Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum atenguliwa

Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum atenguliwa

Amfuatee mwenziee Kimaro likizo isiyo na kikomoo.....

Ila shehe siku si nyingi atakuja na tiba yake mbadala kwenye tv, radio na mitandao na atapiga watu helaa na maisha yataendeleaa....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wamechelewa sana.

Wakati Mange anaanika uchafu wake na wanawake wakajitokeza kumuomba asiendelee kuwaweka mitandaoni kwani yamepita na wao ni wake za watu kwa sasa

Hapo walitukosea sana kumuacha na kuongoza watu akiwa mchafu

Kama ni kweli basi wamepata mganga au wameingia wanao muogopa Mungu haswa

Mtu akishukiwa tu na mabaya ni lazima aondoke
Huwezi kuwa na dhana ya aina yoyote kama wewe ni kiongozi
 
Uamuzi huo umefikiwa baada vikao vya siku mbili vilivyofanywa na Baraza la Ulamaa la Baraza Kuu la Kiislamu Tanzania (BAKWATA) chini ya Mwenyekiti wake, Mufti Mkuu, Abubakar Zube...
Uamuzi wa kumtengua Sheikh Alhad umekuja ikiwa imepita wiki moja tangu, kiongozi huyo alipotangaza kuivunja ndoa hiyo ya mtaalamu wa tiba mbadala, Juma Mwaka Juma maarufu kwa jina la Dk Mwaka na mkewe Queen Masanja Januari 25 mwaka huu, kufuatia ombi la mwanamke huyo kudai talaka.

Hata hivyo, siku mbili baadaye, yaani Januari 27, Baraza la Ulamaa lilikutana kwa dharura na kubatilisha uamuzi huo.

Akisoma taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu wa baraza hilo, Hassan Chizenga leo Februari 2, 2023, Mjumbe wa Baraza hilo, Issa Othman alisema umetokena na kikao chao cha Februari 1 na 2, mwaka huu amesema uamuzi huo umefuatia kikao chake kilichofanyika Februari 1 na 2 jijini hapa chini ya Mwenyekiti wake, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dk Abubakar Zubeir bin Ally.

“Baraza la Ulamaa katika kikao chake kilichofanyika Februari 1 na 2 jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dk Abubakar Zubeir bin Ally limetengua uteuzi wa Sheikh Alhad Mussa Salum kama Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam kuanzia leo Februari 2, 2023,” amesema.

Ameendelea kusema kuwa Mufti na Sheikh Mkuu, amemteua Sheikh Walid Alhad Omar kukaimu nafasi ya Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam kuanzia leo Februari 2, 2023.
 
Duuuh mbombo ngafu naloli

Screenshot_20230202-212239.png
 
Khatari sana, mtu wa amani ametolewa !




Toka maktaba :

19 January 2023
Dar es Salaam, Tanzania

SHEIKH ABUU - HATARI INAKUJA TUSIPOTOA TAHADHARI KWA MADHEHEBU HAYA MAWILI



Sheikh Abuu Iddi ambaye ni Msaidizi wa Mufti wa Tanzania ametoa tahadhari hiyo kwa kuwa inaweza kupelekea amani kuvunjika nchini Tanzania.

Sheikh Abuu Iddi CV (wasifu) yake imesheheni nyadhifa kadha wa kadha ktk utumishi kwa dini na jamii kwani yeye ni imamu mkuu msikiti wa Masjid Mnyamani Buguruni jijini Dar es Salaam. Pia kwa miaka 16 amekuwa akiendesha kipindi ktk kituo cha televisheni cha Channel Ten kutoa daawa na darsa, mratibu Al Risala Foundation, Mratibu wa Kudumisha Amani katika mkoa wa Dar es Salaam, Mwandishi wa kitabu kinachokwenda kwa jina Misingi 15 ya amani, mwandishi wa makala katika gazeti kubwa la Mwananchi pia ni Mshauri wa dini na jamii wa Mufti Mkuu wa Tanzania.

Sheikh Abuu Iddi ameelekeza tahadhari hii hususan kwa madhehebu ya Sunni na Shia yanayo shambuliana kupitia majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii wakiongozwa na viongozi wao.

Amewataja Sheikh Mziwanda na Samir wa upande wa Sunni huku upande wa madhehebu ya Shia kupitia Sheikh Hemed Jalala, Sheikh Abdul na wenzie watatu wakijitetea.

Na pande hizi mbili za madhehebu haya yakinukuu kile wanachoamini kwamba ni sawa kwa upande wa madhehebu yao.

Pande hizo zimewekuwa zikirushiana maneno yanayotishia amani za kila aina mfano amani ya viungo, amani ya roho, kuvunjiana heshima n.k huku wote wa pande hizi mbili wakiwa na wafuasi wao hivyo kutishia amani kwa ujumla ya Tanzania maana wafuasi wa pande hizi mbili zinaweza kukabiliana kutetea pande zao na viongozi wao .

Mfumo wa uendeshaji wa mijadala hii imeleta ukakasi mkubwa huku maneno ya kutishiana uhai baina ya pande hizo yakitamkwa asema Sheikh Abuu Iddi kwa masikitiko makubwa.

Sheikh Abuu Iddi anasisitiza kuwa BAKWATA ni ya kwa ajili ya madhehebu yote na hivyo haiwezekeni dhehebu moja kuzuiwa kuja ktk shughuli za BAKWATA kama inavyochagizwa na baadhi ya waumini kuwa viongozi wa madhehebu ya Mashia watengwe...... Source :

 
UTV wanalipoti muda huu kuwa shekhe mkuu wa mkoa wa Dar es salaam alhaji ISSA salimu ametolewa kwenye nafasi yake sio tena shekhe wa mkoa


Baraza la waislamu BAKWATA limfuta kazi kutokana na mienendo isiyofaa aliyoionesha tangu siku za nyuma na kufuatia kulumbana na baraza la Maulamaa

Juzi vyombo vya habari hapa nchini vilimnukuu akisema yeye augombani uongozi wa juu wa BAKWATA wa kitaifa


Huu isiwe ile vita na mke wa mtu na wale Maulamaa walivyomkalia kooni

USSR
View attachment 2504080
Atateuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya
 
Kwa bongo kuna raia jamaa watamuona ni shujaa wao [emoji1][emoji38]
 
Huyu alikuwa mnafiq sana na alifkia hatua ya kumsifia Magufuli kuwa yeye zaidi ya Yesu Kristo,ni zaidi ya Mtume Mohammed SAW na kumalizia kuwa Magufuli ni zaidi ya Mungu. Huyu hapa
 
Back
Top Bottom