Sheikh Mkuu wa Tanzania: Muislam hajiendei endei tu,bila amani na utulivu hatuwezi kufanya Ibada zetu na kuishi vyema

Mkunazi Njiwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2023
Posts
8,538
Reaction score
7,559
Amani na utulivu..

Ametuasa TUSIJIENDEE ENDEE tu....tusifuate mambo bila kujua undani wake.....

Tusipelekwe pelekwe tu kwani Uislam unataka tutumie vyema matumizi ya akili.....

Amesema ,tufahamu UMUHIMU WA AMANI na UTULIVU katika nchi.

#Nchi Kwanza😍
#Uwe na uchungu na nchi yako 😍
 
Mkuu umeelewa alichokizungumza Mufti?
Fafanua
Amani na utulivu..

Ametuasa TUSIJIENDEE ENDEE tu....tusifuate mambo bila kujua undani wake.....

Tusipelekwe pelekwe tu kwani Uislam unataka tutumie vyema matumizi ya akili.....

Amesema ,tufahamu UMUHIMU WA AMANI na UTULIVU katika nchi.

#Nchi Kwanza😍
#Uwe na uchungu na nchi yako 😍
 
Nafuatilia sherehe za mazazi ya Bwana Mtume Muhammad (SAW) zinazofanyika mkoani Geita.

Nimemsikiliza Mufti wa BAKWATA Sheikh Zuberi, ambaye ameongea mengi na zaidi kaongelea suala la amani.

Ingawa sio moja kwa moja, ila amewasihi waislamu wasijihusishe na kurukia mambo (kwa uelewa wangu alikuwa analenga maandamano yaliyotangazwa na Chadema).

Nchi yetu ipo katika mtanzuko wa utekaji na mauaji. Nilitegemea leo aweze kukemea tabia hii, lakini amepiga kimya kama hakuna kinachoendelea.
 
BAKWATA ilianzishwa na Serikali kwa nia ya kuwadhibiti waislam kuhusiana na mambo ya kisiasa, na imeendelea hivyo mpaka leo.

Kuitegemea BAKWATA itoe kauli dhidi ya mambo yanayofanywa na Serikali ya CCM, ni sawa na kusubiria UVCCM itoe kauli dhidi ya uovu unaofanywa na Serikali ya CCM.
 
Nchi yetu ipo katika mtanzuko wa utekaji na mauaji. Nilitegemea leo aweze kukemea tabia hii, lakini amepiga kimya kama hakuna kinachoendelea.
Inawezekana huko kuteka na kuua baadhi ya waTanzania ambao hawapo upande anao ukubali yeye ndiyo amani yenyewe na kupendana!

Mambo ya aina hii wala hayahitaji kisomo kukubwa mtu awe nacho kuyatambua. Akili ya utu tu, ubinaadam inatosha kumfahamisha mhusika yeyote mazuri na mabaya
 
. BAKWATA ni sawa na UVCCM na UWT, zote ni taasisi za CCM
Na ukichambua kwa karibu zaidi haya maneno machache kuhusu CCM ilipo sasa utagundua kuwa matatizo yanaanzia na kuhusika moja kwa moja na uhusiano huo. Ndani ya CCM siku hizi uongozi hauendani na uwezo wa mtu, bali ni "uwenzetu" baina yetu. Na imekuwa hivyo hivyo hata ndani ya serikali..
 
BAKWATA ilianzishwa na Serikali kwa nia ya kuwadhibiti waislam kuhusiana na mambo ya kisiasa, na imeendelea hivyo mpaka leo.
Hili la "kudhibiti" silielewi vizuri; lakini fikiria pia hali ingekuwaje wakati huu ndani ya nchi hii kama hizi dini zote zingeachwa zifanye kivyao kuhusu uhusika wao na maswala ya siasa!
Tatizo ninalo ona ni kwa CCM kuwa shikilia kwa karibu zaidi hao BAKWATA kwa kuwa na hofu na wale ambao wapo nje ya BAKWATA. Sasa imekuwa kama BAKWATA ndio wameiteka CCM!
 
Back
Top Bottom