Sheikh Mkuu wa Tanzania: Muislam hajiendei endei tu,bila amani na utulivu hatuwezi kufanya Ibada zetu na kuishi vyema

Sheikh Mkuu wa Tanzania: Muislam hajiendei endei tu,bila amani na utulivu hatuwezi kufanya Ibada zetu na kuishi vyema

Amani na utulivu..

Ametuasa TUSIJIENDEE ENDEE tu....tusifuate mambo bila kujua undani wake.....

Tusipelekwe pelekwe tu kwani Uislam unataka tutumie vyema matumizi ya akili.....

Amesema ,tufahamu UMUHIMU WA AMANI na UTULIVU katika nchi.

#Nchi Kwanza😍
#Uwe na uchungu na nchi yako 😍
Sasa kama katoa ujumbe wa mafumbo hivyo unamgusa nani? Si kila mmoja ataona haumhusu, au kalenga mahali fulani? Ujumbe lazima ulenge audience (hadhira). Kama ujumbe ni kwa X, then exclude Y au kama ni kwa X na Y, then tuonyeshe hivyo.
 
BAKWATA ilianzishwa na Serikali kwa nia ya kuwadhibiti waislam kuhusiana na mambo ya kisiasa, na imeendelea hivyo mpaka leo.

Kuitegemea BAKWATA itoe kauli dhidi ya mambo yanayofanywa na Serikali ya CCM, ni sawa na kusubiria UVCCM itoe kauli dhidi ya uovu unaofanywa na Serikali ya CCM.
CCT na TEC ikaanzishwa na waumini baada ya hiyo BAKWATA kuanzishwa na serikali ?!! 😲😲

Hoja dhaifu sana mzee wangu....

Taasisi zote zina ITHIBATI na leseni kutoka serikalini....

Nitajie taasisi ambayo haina leseni halali kutoka serikalini ?!!

Lini serikali imekuwa mbaya kuyasimamia maslahi ya taifa letu?!!

Lini ?!!
 
Sasa kama katoa ujumbe wa mafumbo hivyo unamgusa nani? Si kila mmoja atapona haumhusu, au kaulenga mahali fulani? Ujumbe lazima ulenge audience (hadhira). Kama ujumbe ni kwa X, then exclude Y au kama ni kwa X na Y, then tuonyeshe hivyo.
Nimemsikiliza vyema....

Kauli ya Quran "enyi waumini muwe makini-ulil al baab".
...."enyi waumini hamtafakari-afalaa yatafakkarun".

".... pindipo inapowajia hoja ichunguzeni kwanza ili msije mkadhuru wasio na hatia...".

👆👆👆👆👆

Mufti amepita humo.....una jengine ?!!

#Nchi Kwanza😍
#Amani na utulivu 😍
 
BAKWATA ilianzishwa na Serikali kwa nia ya kuwadhibiti waislam kuhusiana na mambo ya kisiasa, na imeendelea hivyo mpaka leo.

Kuitegemea BAKWATA itoe kauli dhidi ya mambo yanayofanywa na Serikali ya CCM, ni sawa na kusubiria UVCCM itoe kauli dhidi ya uovu unaofanywa na Serikali ya CCM.
Bakwata pale kinondoni walikuwa wanapeperusha BENDERA ya CCM
 
...mtume SAW amezaliwa "mwezi 12 mfunguo sita" na leo ndio tunamuadhimisha....ulitaka mufti ayasemee hayo kabla ya tarehe hii?!!😲

Uislam hautaki mtu kujiendea endea tu....
Wakati watu wanatekwa na kuuwawa, yuko kimya,. Sasa sijui hui ndio uislamu?!
 
Amani na utulivu..

Ametuasa TUSIJIENDEE ENDEE tu....tusifuate mambo bila kujua undani wake.....

Tusipelekwe pelekwe tu kwani Uislam unataka tutumie vyema matumizi ya akili.....

Amesema ,tufahamu UMUHIMU WA AMANI na UTULIVU katika nchi.

#Nchi Kwanza😍
#Uwe na uchungu na nchi yako 😍
Hawa ndiyo huwa wanatamba wemepigania uhuru wa Tanganyika....ni vichekesho tu....ila ya Gaza yanawauma saana
 
waislamu wa siku hizi waoga waoga sana, mbna kna Muhhamad waliingia vitani kupigania haki "Jihad"
 
Hawa ndiyo huwa wanatamba wemepigania uhuru wa Tanganyika....ni vichekesho tu....ila ya Gaza yanawauma saana
Makabila yote yalipigania Uhuru wa Tanganyika....makabila hayo yako ndani ya TEC ,yako ndani ya BAKWATA na taasisi nyinginezo.....

Masuala makubwa hayataki fikra za "kibubusa"....
 
Si kweli....

BAKWATA ni taasisi yetu waislamu kwa ajili ya maslahi yetu ya kidini.....acha "kujiendea endea "....
#Nchi Kwanza😍
Bakwata iliasisiwa na Mwenyeheri Julius Kambarage Nyerere 😂 wa Kanisa Moja Takatifu La Mitume 🌹 Ili kulinda Amani!
 
Naunga mkono hoja, kwa lugha nyingine ni Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu amepiga marufuku Waislamu kushiriki maandamano ya Chadema!.

Hii maana yake ni the "the status quo" imetishika na maandamano haya sasa inawatumia viongozi dini kuwatisha waumini wao. Mtashuhudia viongozi mamluki wa dini, wakiingiza siasa mimbarini na madhabahuni!.

Jana nimemsikia Mufti akizunguka zunguka na kujiuma uma kulitangaza hili ikiwa ni kiashiria amechomekewa!.
Nakumbuka enzi zangu niko newsroom, ile uchaguzi wa 2010 awamu ya pili ya JK, Mzee wa Msoga alikuwa na hali mbaya, ikabidi kutumika rescue strategies kuwatumia viongozi wa dini kusaidia kuokoa jahazi, na kiukweli walisaidia sana , vinginevyo jahazi lingezama! Elections 2010 - Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

P
Nami nilishuhudia hii strategy and it worked well in his favour. Taifa kwanza undugu uje baadaye, hata kama ni mwenzako akikisoea mwambie ukweli ndipo utakuwa unamsaidia ili ajisahihishe.
 
waislamu wa siku hizi waoga waoga sana, mbna kna Muhhamad waliingia vitani kupigania haki "Jihad"
....mtume SAW aliporejea vitani ,akawaambia maswahaba wake (radhiAllahu anhumma) kuwa "tumetoka katika Jihad ndogo* na tunaelekea katika jihad kubwa*....

Jihad kubwa * ni jihad ya nafsi....nafsi....nafsi.....nafsi....

Yaani mathalani kupinga vita UZINZI....USHOGA....ULAWITI....USAGAJI.....
 
Naunga mkono hoja, kwa lugha nyingine ni Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu amepiga marufuku Waislamu kushiriki maandamano ya Chadema!.

Hii maana yake ni the "the status quo" imetishika na maandamano haya sasa inawatumia viongozi dini kuwatisha waumini wao. Mtashuhudia viongozi mamluki wa dini, wakiingiza siasa mimbarini na madhabahuni!.

Jana nimemsikia Mufti akizunguka zunguka na kujiuma uma kulitangaza hili ikiwa ni kiashiria amechomekewa!.
Nakumbuka enzi zangu niko newsroom, ile uchaguzi wa 2010 awamu ya pili ya JK, Mzee wa Msoga alikuwa na hali mbaya, ikabidi kutumika rescue strategies kuwatumia viongozi wa dini kusaidia kuokoa jahazi, na kiukweli walisaidia sana , vinginevyo jahazi lingezama! Elections 2010 - Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

P
QURAN TUKUFU INAMTAKA MUISLAM KUWA MAKINI SANA LINAPOKUJA JAMBO

Katika Quran, kuna aya inayosema kuhusu umuhimu wa kuchunguza habari kabla ya kuzipokea au kueneza. Aya hiyo inapatikana katika sura ya 49, aya ya 6:

"Enyi mliyoamini! Ikiwa mja mmoja kutoka kwenu anakuja na habari, ithibitisheni kwa uangalifu, ili msije mkawadhulumu watu kwa kukosea, na kisha mkawa wenye huzuni kwa yale mliyofanya."
Aya hii inasisitiza umuhimu wa kufanya uchunguzi na kuthibitisha ukweli wa taarifa kabla ya kueneza au kuamua juu yake. Hii ni kanuni muhimu kwa ajili ya kuhakikisha usahihi na haki katika maamuzi na vitendo vyetu.
 
Hivi huyo sheikh ana elimu gani nje ya elimu ya dini?
sio hoja ya msingi. dini X tunaambiwa nchi hii nido wenye alimu , lkn siku zote tunalalamika maisha magumu na rushwa imeenea na utekaji. swala hio elimu ya dini X imesaidia nini?
 
Amani na utulivu..

Ametuasa TUSIJIENDEE ENDEE tu....tusifuate mambo bila kujua undani wake.....

Tusipelekwe pelekwe tu kwani Uislam unataka tutumie vyema matumizi ya akili.....

Amesema ,tufahamu UMUHIMU WA AMANI na UTULIVU katika nchi.

#Nchi Kwanza😍
#Uwe na uchungu na nchi yako 😍
Comments reserved
 
Back
Top Bottom