Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum atenguliwa

Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum atenguliwa

Taasisi kubwa kama ile halafu haina "programmed decision making" hata atakayeweka hapo atakuwa anafanya maamuzi kwa utashi wake na siyo kwa maslahi mapana ya Taasisi na lengo kuu la taasisi.

Hiyo itaendelea kuleta misuguano kati ya wahanga wa maamuzi ya viongozi.
 
evidence?
IMG-20230202-WA0012.jpg
 
Itakuwa tafrani kubwa sana, atautaka umufti kabisa
 
Tatizo siasa, mtu gani yupo activitie kwenye mambo ya kijamii ya kawaida kabisa lakini ya kiroho ni mzito sana.

Hapa pia bado naona namna ya kupatikana kwa viongozi wa kanisa haswa wakatoliki ni bora kidogo kuliko upande mwingine.

Kumbe huko unateuliwa na kutenguliwa!
 
Baada ya baraza la maulamaa kukaa kikao kuanzia jana tarehe 1 Februari na kufikia leo tarehe 2 Februari likiwa chini ya Mwenyekiti wake Mufti ma Sheikh mkuu wa Tanzania Abubakar Zubeir. Limefikia uamuzi wa kutengua uteuzi wa Sheikh Alhad Mussa Salum na nafasi yake itachukuliwa na Sheikh Waliid Alhad Omar ambaye ni imamu mkuu wa msikiti wa kichangani.

Ikumbukwe malalamiko yalikuwa mengi juu ga Alhad na kufikia watu kuona baraza la masheikh aliloliongoza lilienda kihuni. Haikuishia hapo hivi karibuni likaibuka suala la Dokta Mwaka na mkewe, ambalo liliingiliwa naye na kutoa maamuzi ya kuvunja ndoa ilihali hakuwa na mamlaka ya kulishughulikia jambo lile kabisa achilia mbali kuvunja hiyo ndoa.

Bado alikwenda kinyume na kulishutumu baraza la Ulamaa ambalo kiuongozi nchi nzima lipo chini ya Mufti mwenyewe akiwa Mwenyekiti wake.

IMG-20230202-WA0003.jpg
 
Uamuzi huo umefikiwa baada vikao vya siku mbili vilivyofanywa na Baraza la Ulamaa la Baraza Kuu la Kiislamu Tanzania (BAKWATA) chini ya Mwenyekiti wake, Mufti Mkuu, Abubakar Zubeir

Uteuzi wa Sheikh Alhad Mussa Salum umetenguliwa kuanzia kuanzia Februari 2, 2023 ikiwa ni siku chache baada ya Baraza hilo kutengua uamuzi wa Sheikh huyo wa kuvunja Ndoa ya Dkt. Mwaka

Sheikh Mkuu Dkt. Abubakar Zubeir bin Ally amemteua Sheikh Walid Alhad Omar kukaimu nafasi ya Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam kuanzia Februari 2, 2023.
IMG_20230202_212752_974.jpg
 
Back
Top Bottom