Sheikh Mkuu Zuberi jenga shule kubwa badala ya misikiti mikubwa

Kulinganisha taasisi za kikristo na kiislamu katika kumiliki shule/ vyuo ni ujinga. Mfano mi nipo Arusha, shule za kiislamu hazizidi 5, na hakuna chuo. Wakati wakristo wana shule zaidi ya 100 na vyuo vya kutosha..sasa unashindanisha Nini hapo. Na tena shule za kiislamu ndio zinaongoza kufelisha ukilinganisha na seminary. Waislamu bado sana, acha kujipa moyo..
 
Wewe uko eneo lenye waislamu wachache,nenda maeneo yenye waislamu wengi,hamia mikoa hiyo.Ukaone shule na vyuo na wanafunzi wanavyosoma wa kiislamu.Kwa mfano iko wilaya ina waislamu,na wilaya ndogo,lakini ina shule za kiislamu zinafika 8,hapo hujahesabu shule za serekali,ambazo watoto wa kiislamu wanasoma kwa idadi kubwa,tembea,hapo sijamalizia wilaya nyingine,zinazofika 8,huko pia kuna shule za kiislamu.
 
Kama wapi? Dar nimekaa, Pwani nimekaa, Tabora naijua. Ni mkoa gani shule za kiislamu zinaweza zidi za wakristo?
 
Kama wapi? Dar nimekaa, Pwani nimekaa, Tabora naijua. Ni mkoa gani shule za kiislamu zinaweza zidi za wakristo?
Kiuhalisia idadi ya shule zinazoendeshwa na Christianity ni nyingi kushinda Islam maeneo mengi sana, same applies to hospital/health centers.

Pia ninapenda kugusia hili suala la uwepo wa Muslim wenye vyeti vikubwa. Kwa uwazi baadhi ya watu wizara ya elimu wamekuwa wakiwaangusha watu wenye mlengo wa Islam au wenye utambulisho chimbuko la Mashiriki ya kati/Arabs.
 
Wanawaangusha vp Wakati mitihani inafanywa kwa namba?
 
Poa.
 
Lakini Waislamu ndio matajiri wakubwa hapa nchini sijui nao wamependelewa na nani, na pia kwenye makampuni yao asilimia 90 ya wanaoajiriwa ni Waislamu nadhani ungeanzia huko kwanza mkuu.
 
Kama Bakwata haitaacha kuwa chombo cha kisiasa waislamu watakuwa wasindikizaji milele kwenye taifa lao. Hali ya waislam inatisha sana, kuna taasisi za umma zinafungua mikutano yao kwa sala kwakuwa wengi ni dini moja tu.
Mkuu marehemu Malima alikuwa na '' msikiti wake'' pale hazina na vivyo hivyo Dau pale NSFF sasa ni yupi na afadhali na yule anayeanzia salamu au yule aliyegeuza ofisi kuwa msikiti. Pale NSFF enzi za Dau mbona mlijaa na watu hawakulalamika?
 
Kujenga msikiti na madrasa zitazosomesha Qur'aan na Sunnah ni bora mara elfu kuliko kujenga shule.
Kwa mawazo haya, wakristo wataendelea kuwatawala siku zote.

Wakatoliki/Wakristo wakijenga kanisa, pembeni wanajenga Hospitali na Shule.
 
Kwa akili hizi mtaendelea kutawaliwa na mifumo ya wakristo milele.
 
Kama Bakwata haitaacha kuwa chombo cha kisiasa waislamu watakuwa wasindikizaji milele kwenye taifa lao. Hali ya waislam inatisha sana, kuna taasisi za umma zinafungua mikutano yao kwa sala kwakuwa wengi ni dini moja tu.
Pumbavu mkubwa wewe Toka hapa
 
Usipende ubishi wa kitoto na WA kijinga naenda udsm, mzumbe, sua fanya observation utaona watu wa upande upi ni wengi swala sio kuponda waislamu hapana, lakin sio wengi kwenye elimu za juu
 
Taasisi zote hizo idadi ya shule zao haziwezi hata kulingana na idadi ya shule za taasisi moja ndogo tu ya Kikristo niliyoitolea mfano hapo,TAG (Tanzania Assembies of God).

Hapo sijataja taasisi kubwa kama RC,KKKT,Anglican,SDA etc...

Yaani waislam hamna taasisi inayoweza kushindana na taasisi ya dhehebu moja tu la kikristo..Wewe huoni tatizo hapo?

Kuna taasisi yoyote ya kiislam inayomiliki shule angalau ROBO ya idadi ya shule zinazomilikiwa na Roman Catholic?
 
Taasisi ya Roman Catholic wana chuo kikuu. Kinaitwa St Augustine University, kipo Mwanza.

Taasisi ya Lutheran(KKKT) ina chuo kikuu, kinaitwa Tumaini University. Kina matawi mikoa mingi sana TZ.( KCMC ni tawi mojawapo la Tumaini University)

Taasisi ya Anglican ina chuo kikuu kinaitwa St John University kipo Dodoma.

Taasisi ya SDA(Wasabato) wana chuo kikuu kinaitwa University of Arusha, kipo Arusha.


TAAAISI ZA KIISLAM ZINA NINI?

Bado tu hujaona tatizo mlilonalo waislam kwenye kuipa elimu kipaumbele?
 
Hayo yote yatawezekana iwapo wataamua kujiendesha kisasa, Kuanzia viongozi wa juu hadi wangazi za mitaa. Otherwise nothing will happen
 
Ndio maana nikakuambia,usifananishe uislamu na ukristo,ukristo umegawanyika kimadhehebu sana,hapo hizo madhehebu za kikristo,zimejenga vyuo tofauti kutokana na ibada zao ziko tofauti,hawezi wanafunzi wa dhehebu moja kusoma kwenye dhehebu jingine.
Lakini angalia katika uislamu,Muislamu yoyote anaweza akasoma chuo cha Aghakan,au akasoma MUM(Muslim University of Morogoro),bila kuwa kinyume na ibada zinazofanyika hapo chuoni.
Wala kuwa na vyuo vingi ndio ubora wa elimu,kinachotizamwa ni quality(ubora) sio quantity(wingi).
 
Huu utetezi wa kijinga ndio unafanya mpaka leo hii muendelee kuwa wa Mwisho kwenye elimu.

Unasema "haiwezekani wanafunzi wa dhehebu moja wakasoma kwenye dhehebu lingine", hivi huko kwenye shule/vyuo huwa wanafundishwa mafundisho ya dhehebu au Elimu ya darasani!!

Kila taasisi ina anzisha shule zake kwa sababu TAASISI ZA KIKRISTO ZINATHAMINI ELIMU, na kila taasisi INA KIPAUMBELE KIKUBWA SANA CHA ELIMU na Inawekeza kwenye Elimu.

Kama huu ndio utetezi mnaokuja nao,mtaendelea kuongozwa na wakristo milele.
 
Wewe jamaa unachekesha sana.

Eti "muislam yoyote anaweza kusoma MUM".

Kwani mkristo yoyote hawezi kusoma chuo cha dhehebu lingine la kikristo?Kule wanafundisha masomo ya madhehebu?
We jamaa unaongea utopolo gani?

Vyuo vya katoliki(SAUT kwa mfano) wanasoma wakatoliki tu? Hakuna Walutheri,Wasabato,Walokole mule??

KCMC(Chuo kishiriki cha Tumaini cha KKKT) wanasome Walutheri tu? Hamna Wakatoliki, Wasabato,Walokole etc mule?

Mimi ni mlutheri, nimesoma chuo cha katoliki...na nilikuwa Very comfortable. Na pale tulikuwa watu wa madhehebu yote mpaka Waislam walijazana pale.

Narudia, Kama akili zenu ndio hizi za kwenye hii comment,basi mtaendelea kuongozwa na wakristo milele
 
Unazungumzia Roman Catholic au kanisa la Gwajima? Naomba tutofautishie kidogo hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…