Sheikh Kundecha akemea Maudhui ya Twitter ( X ) hususani chapisho la Maria Sarungi, awataka Waislam kuikataa Twitter (X)

Sheikh Kundecha akemea Maudhui ya Twitter ( X ) hususani chapisho la Maria Sarungi, awataka Waislam kuikataa Twitter (X)

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Na Mwandishi wetu.

Mwenyekiti Jumuiya na Taasisi za Kiislaam nchini Tanzania, Shekhe Mussa Kundecha amefunguka na kukemea wazi wazi kitendo cha Mwanaharakati wa mitandaoni Maria Sarungi kuweka chapisho la Picha za Kumdhihaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu na kusema picha hizo sio tu zinamdhihaki Rais bali zinadhihaki Vazi la kislaam na Waislam wote.

Ambapo katika Chapisho hilo Maria Sarungi alituma picha ya Chura akiwa amevaa vazi la Hijab, jambo ambalo ni sawa na kuikashifu na kutukana jamii ya Waislamu Tanzania na Duniani kiujumla.

Shekh Mussa Kundecha amemtaka Maria Sarungi afute chapisho hilo haraka sana kabla wauumini wa dini ya kislamu hawajaungana kwa pamoja kushitaki kwa MwenyeziMungu juu ya jambo hilo ambalo halina taswira nzuri kwa waumini wa Dini ya Kiislamu.

 
Kwahiyo angepost kwenye ubao fulani wa shule tungekataa shule?

Na Hijab ndio uislamu? Na kama anataka kutoa taswira ya Samia angeweka chura amevaa kapelo au dreads tungejua vipi kwamba ni Samia?

Nadhani aliyelikoroga ni yule aliyesema watu wazibe masikio na kujifanya vyura wakati wanaolalamika ndio mabosi wao na wanawalipa mishahara...

Hatulipi kodi ili watu wakajigeuze kuwa Vyura
 
TOKA MAKTABA

Mapito ya mwanaharakati sheikh Kundecha kutoka enzi zake za kuichachafya serikali hadi leo kuwa mdau mkubwa wa kuitetea kidete

Sheikh Mussa Kundecha asimulia kashikashi nyingi alizopitia akiwa mwanaharakati Tanzania

View: https://m.youtube.com/watch?v=rDaa_3GLI2Y&

Kiongozi wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu asimulia jinsi alivyopewa kesi ya mauaji baada ya kutoafikiana na Polisi waliolazimisha aongee mbele ya vyombo vya habari kituo cha Polisi awaombe Waislamu waliokuwa na mpango wa kuandamana wasifanye hivyo. ...

Wakati huo Polisi Dar es Salaam mkuu wa upelelezi mkoa ni RCO Abdallah Zombe anaongoza .... nikatupwa selo asubuhi mahakamani nikasomewa kesi ya mauaji ya watu wawili kwa risasi mmoja askari polisi na mwingine raia, kutoka hapo nikapelekwa rumande Segerea miezi 6 ....

Kuhusu siasa Sheikh Mussa Kundecha anasema huwezi tenganisha siasa na dini.

Upande wa elimu anaelezea umuhimu wa suala hilo ... nilisoma Tabora kisha kwenda nje Burundi, Kenya, Saudi Arabia kuongeza elimu nikarudi Tanzania nikafundisha Tabora, Arusha na Dar es Salaam mitaa wa Kiungi Magomeni pia Kinondoni Mkwajuni na msikiti wa Kichangani Magomeni.

Mihadhara ya MwembeChai iliyoshamiri kuanzia mwaka 1994 hadi 1997 jijini Dar es Salaam iliniletea matatizo miaka hiyo ikiongozwa na kina sheikh Mazinge na wengine ...

Pia nilifanya kazi ya kuunganisha waislamu ambao ni wasomi (professionals) wa elimu pana ya kisecular na masheikh wa wanaotoa elimu ya dini, kwani makundi haya mawili yaani professionals wa kiislamu waliona masheikh wao hawana ufahamu wa masomo ya elimu ya secular huku pia masheikh wakiona waislamu wasomi kuwa hawana ufahamu wa dini yao.

Harakati hizi zimeleta mafanikio kuna misikiti zaidi ya 3,000 na huku kuna shule zaidi ya 300 za waislamu kutokana na kuunganisha nguvu za waislamu ....

Mussa Kundecha anaulizwa sheikh ni nani hasa ... pamoja ya kuwa sheikh ni kama inatumika kuonesha kuwa ni mtu mzima isipokuwa katika utaratibu ....

Sheikh Mussa Kundecha akiangalia mbele kuhusu kupata elimu ya dini, anashukuru kuwa mazingira yanazidi kuwa mazuri vitabu vipo vingi tofauti na zamani hapa Tanzania kilikuwapo kitabu kimoja cha Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy .. sasa kuna vingi zaidi ...

Kuhusu BAKWATA - Baraza Kuu La Waislamu Tanzania kutokubaliwa na baadhi ya waislamu, Sheikh Mussa Kundecha anasema kila mmoja ana nafasi yake hivyo ...

Wateja wengi wa Islamic Banking Tanzania ni wale wasio waislamu na wamewapita kwa idadi kubwa huku waislamu wakiwa wachache hivyo ni jambo jema la kijamii kwa wasio waislamu kuwa wengi sana kwa idadi ktk Benki za Kiislamu ...anabainisha Sheikh Kundecha..


KUTOKA MAKTABA :

10 August 2023
WAISLAM WAIKAANGA SERIKALI MTAALA ELIMU YA DINI "KUHUSU BANDARI WAMETUITA KWANINI SIO HILI".



Viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania viongozi wake Sheikh Ponda, Sheikh Kundecha, Sheila Suleiman Daudi, Sheikh Abdallah Mrisho na Sheikh Hassan Abbas wametoa taarifa kwa umma juu ya mstuko wao mpango wa serikali kujichukulia jukumu la kuisimamia dini na kuifundisha dini baada ya kutoa mtaala wake kuanzia angazi ya kindergarten hadi vyuo vya ualimu.

Habari kwa kina:

Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar

Taasisi na jumuiya za kiislamu Tanzania, haikubaliani na hatua ya Serikali kusimamia dini ya kiislamu na kuifundisha

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 10, 2023, Amiri Jumuiya na Taasisi za Kislamu Tanzania Alhajj Sheikh Musa Kundecha, amesema wamepokea kwa masikitiko makubwa kwamba,Serikali sasa imekwishaandaa silabasi za masomo ya dini na kuondoa mambo yote ya imani ya dini inayohusiana na dini hizo.

Amesema kwamba katika kikao chao cha Julai 23/7/2023 kilichofanyika Masjid EFA viongozi wa jumuiya na taasisi za kislaam walipokea kwa mstuko mkubwa taarifa kwamba Serikali sasa inasimamia dini na kufundisha.


“Mstuko huu unakuja katika ukweli kwamba kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu, serikali haina dini na kuwa mambo ya dini yapo nje ya utendaji wa Serikali na kila dini itasimamia mafunzo ya dini yake na kwa kuzingatia kwamba dini na masomo yake yalipangwa kwa pamoja baina ya taasisi za dini na Serikali kupitia vitengo vyake vya elimu na kuandaa silabasi na vitabu vya kufundishia” amesema Sheikh Kundecha.

Sheikh Kundecha amesema kwa mujibu wa historia ya masomo ya dini na kufundishwa kwake,ilikwishatokea Serikali kuingilia masomo ya dini na wasilamu kupinga kuingiliwa huko hatimaye kukubalika masomo ya dini yataandaliwa kwa pamoja baina ya wananchi na Serikali na kupatikana silabasi na vitabu kuanzia ngaizi ya wali hadi vyuo vya ualimu.

”Sasa jambo hili linatulazimisha kuamini kuwa serikali inakuja na mfumo wa dini mpya, ikizingatiwa kwamba dini yetu ya kiislamu na serikali ipo tofauti kubwa za misingi”amesema Shekhe Kundecha.

Ametoa mfano kwenye Serikali kuna pombe zote ni halali, wakati katika uislamu pombe zote ni haramu.

Shekhe Kundecha amesema kutokana na uzito wa jambo hilo,walilazimika kumuandikia Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, kumuomba kukutana ili kulingalia jambo hilo kwa mustakabali wa taifa letu barua ambayo ilifika ofisini kwake Julai 25,2023 lakini mpaka sasa hawajaitwa wala kujibu barua hiyo.

“Serikali yenyewe haina dini na sasa imeandaa, mafundisho ya dini ya kiislamu na kuondoa mambo yote ya kiimani dini ya uislamu bila imani hakuna dini sasa sisi tunaomba waziri akutane nasi ili kujenga mustakabali mwema wa nchi yetu,” amesema
 
Kwahio angepost kwenye ubao fulani wa shule tungekataa shule ?

Na Hijab ndio uislamu na kama anataka kutoa taswira ya Samia angeweka chura amevaa kapelo au dreads tungejua vipi kwamba ni Samia ?

Nadhani aliyelikoroga ni yule aliyesema watu wazibe masikio na kujifanya vyura wakati wanaolalamika ndio mabosi wao na wanawalipa mishahara...

Hatulipi kodi ili watu wakajigeuze kuwa Vyura
Hivi hiyo kauli ya chura aliitoa nani!?
 
Back
Top Bottom