Kumbuka BAKWATA ni Baraza kuu la Waislamu Tanzania,zipo Taasisi nyingi za kiislamu,zina shule, vyuo.Na Taasisi hizo ziko Tanzania nzima.Zipo zinazomiliki zaidi ya shule tatu,na zaidi ndani ya mkoa mmoja.
Uislamu uko tofauti na ukristo,kuwa ukristo umegawanyika,na kutofautiana mambo mengi katika ibada,lakini katika uislamu nyingi ya taasisi katika ibada ziko sawa.,ndio ikawa wengi wasio kuwa waislamu,wanashindwa kutofautisha baina ya BAKWATA na Taasisi za kiislam,na kujuwa kuwa BAKWATA ni kiongozi katika uislamu,Tanzania,katika uislamu ziko tasisi nyingi,lakini hazitofautiani katika ibada,ndio ukaona katika kuomba dua,za kitaifa,anakuja Sheikh mmoja tu,kuwakilisha Taasisi zote za kiislamu,Swala zinasaliwa bila utofauti,siku ya ijumaa,waislamu wote wanaswali ijumaa,hakuna wanaoswali jumamosi au jumapili kama wakristo walivogawanyika,waislamu wote wanakwenda Hija mji mmoja wa Maka,kwenye Qur'an wote wanafuata Qur'an hiyo hiyo,hawana utofauti,kama katika ukristo kila dhehebu lina Biblia yake.
Kwa hiyo jua,ziko Taasisi nyingi za kiislamu Zina shule zao pia,mbali na BAKWATWA.
Kuna Taasisi kama Istiqama,ina shule zake Tanzania nzima,kuna Islamic Foundation,Wana shule zao ,kuna African Muslim Agency(direct aid),Wana shule zao,kuna Maawah Islamia,kuna Answar muslim,Wana shule zao,kuna Jumuia ya kuhifadhisha Qur'an,Wana shule zao,kuna Ilala Islamic,wana shule zao,Nk ni Taasisi nyingi,hapo hatujagusa madhehebu mengine,kama Shia,Bohora,Aghakhan,Suni Jamaat nk