, hata kama walikuwa madhalimu, kwa sababu usalama na utulivu wa nchi unahusiana sana na hali ya uongozi.

Imam Al-Barbahari (rahimahullah) alisema:

"Ukiona mtu anawaombea dua mabaya watawala, jua huyo ni mtu wa bid'aa. Na ukiona anawaombea dua njema, jua huyo ni mtu wa Sunnah."




---

5. Misingi ya Kuwachagua Watawala

Katika Uislamu, kiongozi anatakiwa awe:

Muislamu

Mcha Mungu

Ana elimu ya dini

Ana uwezo wa uongozi


Lakini kama watu watampata kiongozi kinyume na haya (mfano kwa nguvu au uchaguzi mbaya), basi bado anatakiwa kutiwa mradi hajatangaza ukafiri wa wazi.


---

Hitimisho:

Msimamo sahihi wa Kiislamu kuhusu watawala ni:

1.Kuwatii katika mambo ya halali

2.Kuepuka kuwasi na kuwachongea hadharani

3.Kuwanasihi kwa siri

4.Kuwaombea dua njema

5.Kuvumilia dhulma zao kwa subira na kufanya dua.
 
Unaongelea aki gani? Kama unataka haki njoo hapa police kwa dci uyatapike yanayokukereketa. Tena kwa icho kibri ulichonacho uje nacho hivyo hivyo. Uki hisi haliwezekani basi fanya juhudi kuangaika na kutafuta ugali wako. Usifwate shari, wala usi hubiri shari. Yako uliyonayo yanakuitajia kuliko icho unachokikaribisha.
 
Msimamo sahihi wa Kiislamu juu ya watawala (yaani viongozi wa dola au serikali) ni jambo muhimu sana katika dini ya Uislamu, na limeelezewa kwa kina katika Qur’an, Sunnah, na maelezo ya Maswahaba na Maulamaa wa Salaf (waliotangulia).

Hapa chini ni muhtasari wa msimamo wa Kiislamu kuhusu watawala kwa mujibu wa mafundisho ya Salafus-Swalih:


---

1. Wajibu wa Kuwatii Watawala wa Kiislamu

Mtume (ﷺ) amesema:


(Imepokewa na Bukhari na Muslim)



Utiifu kwa viongozi wa Kiislamu ni wajibu kwa mambo ambayo hayapingani na sheria ya Allah. Ikiwa wataamrisha maasi, basi hapana utiifu:


(Ahmad, Bukhari)




---

2. Haramu Kuasi Watawala, Hata Wakiwa Wenye Dhalimu

Mtume (ﷺ) amesema:


(Bukhari na Muslim)



Maulamaa wa Salaf walikubaliana kuwa kuasi watawala na kuchochea uasi ni jambo linaloleta fitna kubwa zaidi kuliko uovu wa kiongozi.


---

3. Kuwanasihi Watawala kwa Siri, Si kwa Kuwafedhehesha Hadharani

Mtume (ﷺ) amesema:


(Ahmad, Ibn Abi ‘Asim)



Hii inaonyesha kuwa njia sahihi ni kushauri kwa hikmah na siri, si kwa maasi au maandamano ya uasi.


---

4. Kuwaombea Dua Watawala

Salaf walikuwa wakiwaombea dua watawala, hata kama walikuwa madhalimu, kwa sababu usalama na utulivu wa nchi unahusiana sana na hali ya uongozi.

Imam Al-Barbahari (rahimahullah) alisema:






---

5. Misingi ya Kuwachagua Watawala

Katika Uislamu, kiongozi anatakiwa awe:

Muislamu

Mcha Mungu

Ana elimu ya dini

Ana uwezo wa uongozi


Lakini kama watu watampata kiongozi kinyume na haya (mfano kwa nguvu au uchaguzi mbaya), basi bado anatakiwa kutiwa mradi hajatangaza ukafiri wa wazi.


---

Hitimisho:

Msimamo sahihi wa Kiislamu kuhusu watawala ni:

1.Kuwatii katika mambo ya halali

2.Kuepuka kuwasi na kuwachongea hadharani

3.Kuwanasihi kwa siri

4.Kuwaombea dua njema

5.Kuvumilia dhulma zao kwa subira na kufanya dua.
Sasa naona umeanza kujitahidi kuongea kielimu,sasa swali linakuja,mtawala wa kiislam ni yupi?
 
Sasa naona umeanza kujitahidi kuongea kielimu,sasa swali linakuja,mtawala wa kiislam ni yupi?
Mtawala wa Kiislamu ni:
1.Muislamu
2.Ana mamlaka juu ya Waislamu
3.Anahukumu kwa Uislamu (au sehemu zake)
4.Hajatangaza ukafiri wa wazi
5.Anatakiwa kutiiwa katika mambo ya halali

"Kiongozi ni ngao, watu hupigana nyuma yake na hujilinda naye."
(Bukhari, Muslim)

Katika nchi mchanganyiko:
*Ikiwa Waislamu ndio wengi, na wana uwezo wa kuongoza – mtawala lazima awe Muislamu.

*Ikiwa Wakristo ndio wengi, au dola si ya Kiislamu – hali huwa ngumu, na Waislamu wanatakiwa kuwa na subira, na kuhifadhi dini yao kwa hekima hadi watakapopata fursa ya kujiendesha kwa Sharia.
 
Mtawala wa Kiislamu ni:
1.Muislamu
2.Ana mamlaka juu ya Waislamu
3.Anahukumu kwa Uislamu (au sehemu zake)
4.Hajatangaza ukafiri wa wazi
5.Anatakiwa kutiiwa katika mambo ya halali


(Bukhari, Muslim)

Katika nchi mchanganyiko:
*Ikiwa Waislamu ndio wengi, na wana uwezo wa kuongoza – mtawala lazima awe Muislamu.

*Ikiwa Wakristo ndio wengi, au dola si ya Kiislamu – hali huwa ngumu, na Waislamu wanatakiwa kuwa na subira, na kuhifadhi dini yao kwa hekima hadi watakapopata fursa ya kujiendesha kwa Sharia.
Shida unaandika kimatamanio,ndio tatizo linapoanzia..ikhlaasw itawale ndio mjadala utaleta natija na sio ujaujanja na kubumba
Maanake umeandika tu hoja pasi na dalili zaidi ya kutoa maoni yako binafsi.
Umeshasema mjadala wa kielimu sasa mbona waandika vitu visivyo na ithibati?
 
Niko tayari kukosolewa ndugu yangu. Ikiwa una maelezo tofauti na haya. Niambie usahihi ni upi?
 
Maelezo mengi pitia kitabu kiitwacho Sharhu Sunnah Cha Imaam Barbahaariy(Sharhu ya Sheikh Fawzaan,Allaah amhifadhi)
 
Niko tayari kukosolewa ndugu yangu. Ikiwa una maelezo tofauti na haya. Niambie usahihi ni upi?
Usahihi ni kuwa uislam umesisitiza Twaa kwa mtawala lakini ni yule anayetawala kwa sheria zake,na ndio maana aya imemalizia kuwa mnapohitilafiana katika jambo mlirudishe kwake na mtume wake (3:59)
Kwa hivyo hizo hoja za kumtii mtawala yoyote hata asiyehukumu kwa sheria zake ni upotofu mkubwa wanoufanya hilo pote la kina Kasim Mafuta pasipokujali kuwa kuna siku ya hukm ambapo tutahukumiwa kwa kila jambo!
Kwa hivyo usahihi ni kuwa mtawala anayepaswa kutiiwa ni yule anayehukumu kwa sheria zake tu bali yule asiyehukumu kwa sheria za Allah ni Twaghut,kwani amechukua cheo cha Allah cha kutaka kuabudiwa na anapaswa kupingwa kwa nguvu zote

بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ لَا انفِصَامَ لَهَا ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

“Basi atakayemkanusha Twaaghuut na akamuamini Allaah, hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika na Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote.”[2:256]
 
Niko tayari kukosolewa ndugu yangu. Ikiwa una maelezo tofauti na haya. Niambie usahihi ni upi?
45. Maana ya Twaaghuut
Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Allaah Ameutumia kila Ummah Mtume, kuanzia kwa Nuuh mpaka kwa Muhammad, ili kuwaamrisha kumuabudu Allaah Peke Yake na akiwakataza shirki. Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):
وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ
“Hakika Tulituma katika kila ummah Mtume [awaamrishe watu wake] kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na Twaaghuut.”” (Ibraahiym 16:36)
Allaah amewafaradhishia viumbe vyote kukanusha Twaaghuut na badala yake kumuamini Allaah. Ibn Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:
“Twaaghuut ni kila chenye kuabudiwa, kinachofuatwa au kutiiwa ambacho mja anapindukia mipaka yake.”
Twawaaghiyt ni wengi. Wakubwa wao ni watano:
Ibliys, Allaah amlaani.
Yule mwenye kuabudiwa hali ya kuwa yuko radhi kwa hilo.
Yule mwenye kuwaita watu katika kumuabudu.
Yule mwenye kudai kujua kitu katika elimu ya ghaibu.
Yule asiyehukumu kwa yale aliyoteremsha Allaah.
Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):
لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ ۖ قَد تَّبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ ۚ فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ لَا انفِصَامَ لَهَا ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
“Hapana kulazimisha katika Dini, kwani imekwishabainika kati ya Uongofu na upotofu. Basi atakayemkanusha twaaghuut na akamwamini Allaah kwa hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika, na Allaah ni Mwenye kusikia, Mjuzi wa yote.” (al-Baqarah 02:256)
MAELEZO
Twaaghuut ni kila chenye kuabudiwa badala ya Allaah na kikaridhika na hilo. Kadhalika kila yule mwenye kuhukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah au akalingania katika hilo. Twaaghuut imetokamana na neno الطغيان na ni kule kuvuka mpaka.
Twaaghuut ni yule anayevuka mpaka ima kwa shirki yake na kufuru yake au akalingania katika hayo yaliyotajwa. Mbaya wao kabisa ni Ibliys, Allaah amlaani. Vilevile inahusiana na kila yule mwenye kuwaita wengine wamuabudu yeye au akaridhia wengine wamuabudu yeye badala ya Allaah, kama alivyofanya Fir´awn na Namruud. Pia anaingia humo kila yule mwenye kudai kujua mambo yaliyofichikana. Mfano wa hao ni makuhani, wapiga ramli na wachawi, katika kipindi cha kishirikiana na baada ya kuja Uislamu. Kadhalika anaingia humo yule mwenye kuhukumu kinyume na yale aliyoteremsha Allaah kwa kukusudia. Hawa ndio wakubwa wa Twawaaghiyt. Kila yule ambaye atavuka mpaka na akaacha kumtii Allaah ni Twaaghuut.
Allaah (Ta´ala) amesema:
لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ ۖ قَد تَّبَيَّنَ الرُّشْدُ مِنَ الْغَيِّ
“Hapana kulazimisha katika Dini, kwani imekwishabainika kati ya Uongofu na upotofu.”
Uongofu ni Uislamu na yale yote aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Upotofu ni kufuru na upotevu. Amesema (Ta´ala):
فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ
“Basi atakayemkanusha twaaghuut na akamwamini Allaah.”
Kukufuru Twaaghuut ina maana ajitenge nayo mbali na aitakidi kuwa ni batili. Anatakiwia kujiweka mbali na shirki. Kumuamini Allaah ina maana asadikishe kuwa Allaah ndiye muabudiwa Wake na kwamba ndiye mungu wa haki, aamini Shari´ah na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ajisalimishe na hayo. Mwenye kufanya hayo ndiye muumini. Halafu (Ta´ala) akasema:
فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ لَا انفِصَامَ لَهَا ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
“… atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika, na Allaah ni Mwenye kusikia, Mjuzi wa yote.” (02:256)
Bi maana ameshikilia kishikilio madhubuti, nayo ni hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah. Anayefanya hivo ameshikilia kishikilio madhubuti kisichovunjika. Mwenye kushikamana kikweli na shahaadah na akawa na msimamo juu yake atafikia Pepo na furaha. Shahaadah ina masharti yake; Allaah peke yake ndiye anatakiwa kuabudiwa, ndiye anatakiwa kutiiwa na Shari´ah Yake inatakiwa kufuatwa.
Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye Mtume na Nabii wa mwisho. Yeye ndiye Mtume wa Allaah kwa walimwengu wote; majini na watu wote. Ni wajibu kwa kila yule ambaye ´ibaadah ni yenye kumuwajibikia kumtii yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kufuata Shari´ah yake. Hairuhusiwi kwa yeyote kuacha kumfuata. Shari´ah yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) imefuta Shari´ah zote zilizotangulia hapo awali. Amesema (Ta´ala):
قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا
“Sema: “Hakika mimi ni Mtume wa Allaah kwenu nyinyi nyote.”” (07:158)
Kabla yake amesema (Subhaanah):
فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنزِلَ مَعَهُ ۙ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ
”Basi wale waliomwamini na wakamtukuza na wakamnusuru na wakafuata Nuru iliyoteremshwa pamoja naye, hao ndio wenye kufaulu.” (07:157)
وَمَن يَكْفُرْ بِهِ مِنَ الْأَحْزَابِ فَالنَّارُ مَوْعِدُهُ
”Atakayeikanusha kati ya makundi, basi Moto ndio mahali pa miadi yake.” (11:17)
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth Swahiyh:
”Ninaapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mkononi Mwake hakuna myahudi wala mnaswara yeyote katika Ummah huu atayesikia kuhusu ujio wangu kisha asiamini yale niliyotumwa nayo, isipokuwa atakuwa katika watu wa Motoni.”[1]
Kuna Aayah na Hadiyth nyingi kama hizo juu ya hilo. Wanachuoni wote wamekubaliana juu ya kwamba haifai kwa yeyote katika Ummah huu kuacha Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba yule mwenye kuonelea hivo ni kafiri.
[1] Muslim (153).
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 58-59
Imechapishwa: 15/02/2017
 
4. Kuwaombea Dua Watawala

Salaf walikuwa wakiwaombea dua watawala, hata kama walikuwa madhalimu, kwa sababu usalama na utulivu wa nchi unahusiana sana na hali ya uongozi.


A man mentioned the tyrant Al-Hajjaj to Imam Ahmad, saying, “Let him be cursed!” Ahmad said, “I do not like for it to be uttered.” Then, Ahmad said, “Surely, the curse of Allah is upon the wrongdoers.” (11:18)

al-Sunnah li-Abī Bakr al-Khallāl 851

Shaykh al-Islam Ibn Taymiyyah commented, “Ahmad is known to have disapproved of cursing specific people by name, such as Al-Hajjaj ibn Yusuf and their likes, but rather he would say as Allah Almighty said: Surely, the curse of Allah is upon the wrongdoers.” (11:18)

Minhāj al-Sunnah 4/569
 
Back
Top Bottom