#COVID19 Sheikh Ponda Issa Ponda aunga mkono waraka wa KKKT na Kanisa Katoliki kuhusu kujikinga na Corona

#COVID19 Sheikh Ponda Issa Ponda aunga mkono waraka wa KKKT na Kanisa Katoliki kuhusu kujikinga na Corona

View attachment 1702454

Sheikh Ponda ambaye ni miongoni mwa Masheikh wanaoheshimika sana na Waislam wa Africa kutokana na kupigania haki za Waislam bila uoga , amesema Juhudi za Makanisa kuwaelekeza waumini wao njia bora za kujikinga na Corona haziwahusu waumini hao pekee , bali zinawahusu wananchi wote wa Tanzania .

Amewaasa wananchi wote kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa hatari wa Corona .

Chanzo : MwanaHalisi Digital

Kuna mmoja hapa hata naogopa kusema “korona tanzania hakuna”
 
Inategemea sijui anamaanisha nini maana tangia uchaguzi uishe mpaka leo hajawahisikika sijui kaona nini? Ila tuendelee kuchukua taadhali.
 
Masheikh UBWABWA wa bakwata kimyaaaaaa swala la Watanzania kujikinga na corona wao haliwahusu.
View attachment 1702454

Sheikh Ponda ambaye ni miongoni mwa Masheikh wanaoheshimika sana na Waislam wa Africa kutokana na kupigania haki za Waislam bila uoga , amesema Juhudi za Makanisa kuwaelekeza waumini wao njia bora za kujikinga na Corona haziwahusu waumini hao pekee , bali zinawahusu wananchi wote wa Tanzania .

Amewaasa wananchi wote kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa hatari wa Corona .

Chanzo : MwanaHalisi Digital
 
Watu wenye ushawishi kama hawa wanapoamua kuingilia kati mambo haya wanazidi kuwaamsha raia
How? Ina maana watu hawajiangalii sababu serikali haijasema? Mbona watu wa kawaida wanapeta na wanaendeleza libeneke? Huu ugonjwa hauna fundi so far. Kila mtu lazima ajiangalie vizuri
 
Shehe wa kweli wa kiislamu anayesimamia ukweli wa Mungu, na sio kama shehe Mkuu na wa mkoa wa Dar ambao ushehe wao ni kwa ajili na ccm na ubaradhuli wao wote
1660090_FB_IMG_1514731600839.jpg
 
Safi Sana Shekhe wetu sijajua Shekhe was Dar kasemaje
 
"Niponde nisiponde?, maalim Pondaaa"

What's up Nash MC.

-Kaveli-
 
View attachment 1702454

Sheikh Ponda ambaye ni miongoni mwa Masheikh wanaoheshimika sana na Waislam wa Afrika kutokana na kupigania haki za Waislam bila uoga amesema Juhudi za Makanisa kuwaelekeza waumini wao njia bora za kujikinga na Corona haziwahusu waumini hao pekee, bali zinawahusu wananchi wote wa Tanzania.

Amewaasa wananchi wote kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa hatari wa Corona .

Chanzo: MwanaHalisi Digital
Afya haina dini asante sheikh
 
Sisi waislamu, tunamshukuru Allah kutupatia Sheikh Ponda.

Ushauri wangu kwa Sheikh Ponda, achana na siasa za kichama, wewe ni wa umma wote suo wa ACT wala Chadema, wewe ni wa Watanzania wote. Jenga msimamo wako, tunahitaji kiongozi wa kiislamu jasiri kama wewe, sio wale vilaza wa Bakwata.
 
Huyu muzee ndio Kiongozi wa Dini (Sheikh)! Sio wale masheikh feki!
 
Lisu hana hamu naye huyo Ponda alimlaghai akala pesa yake kuwa anamtafutia mashehe wa kuloga Magufuli asishinde Tundu Lisu akampa mamilipni ya pesa za kuwalipa hao mashehe mwisho wa siku akashindwa

Shehe Ponda tapeli wa kutupwa anayebisha amuulize Tundu Lisu
 
Back
Top Bottom