Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Walid Omar Kawambwa atenguliwa kwa kukiuka 'misingi' ya Uongozi

Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Walid Omar Kawambwa atenguliwa kwa kukiuka 'misingi' ya Uongozi

Tatizo kubwa la matatizo ya kiuongozi linalouandama uongozi wa Taasisi za Kiislamu hapa nchini ni kukosa centralised hierarchical system kama waliyonayo wenzao Wakatoliki.
Kanisa Katoliki lina mfumo thabiti na imara sana wa kimamlaka kutoka juu kwenda chini. Maamuzi yao yote makubwa, kuanzia teuzi hadi utenguzi wa viongozi, yanaongozwa na Sheria moja ya Kanisa (Canon Law) na kuidhinishwa na mamlaka kuu moja duniani (Vatican). Mfumo huu unawapa uhuru mkubwa wa kitaasisi na kiuchumi, jambo linalowaepusha na upepo wa kisiasa au kuingiliwa na serikali zilizopo madarakani.
Kwa upande wa taasisi za Kiislamu kama BAKWATA, muundo wao wa kiutawala umekuwa "decentralised" na unakabiliwa na ushindani mkubwa wa ndani, huku kihistoria baraza hilo likiwa na ukaribu mkubwa sana na serikali yoyote iliyopo madarakani. Kutokana na kukosa mfumo huo mkuu na thabiti unaojitegemea, maamuzi ya ndani ya baraza—kama huu utenguzi wa ghafla wa Masheikh wa Mikoa—yanajikuta yanagubikwa na hisia za kiitikadi au hisia za shinikizo la kisiasa (kama vile baadhi ya watu wanavyouhusisha na matukio ya Oktoba 29).
Mpaka hapo taasisi hizi zitakapofanya mageuzi makubwa ya kikatiba na kujenga mfumo mkuu unaoeleweka na unaojitegemea kiuchumi, migogoro na sintofahamu za namna hii hazitaisha.
 
Malaria 2 na THE BIG SHOW, maoni yenu tafadhali. Safari hii siyo wale jamaa wa Katoliki. Ni Sheikh wenu wa Mkoa wa Dar Es Dalaam ndiyo anajadiliwa.
Bàada ya kuona ile video ya yule mwanamke dhidi ya sheikh Alhad
Kwa mtazomo wangu mambo 2 inawezekana yametokea
1. Sheikh kateleza
2. Wakubwa hawamtaki akaundiwa zengwe
Zaidi yeye mwenyewe na Muumba wake ndio wanaomjua
 
Bàada ya kuona ile video ya yule mwanamke dhidi ya sheikh Alhad
Kwa mtazomo wangu mambo 2 inawezekana yametokea
1. Sheikh kateleza
2. Wakubwa hawamtaki akaundiwa zengwe
Zaidi yeye mwenyewe na Muumba wake ndio wanaomjua
Hio sababu namba 2 ndio haswaa iliomuondoa, Wakubwa hawamtaki hivyo ile ishu ya yule mwanamke ndio zengwe lenyewe lililoundwa ili kumuondoa.
 
Back
Top Bottom