PostGE2025 Sheikh Ndauga: Vijana msidai haki bila kutimiza wajibu wenu, tusikubali tofauti za kidini zituhukumu

PostGE2025 Sheikh Ndauga: Vijana msidai haki bila kutimiza wajibu wenu, tusikubali tofauti za kidini zituhukumu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Rais wa Umoja wa Wanazuoni Tanzania (Hay-Atul Ulamaa), Sheikh Abdallah Ndauga, ametoa wito mahsusi kwa vijana kote nchini kujitokeza kudai haki zao kwa njia ya ustaarabu, lakini bila kusahau wajibu wao kama nguzo muhimu ya ujenzi wa taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari tarehe 17 Novemba 2025 kufuatia matukio yaliyojitokeza wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, Sheikh Ndauga amesema kuna haja kubwa kwa vijana kutojiingiza kwenye ghasia, uharibifu au vurugu, kwani “serikali zinakuja na kuondoka, lakini nchi inabaki pale pale.”

“Kila haki ina wajibu. Msidai haki zenu huku mkisahau wajibu wenu kama vijana wa Tanzania,” amesisitiza Sheikh Ndauga, akiongeza kuwa kundi hilo linapaswa kuwa ‘nuru ya taifa, si giza lake’.

Sheikh Ndauga amesema vijana wana nafasi ya kuleta mabadiliko chanya, lakini mabadiliko hayo yanapaswa kuongozwa na hekima, uadilifu na uzalendo. Ametahadharisha kwamba chuki, uhasama, vurugu na mauaji haviwezi kuwa mbegu za kujenga taifa bora.

Aidha, Sheikh huyo ametoa wito mpana kwa makundi yote nchini- wanasiasa, viongozi wa dini, taasisi za kiraia, vyombo vya dola, pamoja na wananchi kuunga mkono wito wa maridhiano unaoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema maridhiano ni zaidi ya neno linalotamkwa kirahisi, bali ni safari ya kusikilizana, kutathmini makosa, kusameheana kwa dhati na kuanza upya bila chuki.

Sheikh Ndauga pia amelitaka Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuendesha majukumu yao kwa busara, kuepuka matumizi ya nguvu kupita kiasi, na kuzingatia kinga ya raia na misingi ya haki.

Vilevile ameshauri kuanzishwa kwa mfumo wa kudumu wa majadiliano ya kitaifa kati ya Serikali, viongozi wa dini, wanasiasa na vijana ili kuzuia migogoro kabla haijazidi na kuvuka mipaka


 
Wajibu wetu ni kulipa kodi,tumeshatekeleza
 
Back
Top Bottom