BARAZA la Habari la Kiislamu Tanzania (BAHAKITA), limesema hoja ya watu wa Mtwara kutaka gesi iwanufaishe wao kwanza ni upuuzi, kwa kuwa hoja hiyo itajenga ukanda katika Tanzania isiyoamini mgawanyiko wa kikabila. Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa BAHAKITA, Shekhe Said Mwaipopo.
Alisema kitendo cha watu wa Mtwara na wengine kutoka nje ya Mtwara, kusema gesi hiyo ni yao ni kitendo cha kukosa busara. "Tukianza kugawana mafungu si kitu kizuri. Leo hii watu wa Mwanza wanasema maji yao yasiende Shinyanga hadi wao wayatumie, Wazaramo nao waseme watu wote ambao si wa Dar es Salaam watoke, si hoja ni upuuzi na kauli za kichochezi," alisema Mwaipopo.
Aidha, aliwaonywa baadhi ya wanasiasa na viongozi wa dini wanaotoa kauli za kichochezi na kusema watu hao wamefilisika kisiasa.
"Hawa viongozi wa kisiasa hususani wa Chadema wamefilisika kisiasa, ni wanasiasa uchwara na mbaya zaidi wenyewe wamekiri kupitia Katibu wao Mkuu Dk. Wilbroad Slaa kuwa vitendo vinavyofanywa na watu wa Mtwara ni matokeo ya M4C. "Lakini cha kushangaza ndani ya CCM pia wapo viongozi wakubwa akiwamo Mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnein Murji ambaye alitoa kauli hadharani za kuchochea vurugu za watu wa Mtwara kwa kuwaunga mkono kuwa gesi ni ya kwao.
"Kuchoma moto nyumba si busara, mali zimeharibiwa, kwa mambo haya tunaliomba Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua wale wote ambao wamehusika katika zile vurugu na uharibifu wa mali, ile gesi ya Watanzania wote," alisema Mwaipopo. Kwa upande wake, Katibu wa BAHAKITA, Chifu Hussein Msopa, alisema vyama vya siasa viache kutumia gesi ya Mtwara kama chanzo cha uvunjifu wa amani.
"Tunaomba ndugu zetu wa Mtwara wawe na subira katika kipindi hiki ambacho Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amekwenda kuzungumza nao. "Tunalaani vurugu zote ikiwamo uchomaji nyumba na uharibifu wa mali, tunaomba Jeshi la Polisi liwachukulie hatua wote waliohusika.
"Tunawaomba wanasiasa, viongozi wenzetu wa dini na asasi zisizo za kiserikali, kuacha kufanya jambo hili mtaji, iwe viongozi wa Kikristo na wale wa Kiislamu, waache kuchochea jambo hili, tuache kupandikiza chuki kwa kuwa suala hili liki achiwa litaibua hoja ya ukanda," alisema Shekhe Msopa.
Source. Mtanzania.
Jamani tusiwashe moto tena kusini cha muhimu kwa baraza la habari hili ni kuangalia je Rasilimali hizo zinasaidia watu wote? Ndipo watoe kauli kama hiyo.
hili baraza la habari la kiislam halijui linachezeshwa mziki gani na serikali.
Shura ya maimamu huko mtwara imeshato tamko lake kuwa sinema ya mtwara inaanza upya.
Na sasa mapambano yanafanyika kiungwana kabisa, hakuna kuchoma nyumba wala kurusha mawe.
Sinema ya sasa hivi ni 3d.
....tamko tamu sana hili ila tunamuomba akalitolee mtwara
Bora pachimbike ili wapiga porojo za siasa wakose seheme ya kufanyia ufisadi waoAkili au matope?mafuta ya mtwara ni kwa wanamtwara lakini mafuta ya zanzibar ni ya muungano,patachimbika.
haahaaahaaaa!
BARAZA la Habari la Kiislamu Tanzania (BAHAKITA), limesema hoja ya watu wa Mtwara kutaka gesi iwanufaishe wao kwanza ni upuuzi, kwa kuwa hoja hiyo itajenga ukanda katika Tanzania isiyoamini mgawanyiko wa kikabila. Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa BAHAKITA, Shekhe Said Mwaipopo.
Hawa viongozi wa kisiasa hususani wa Chadema wamefilisika kisiasa, ni wanasiasa uchwara na mbaya zaidi wenyewe wamekiri kupitia Katibu wao Mkuu Dk. Wilbroad Slaa kuwa vitendo vinavyofanywa na watu wa Mtwara ni matokeo ya M4C. Lakini cha kushangaza ndani ya CCM pia wapo viongozi wakubwa akiwamo Mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnein Murji ambaye alitoa kauli hadharani za kuchochea vurugu za watu wa Mtwara kwa kuwaunga mkono kuwa gesi ni ya kwao.
Kuchoma moto nyumba si busara, mali zimeharibiwa, kwa mambo haya tunaliomba Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua wale wote ambao wamehusika katika zile vurugu na uharibifu wa mali, Tunalaani vurugu zote ikiwamo uchomaji nyumba na uharibifu wa mali, tunaomba Jeshi la Polisi liwachukulie hatua wote waliohusika.
Tunawaomba wanasiasa, viongozi wenzetu wa dini na asasi zisizo za kiserikali, kuacha kufanya jambo hili mtaji, iwe viongozi wa Kikristo na wale wa Kiislamu, waache kuchochea jambo hili, tuache kupandikiza chuki kwa kuwa suala hili liki achiwa litaibua hoja ya ukanda, alisema Shekhe Msopa.
Source. Mtanzania.
Jamani tusiwashe moto tena kusini cha muhimu kwa baraza la habari hili ni kuangalia je Rasilimali hizo zinasaidia watu wote? Ndipo watoe kauli kama hiyo.
Nimesoma makala ya Sheikh Mwaipopo na Msopa, hawa jamaa wanachokifanya wanataka popularity au niseme "Umaarufu" wa kidini, na wanajipendekeza kwa serikali. Kwanza ni wanafiki sana. Wanachosema ndicho ambacho wamekuwa wakikipigia debe misikitini. Vurugu za Mbagala ambapo makanisa yalichomwa moto HAWAKUTOA KAULI YOYOTE. Nini nyumba ya mwana CCM mwenzao ukilinganisha na Makanisa tena kwa kosa ambalo limefanywa na age ambayo ni "minor". Ningemuunga mkono sana kama huyu angekuwa aliwahi kutoa kauli ya kuwatuliza WAANDAMANAJI WAKE KULE MBAGALA. Acha kujipendekeza Sheikh Mwaipopo mtaji wako mkubwa ni kukashifu Dini ya Kikristo sijui huwa unalipwa Dinari ngapi????
haki ya mungu njaa mbaya sana kwa kweli..!
Hapo ukimsachi mfukoni utamkuta na ndizi tayari kujiandaa na mikao ya ubwabwa ubwabwa tuh,hovyo kabisa pro- bakwataccm hawa..!
Bure kabisa,ndugu yake nani??
Aende zake mbele huko..,wanafiki na njaa kali wa hali ya juu..