Sheikh Mkuu Zuberi jenga shule kubwa badala ya misikiti mikubwa

Sheikh Mkuu Zuberi jenga shule kubwa badala ya misikiti mikubwa

Ndipo hapa tunapokwama... Kwa nini visijengwe vyote? Hii ndiyo inafanya waumini wanashindwa kujitegemea kimaisha kwani maisha ya dunia ya leo yanahitaji shule/elimu dunia. Juzi nilikuwa kwenye sala ya Eid, huwezi amini michango ya waumini kwa ajili ya kuboresha msikiti haikufika haya laki mbili wakati waumini wake kwa waume walijaza kiwanja kikubwa kabisa jirani na msikiti. Hii maana yake waumini hawana fedha na stable employments. Matokeo yake ni viongozi wa misikiti kugombea sadaka na mali za misikiti. Pia kwa viongozi wa BAKWATA inakuwa rahisi kurubuniwa kifedha na mali na wanasiasa, hivyo kushindwa kutetea Waislamu.
Soma Dini uelewe ulicho andika hakihusiani kabisa na kusoma,umeandika kutoa,suala la kutoa ni mtu husika kujua wajibu wako. Wapo watu hawajasoma "secular" na wana hela. Mola wetu muadilifu sana mzee. Amejaalia rizki katika njia nyingi sana.
 
Taasisi ya Roman Catholic wana chuo kikuu. Kinaitwa St Augustine University, kipo Mwanza.

Taasisi ya Lutheran(KKKT) ina chuo kikuu, kinaitwa Tumaini University. Kina matawi mikoa mingi sana TZ.( KCMC ni tawi mojawapo la Tumaini University)

Taasisi ya Anglican ina chuo kikuu kinaitwa St John University kipo Dodoma.

Taasisi ya SDA(Wasabato) wana chuo kikuu kinaitwa University of Arusha, kipo Arusha.

TAAAISI ZA KIISLAM ZINA NINI?

Bado tu hujaona tatizo mlilonalo waislam kwenye kuipa elimu kipaumbele?
Tuna Moslem University of Morogoro (MUM) mkuu...
 
Sio waisilamu tu, Hata wakiristo.
Wako busy kujenga makanisa, vishule vya watoto wao vipo hovyo.
Waislamu na wakiristo wote waamke akili, waache tabia ya mkoloni ya kuwadumaza akili misikitini na makanisani.
Watu wote tuboreshe shule zinazotuzunguka, kwa kweli ni kama magofu, hizo saint ni chache tu na wala sio tegemeo ka jamii kubwa bali wachache tu.
Wachungaji ba mashehe hawzhawahi kuitisha harembee ta shple zinaziwazunguka bal kuongeza majengo.
Tanzania haina uhaba wa misikiti na makanisa ila shule, hospitali na vifaa vyake.
Uliposema na Wakristu ulimaanisha na Wakatoliki? Unazifahamu shule zao au unasimuliwa?
 
Tuna Moslem University of Morogoro (MUM) mkuu...
Kuanzia walivyopewa hicho chuo,hawajawahi kupska hata Rangi ha majengo, pia Wana campus moja Mtwara,
Lakini SAUT ambao walipewa kwa siku mmoja pale Malimbe Mwanza,chuo wamekipanua Sana ,pia wamefungua campus kalibu kila mkoa,
Hebu nitajie Hospital ya Rufaa hata moja inayomil kiwa na waisilam
 
Tuna Moslem University of Morogoro (MUM) mkuu...
Sasa waislam mna chuo kikuu kimoja miaka 60 baada ya uhuru.

Wakristo wana vyuo vikuu 5 miaka 60 baada ya uhuru.

Bado huoni tatizo tu hapo?
 
Hayo na wewe ni mawazo yako, usiwasemee Waislamu. Kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake, kama umechefukwa ina maana hupendi mawazo mbadala kama ilivyo kwa viongozi wa BAKWATA. Hoja ya msingi iliyotolewa ni kwamba hapa duniani elimu ya kuyakabili maisha na kupata stadi za maisha ni muhimu. Tukienda misikitini tunatakiwa kusaidia ujenzi wa misikiti na madrasa, sasa tutaludanyaje hilo ikiwa hatuwekezi kwenye shule na vyuo ili waumini wapate ujuzi wa kuajiriwa, kujiajiri na hata kuajiri Waislamu wenzao? Hata biashara au viwanda au kilimo cha kisasa vyote vinahitaji elimu, sasa wewe tatizo unaliona wapi hapo? Kuna kipindi Waislamu walikuwa vinara wa kulalamika kuachwa nyuma kwenye uongozi wa nchi kuanzia wabunge, mawaziri, makatibu wakuu na nafasi nyingine. Je bila elimu ya kutosha rais atawachaguaje kumsaidia kuongoza nchi?? Inaonekana Mkapa alivyofanya uamuzi wa kukigeuza chuo cha Tanesco pale Msamvu Morogoro kuwa chuo kikuu cha Waislamu roho yako ilikuuma sanaaaaa maana Waislamu watakuwa hawaendi misikitini na kwenye madrasa (kwa mtazamo wako) si ndiyo?? Unafahamu faida waliyoipata Waislamu kwa uwepo wa chuo hicho cha MUM shehe wangu???
Yaani unalinganisha Elimu ya Kiislamu na Elimu ya Kikafir? Wewe upo vizuri kichwani kweli? Sidhani. Elimu hii iliyotengenezwa na makafir unataka ndo tukae kuhangaika nayo badala ya kusoma dini tuifahamu vizuri na namna ya kuishi katika njia zake allah. Wewe siyo bure. Na wewe huwezi kuwa muislam hakuna muislam wa kuwaza namna hii. Unapaswa uombe toba. Chuo alikitoa mkapa kinasaidia nini? Angekuwa anatupenda waislamu si engetujengea msikiti mkubwa hapo Morogoro au Mkoa mwingine. Hicho chuo ni lengo lile lile la makafir kutuondoa kwenye reli. Tukasome ukafir wao.
 
Hiyo simu unayotumia imetengenezwa kutokana na elimu ya Kikafir.
Hata hii JF unayoitumia ni matokeo ya elimu ya Kikafir.

Au unadhani Simu zinatengenezwa kwa Elimu akhera?

Unaonaje ukaachana na hiyo simu na mitandao hii inayotokana na elimu ya makafir?
 
Yaani unalinganisha Elimu ya Kiislamu na Elimu ya Kikafir? Wewe upo vizuri kichwani kweli? Sidhani. Elimu hii iliyotengenezwa na makafir unataka ndo tukae kuhangaika nayo badala ya kusoma dini tuifahamu vizuri na namna ya kuishi katika njia zake allah. Wewe siyo bure. Na wewe huwezi kuwa muislam hakuna muislam wa kuwaza namna hii. Unapaswa uombe toba. Chuo alikitoa mkapa kinasaidia nini? Angekuwa anatupenda waislamu si engetujengea msikiti mkubwa hapo Morogoro au Mkoa mwingine. Hicho chuo ni lengo lile lile la makafir kutuondoa kwenye reli. Tukasome ukafir wao.
Kwa akili hizi Wakristo wataendelea kuwatawala milele
 
Ni rahisi tuu, anza na wewe mwenyewe na rafiki zako : mlivyokuwa shule ya msingi ratio ya Wakristo Vs waislam ilikuwaje? Sekondari ikawaje? University ikawaje? Etc....
Ok.
Shule ya msingi mkristo mmoja na muslims 44.
Secondary school wakristo 12 na muslims 33.

Right now bado nasoma nikimaliza secondary nitaleta takwimu za university.

Sasa wewe leta takwimu za kitaifa kati ya Muslims na wakristo.....?
 
Kutawala nini?

This is some kind of religious hypocrisy.
Sasa kama muislam mwenzako hapo juu kwenye comment yake anaita elimu ya darasani ni elimu ya Kikafir, si mtatawaliwa na wakristo milele? (ambao hiyo elimu ya darasani anayoiita ya Kikafir wakristo wanaipa kipaumbele kuliko kawaida)
 
Almost 50 percent of the whole tanzania population are Muslims.

Yaani kabisa unadhani mtu mmoja tu (1) jamiiforums.
anaweza leta impact yoyote kwenye watu ambao ni karibu nusu ya taifa zima?

Unadhani kabisa hicho kitu kinawezekana?

Bado hujajibu hili swali.

Kutawaliwa kwenye nini?
 
Uliposema na Wakristu ulimaanisha na Wakatoliki? Unazifahamu shule zao au unasimuliwa?
Huko vijijini vishule vinavyozunguka jamii achana na hizo chache za kulipia. shule nyingi ni zile za kata. Zinafuatia za watu binafsi kundi la mwisho ni hizo za dini wala si nyingi kivile kiasi cha kuweza ku accomodate majority of christian.
Nimekaa sana vijiji vya wakiristo wengi nyanda za juu kusini.
Ni watu wachache tu ndio wenye uwezo wa kupeleka shule bora za kulipia wengi wanaenda kayumba na kuishia kupata maziro.
 
Ok.
Shule ya msingi mkristo mmoja na muslims 44.
Secondary school wakristo 12 na muslims 33.

Right now bado nasoma nikimaliza secondary nitaleta takwimu za university.

Sasa wewe leta takwimu za kitaifa kati ya Muslims na wakristo.....?
Takwimu inategemea na ukanda.
Huwezi niambia Tanga kuwe na wanafunzi wengi wakiristo kuliko waislamu.
Mbeya kuwe na wanafunzi wengi waislamu kuliko wakiristo, haiwezekani.
Jadilini kuboresha maisha ya Watanzania achaneni na hizi habari hazina tija yoyote.
Uwe msilamu uwe mkiristu, you have to struggle to achieve.
 
Sasa waislam mna chuo kikuu kimoja miaka 60 baada ya uhuru.

Wakristo wana vyuo vikuu 5 miaka 60 baada ya uhuru.

Bado huoni tatizo tu hapo?
Yaani hata kulinganisha tu Waislam na Wakristo katika maendeleo ya kielimu Tanzania unakosea sana.

Yaani in tofauti kama Giza na Nuru

Waislam wanatuzidi tu kusoma juzuu na kutawadha
 
Sio waisilamu tu, Hata wakiristo.
Wako busy kujenga makanisa, vishule vya watoto wao vipo hovyo.
Waislamu na wakiristo wote waamke akili, waache tabia ya mkoloni ya kuwadumaza akili misikitini na makanisani.
Watu wote tuboreshe shule zinazotuzunguka, kwa kweli ni kama magofu, hizo saint ni chache tu na wala sio tegemeo ka jamii kubwa bali wachache tu.
Wachungaji ba mashehe hawzhawahi kuitisha harembee ta shple zinaziwazunguka bal kuongeza majengo.
Tanzania haina uhaba wa misikiti na makanisa ila shule, hospitali na vifaa vyake.
Mtaa Nina oisho Mimi pale Moro Kuna shule za kikristo kama 6 hivi na hakuna hata moja ya kiislamu

Huo mfano tosha

Angalia hapo ulipo Hali ikoje.

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Idadi ya wiaslamu wako kwenye vyuo vikuu, ofisi za umma na sehemu zote za utumishi ni ndogo sana kulinganisha na watu wa dini nyingine.

Bila shaka pamoja na mambo mengine ya kihistoria, imani, ukabila, ukanda na kiuchumi lakini idadi ndogo ya watoto wa kiislamu kwenye vyuo vikuu ukilinganisha na watoto wa dini nyingine inaweza kuwa sababu ya msingi ya shida hii

Badala ya kuwaza kujengewa misikiti mingi na mikubwa weka jitihada zako kwenye kujenga shule na vyuo vingi ambako watoto wengi wa kiislam watapata ilmu dunia pia. Elimu hii ndiyo inayotoa wahandisi, madaktari, wauguzi, walimu, marais, mawaziri, wakurugenzi na watumishi wengine.

Fanya sensa ya watumishi kwenye kila wizara, ofisi, shule Na vyuo vya umma Na binafsi ujionee hali ilivyo. Pitapita huko uone idadi ya walimu wa vyuo vikuu huko.

Mazoezi ya kuhifadhi Qur'an yaende sambamba na mazoezi ya kuhifadhi hisabati Na fizikia kwenye madrasa zao.

Kama viongozi wa ofisi mbalimbali wengi ni wa dini fulani bila shaka watumishi wanaotegemea maoni yao kwenye kuajiliwa na kuteuliwa kwenye nafasi mbalimbali bila shaka watakuwa kama wa dini za wanaowateua. Like dissolve like.
Shule watasoma za Katoliki
 
Back
Top Bottom