Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Naunga mkono hoja, kwa lugha nyingine ni Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu amepiga marufuku Waislamu kushiriki maandamano ya Chadema!.Amani na utulivu..
Ametuasa TUSIJIENDEE ENDEE tu....tusifuate mambo bila kujua undani wake.....
Tusipelekwe pelekwe tu kwani Uislam unataka tutumie vyema matumizi ya akili.....
Amesema ,tufahamu UMUHIMU WA AMANI na UTULIVU katika nchi.
#Nchi Kwanza😍
#Uwe na uchungu na nchi yako 😍
Hii maana yake ni the "the status quo" imetishika na maandamano haya sasa inawatumia viongozi dini kuwatisha waumini wao. Mtashuhudia viongozi mamluki wa dini, wakiingiza siasa mimbarini na madhabahuni!.
Jana nimemsikia Mufti akizunguka zunguka na kujiuma uma kulitangaza hili ikiwa ni kiashiria amechomekewa!.
Nakumbuka enzi zangu niko newsroom, ile uchaguzi wa 2010 awamu ya pili ya JK, Mzee wa Msoga alikuwa na hali mbaya, ikabidi kutumika rescue strategies kuwatumia viongozi wa dini kusaidia kuokoa jahazi, na kiukweli walisaidia sana , vinginevyo jahazi lingezama! Elections 2010 - Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?
P