Sheikh S. Mwaipopo: Hoja ya watu wa Mtwara juu ya gesi ni Upuuzi!

Sheikh S. Mwaipopo: Hoja ya watu wa Mtwara juu ya gesi ni Upuuzi!

BARAZA la Habari la Kiislamu Tanzania (BAHAKITA), limesema hoja ya watu wa Mtwara kutaka gesi iwanufaishe wao kwanza ni upuuzi, kwa kuwa hoja hiyo itajenga ukanda katika Tanzania isiyoamini mgawanyiko wa kikabila. Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa BAHAKITA, Shekhe Said Mwaipopo.

Alisema kitendo cha watu wa Mtwara na wengine kutoka nje ya Mtwara, kusema gesi hiyo ni yao ni kitendo cha kukosa busara. “Tukianza kugawana mafungu si kitu kizuri. Leo hii watu wa Mwanza wanasema maji yao yasiende Shinyanga hadi wao wayatumie, Wazaramo nao waseme watu wote ambao si wa Dar es Salaam watoke, si hoja ni upuuzi na kauli za kichochezi,” alisema Mwaipopo.

Aidha, aliwaonywa baadhi ya wanasiasa na viongozi wa dini wanaotoa kauli za kichochezi na kusema watu hao wamefilisika kisiasa.

“Hawa viongozi wa kisiasa hususani wa Chadema wamefilisika kisiasa, ni wanasiasa uchwara na mbaya zaidi wenyewe wamekiri kupitia Katibu wao Mkuu Dk. Wilbroad Slaa kuwa vitendo vinavyofanywa na watu wa Mtwara ni matokeo ya M4C. “Lakini cha kushangaza ndani ya CCM pia wapo viongozi wakubwa akiwamo Mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnein Murji ambaye alitoa kauli hadharani za kuchochea vurugu za watu wa Mtwara kwa kuwaunga mkono kuwa gesi ni ya kwao.

“Kuchoma moto nyumba si busara, mali zimeharibiwa, kwa mambo haya tunaliomba Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua wale wote ambao wamehusika katika zile vurugu na uharibifu wa mali, ile gesi ya Watanzania wote,” alisema Mwaipopo. Kwa upande wake, Katibu wa BAHAKITA, Chifu Hussein Msopa, alisema vyama vya siasa viache kutumia gesi ya Mtwara kama chanzo cha uvunjifu wa amani.

“Tunaomba ndugu zetu wa Mtwara wawe na subira katika kipindi hiki ambacho Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amekwenda kuzungumza nao. “Tunalaani vurugu zote ikiwamo uchomaji nyumba na uharibifu wa mali, tunaomba Jeshi la Polisi liwachukulie hatua wote waliohusika.

“Tunawaomba wanasiasa, viongozi wenzetu wa dini na asasi zisizo za kiserikali, kuacha kufanya jambo hili mtaji, iwe viongozi wa Kikristo na wale wa Kiislamu, waache kuchochea jambo hili, tuache kupandikiza chuki kwa kuwa suala hili liki achiwa litaibua hoja ya ukanda,” alisema Shekhe Msopa.

Source. Mtanzania.

Jamani tusiwashe moto tena kusini cha muhimu kwa baraza la habari hili ni kuangalia je Rasilimali hizo zinasaidia watu wote? Ndipo watoe kauli kama hiyo.

Huyu Mwaipopo ni pandikizi la CCM, siku moja aliitisha kikao na waandishi wa habari pale karibu na Lumumba juu ya maandamano ya vijana wa kislamu kupinga maandamano yanayofanywa na vyama vya upinzani, niliposikiliza pumba zake na nikamuuliza maswali mawili tu nikaona hamna kitu kichwani hata habari yenyewe sikujishughulisha naye hivyo msameheni kwa kupata Coverege huko.
 
Huyu ni kibaraka kwenye kufifisha hoja za wananchi zenye mashiko na kuibana serikali ndio utamuona huyu ubwabwa anatoka mbele kutetea uozo
 
Huyu Mwaipopo ni pandikizi la CCM, siku moja aliitisha kikao na waandishi wa habari pale karibu na Lumumba juu ya maandamano ya vijana wa kislamu kupinga maandamano yanayofanywa na vyama vya upinzani, niliposikiliza pumba zake na nikamuuliza maswali mawili tu nikaona hamna kitu kichwani hata habari yenyewe sikujishughulisha naye hivyo msameheni kwa kupata Coverege huko.
mwaka huu pia kafanya upuuzi huuhuu imekuwaje mtu kama huyu ameendelea kuwa hai mpaka mwaka huu?
 
Naam Hao wame mwaga kwenye misikiti yote nchini , Usiwaone hivyo ni zuga tu hiyo , ukianza kusema ccm vibaya tu wanakwenda kuku report
Nyerere noma sana ,alijilinda kila sehemu sehemu kwa kuweka mainfoma na ndiyo maana enzi zake hadi "wendawazimu" /shoeshiner ilikuwa unakaa naoi mita 100.
 
Mashekhe wa Bakwata mnatakiwa muwaogope sana wote wanakuwaga kwenye payroll ya serikali hao
Mkuu

Usijisumbue kuhusu huruma yako kwao

Iliundwa kwa lengo zuri ila muda Uliharibu umaana

Ni kwamba haina mwaminifu kama yule wa mwanzo

Na ndio iko ilivyo

Bakwata kama fuko la utumbo haujui inataka nini
 
Mkuu

Usijisumbue kuhusu huruma yako kwao

Iliundwa kwa lengo zuri ila muda Uliharibu umaana

Ni kwamba haina mwaminifu kama yule wa mwanzo

Na ndio iko ilivyo

Bakwata kama fuko la utumbo haujui inataka nini
Haikuundwa Kwa lengo zuri fuatilia history ya bakwata utaweza kufahamu

Nyerere ndiye muasisi wa bakwata na wakati wanaiunda palikuwa na mvutano mkubwa sana na waislam nchini ,
 
Haikuundwa Kwa lengo zuri fuatilia history ya bakwata utaweza kufahamu

Nyerere ndiye muasisi wa bakwata na wakati wanaiunda palikuwa na mvutano mkubwa sana na waislam nchini ,
Sina shida na nyerere


Mtu ukizaliwa kabla ya muda lazima uwe masihi wa kijamii

Mimi na wengine ni zao maono yake

Shida si tulipo

Tutafanya nini kwa kuweka utofauti kidogo tukiwa mashahidi

Hata utofauti kidogo bado una mabadiliko
 
Back
Top Bottom