Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Walid Omar Kawambwa atenguliwa kwa kukiuka 'misingi' ya Uongozi

Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Walid Omar Kawambwa atenguliwa kwa kukiuka 'misingi' ya Uongozi

Tatizo kubwa la matatizo ya kiuongozi linalouandama uongozi wa Taasisi za Kiislamu hapa nchini ni kukosa centralised hierarchical system kama waliyonayo wenzao Wakatoliki.
Kanisa Katoliki lina mfumo thabiti na imara sana wa kimamlaka kutoka juu kwenda chini. Maamuzi yao yote makubwa, kuanzia teuzi hadi utenguzi wa viongozi, yanaongozwa na Sheria moja ya Kanisa (Canon Law) na kuidhinishwa na mamlaka kuu moja duniani (Vatican). Mfumo huu unawapa uhuru mkubwa wa kitaasisi na kiuchumi, jambo linalowaepusha na upepo wa kisiasa au kuingiliwa na serikali zilizopo madarakani.
Kwa upande wa taasisi za Kiislamu kama BAKWATA, muundo wao wa kiutawala umekuwa "decentralised" na unakabiliwa na ushindani mkubwa wa ndani, huku kihistoria baraza hilo likiwa na ukaribu mkubwa sana na serikali yoyote iliyopo madarakani. Kutokana na kukosa mfumo huo mkuu na thabiti unaojitegemea, maamuzi ya ndani ya baraza—kama huu utenguzi wa ghafla wa Masheikh wa Mikoa—yanajikuta yanagubikwa na hisia za kiitikadi au hisia za shinikizo la kisiasa (kama vile baadhi ya watu wanavyouhusisha na matukio ya Oktoba 29).
Mpaka hapo taasisi hizi zitakapofanya mageuzi makubwa ya kikatiba na kujenga mfumo mkuu unaoeleweka na unaojitegemea kiuchumi, migogoro na sintofahamu za namna hii hazitaisha.
Unajua huyo Sheiikh yupo suspended na si dismissed?

Unajua ndani ya BAKWATA ni baraza la ulamaa ndiyo pekee wana jukumu hilo? Baraza hilohilo kama Sheikh akikosea kimaamuzi wana mamlaka ya kutengua uamuzi wake. Mfano Sheikh wa Dar kabla ya huyu, alitangaza kuvunja ndoa ya Dokta Mwaka ila uamuzi huo ulitenguliwa na baraza la maulamaa.

System yao kuna baraza hilo tu na lina mamlaka hayo na si kila mmoja..
 
Bàada ya kuona ile video ya yule mwanamke dhidi ya sheikh Alhad
Kwa mtazomo wangu mambo 2 inawezekana yametokea
1. Sheikh kateleza
2. Wakubwa hawamtaki akaundiwa zengwe
Zaidi yeye mwenyewe na Muumba wake ndio wanaomjua
Safi sana Sheikh. Umeelezea kwa uzuri. Sasa fikiria huyu ni Sheikh mwenzako anayeruhusiwa kuoa wanawake wanne! Vipi kuhusu Mapdre na Maaskofu wa Katoliki wanaotakiwa kuishi maisha ya useja? Unatakiwa uwapongeze kwa kweli. Maana wanapambana na vishawishi vingi.
 
Hio sababu namba 2 ndio haswaa iliomuondoa, Wakubwa hawamtaki hivyo ile ishu ya yule mwanamke ndio zengwe lenyewe lililoundwa ili kumuondoa.
Yeye na huyo mwanamke walifanyaje !?
 
Baraza la Ulamaa BAKWATA limeazimia kumsimamisha Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Walid Omar Kawambwa kutokana na mienendeo inayokiuka misingi ya kiungozi ya Kibaraza

View attachment 3629032

Uamuzi wa Baraza hilo umetolewa leo tarehe 14/07/2026, mara baada ya kukutana katika Kikao cha dharura chini ya Kaimu Mufti Sheikh Ali Khamis Ngeruko ambae pia ni Naibu Kadhi Mkuu wa Tanzania

Soma: PreGE2025 - Rais Samia ameahidi kujenga Msikiti wa Kisasa Vigwaza/Migude wenye hadhi ya Rais. Sheikh Walid ampigia debe urais 2025

Nafasi yake kwa sasa itakaimiwa na Sheikh Abbas Ramadhani ambae ni mjumbe wa Baraza la Mashekhe Mkoa wa Dar Es salaam.

View attachment 3629082
14 July 2026

KUTUMBULIWA KWA SHEIKH WALID, SHEIKH SAID MWAIPOPO ATOA NENO


View: https://m.youtube.com/watch?v=ECSSkyYGwKI
 
Kama hakua mzushi na mnafiki kama yule anaejiita mkiti wa kamati za amani lazima wangempangia njama kumtoa hizi ndio kazi za wale jamaa wanaojiita wanajua kulinda nchi kumbe wanalinda matumbo yao tu..Kuza ana mwanamke kuna ubaya gani hadi mtu atolewe uongozi? je na yeye wamemsikiliza au wamejiamulia wao tu kumtoa...Walid madhali wewe ni muislam basi cheo waachie wewe endelea na iman yako inatosha...
 
Back
Top Bottom