Sheikh S. Mwaipopo: Hoja ya watu wa Mtwara juu ya gesi ni Upuuzi!

Sheikh S. Mwaipopo: Hoja ya watu wa Mtwara juu ya gesi ni Upuuzi!

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
5,426
Reaction score
3,309
BARAZA la Habari la Kiislamu Tanzania (BAHAKITA), limesema hoja ya watu wa Mtwara kutaka gesi iwanufaishe wao kwanza ni upuuzi, kwa kuwa hoja hiyo itajenga ukanda katika Tanzania isiyoamini mgawanyiko wa kikabila. Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa BAHAKITA, Shekhe Said Mwaipopo.

Alisema kitendo cha watu wa Mtwara na wengine kutoka nje ya Mtwara, kusema gesi hiyo ni yao ni kitendo cha kukosa busara. "Tukianza kugawana mafungu si kitu kizuri. Leo hii watu wa Mwanza wanasema maji yao yasiende Shinyanga hadi wao wayatumie, Wazaramo nao waseme watu wote ambao si wa Dar es Salaam watoke, si hoja ni upuuzi na kauli za kichochezi," alisema Mwaipopo.

Aidha, aliwaonywa baadhi ya wanasiasa na viongozi wa dini wanaotoa kauli za kichochezi na kusema watu hao wamefilisika kisiasa.

"Hawa viongozi wa kisiasa hususani wa Chadema wamefilisika kisiasa, ni wanasiasa uchwara na mbaya zaidi wenyewe wamekiri kupitia Katibu wao Mkuu Dk. Wilbroad Slaa kuwa vitendo vinavyofanywa na watu wa Mtwara ni matokeo ya M4C. "Lakini cha kushangaza ndani ya CCM pia wapo viongozi wakubwa akiwamo Mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnein Murji ambaye alitoa kauli hadharani za kuchochea vurugu za watu wa Mtwara kwa kuwaunga mkono kuwa gesi ni ya kwao.

"Kuchoma moto nyumba si busara, mali zimeharibiwa, kwa mambo haya tunaliomba Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua wale wote ambao wamehusika katika zile vurugu na uharibifu wa mali, ile gesi ya Watanzania wote," alisema Mwaipopo. Kwa upande wake, Katibu wa BAHAKITA, Chifu Hussein Msopa, alisema vyama vya siasa viache kutumia gesi ya Mtwara kama chanzo cha uvunjifu wa amani.

"Tunaomba ndugu zetu wa Mtwara wawe na subira katika kipindi hiki ambacho Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amekwenda kuzungumza nao. "Tunalaani vurugu zote ikiwamo uchomaji nyumba na uharibifu wa mali, tunaomba Jeshi la Polisi liwachukulie hatua wote waliohusika.

"Tunawaomba wanasiasa, viongozi wenzetu wa dini na asasi zisizo za kiserikali, kuacha kufanya jambo hili mtaji, iwe viongozi wa Kikristo na wale wa Kiislamu, waache kuchochea jambo hili, tuache kupandikiza chuki kwa kuwa suala hili liki achiwa litaibua hoja ya ukanda," alisema Shekhe Msopa.

Source. Mtanzania.

Jamani tusiwashe moto tena kusini cha muhimu kwa baraza la habari hili ni kuangalia je Rasilimali hizo zinasaidia watu wote? Ndipo watoe kauli kama hiyo.

kwa fikra kama hizi, ndio maana twiga hai waningizwa kwenye ndege na kupelekwa uarabuni watu wanjifanya hwayajui. Kudai haki yako inaonekan ni uppuzi?

Matamko kama haya yanakatisha watu tamaa ila kitaeleweka tu.

Watoa tamko hawajaelewa au wanapata faida na mfumo uliopo.Watuweke wazi kwa nini watu wasidai haki zao za msingi pale watu wachache wanapofaidika zaidi.

Huyo Sheikh Mwaipopo hamna kitu kichwani kabisa inaonekana hata hajasoma tamko la shura ya maimamu wa Mtwara. Anatutia aibu kabisa waislamu kwa ukihiyo wake!

hili baraza la habari la kiislam halijui linachezeshwa mziki gani na serikali.
Shura ya maimamu huko Mtwara imeshato tamko lake kuwa sinema ya mtwara inaanza upya.

Na sasa mapambano yanafanyika kiungwana kabisa, hakuna kuchoma nyumba wala kurusha mawe.

Sinema ya sasa hivi ni 3D.

baraza hili sijawahi kulisikia, ndo linajitambulisha kuwepo kwake. watu wamekaa kimazoeazoea ! Noooooooooo!

Tukiwaambia BAKWATA ni pandikizi la ccm huwa mnatubishia kila siku, kiko wapi sasa?
I'm missing you my Hero Sheikh Ponda Issa Ponda!! Mungu atakusaidia utashinda kesi turudi tena kidongo chekundu mpaka hawa wababaishaji na mafisadi wa BAKWATA watupishe.

BAHAKITA ndio kina nani tena khaa? Kama kiongozi wao ni kihiyo namna hiyo vipi mustakbali huko mbeleni?

hili baraza la habari la kiislam halijui linachezeshwa mziki gani na serikali.

Shura ya maimamu huko Mtwara imeshato tamko lake kuwa sinema ya mtwara inaanza upya.

Na sasa mapambano yanafanyika kiungwana kabisa, hakuna kuchoma nyumba wala kurusha mawe.

Sinema ya sasa hivi ni 3D.
Unamaanisha Development Defence and Democracy. Hivi huwa hakuna tamko moja kwa waislamu wote? Maana wengine da ni aibu.

Huyo Sheikh Mwaipopo hamna kitu kichwani kabisa inaonekana hata hajasoma tamko la shura ya maimamu wa Mtwara. Anatutia aibu kabisa waislamu kwa ukihiyo wake!

shehe huyu ananufaika na utawala wa kifisadi au anatumika kama toilet paper maana ni mwepesi wa kutoa kashifa bila kufikiria, ajue ustaarabu ni pamoja na kuheshimu mawazo ya wengine siyo kwenda na kopo la maji maliwatoni tu

Ukisoma habari huu unaona kabisa Sheikh kala mshiko.Hebu aende Mtwara akahutubie hayo aliyowaeleza wana habari kama hajaacha kanzu.

Duh, makubwa, walikuwa wapi siku zote kutoa tamko lao! Wapuuzi tu!

Wameanza wao kwa wao tena kutofautiana?? Movie inaanza.... Where is my popcorn bag

Matusi ni ya nini? Kwani mtu akitoa mawazo yake ni budi atukanwe? Kama una la kuwaelimisha hao viongozi wa DINI basi waelimishe.
Ni kwanini ana PICK and CHOOSE CHAMA... Wa CHADEMA hawajafika MTWARA sijasikia akiwaongelea wa CUF MTWARA wa CUF yule waziri wa afya JUMA HAJI DUNI akiwa MWANZA aliongelea ya MTWARA waachiwe wa MTWARA...

Sasa Sheikh Mwaipopo Unasoma NINI KUPATA VYA DUNIA???

Kisha pewa ubwabwa sasa anashindwa kwa kuupeleka anaamua kuupeleka kwenye gas. Ngoja waislam wezao na shura ya maimamu itasemaje. Angesema askofu hapo hii thread ingekuwa na page Hata 5

huyu huwa anapita pita ofisi za za la aziziz kuchukuwa bahasha zake kama mtikilo

huyu wawapi nae?watu wanataka mtwara iwekama dar?lin itakua kama dar mtwara ikiwa marizote znapelekwa dar apewe ushauli huyo!

Back
Top Bottom