Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Walid Omar Kawambwa atenguliwa kwa kukiuka 'misingi' ya Uongozi

Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Walid Omar Kawambwa atenguliwa kwa kukiuka 'misingi' ya Uongozi

Bàada ya kuona ile video ya yule mwanamke dhidi ya sheikh Alhad
Kwa mtazomo wangu mambo 2 inawezekana yametokea
1. Sheikh kateleza
2. Wakubwa hawamtaki akaundiwa zengwe
Zaidi yeye mwenyewe na Muumba wake ndio wanaomjua
Wakubwa akina nani?
Huko Bakwata Kuna mkubwa kuliko Allah?
 
Kwa nini uikataae namba moja kwani haiwezekani yeye kuteleza na kufanya dhambi??
Yote yanawezekana Allah ndio mwenye kujuwa ukweli
Sawa, lakini mtu akifanya dhambi si anaitwa halafu anapewa onyo la kwanza. Sababu ya pili ndio iliomponza sheikh wetu wa ukweli, na zengwe ametafutwa huyo dada mkimbizi ili alitie nyongo kabisa ila ukweli ni kua wakubwa hawamtaki.
 
Sawa, lakini mtu akifanya dhambi si anaitwa halafu anapewa onyo la kwanza. Sababu ya pili ndio iliomponza sheikh wetu wa ukweli, na zengwe ametafutwa huyo dada mkimbizi ili alitie nyongo kabisa ila ukweli ni kua wakubwa hawamtaki.
Kama iko hivyo hawamtaki na wamemuondoa kwa hila basi hawaja tenda haki. Lakini kama hiyo binti alichokuwa ana sema yupo sahihi na ni kweli basi ywamuzi ulochukuliwa ni sahihi kabisa kwa hao Bakwata kulinda heshima ya taasisi yao kwa wafuasi wao. Ukiangalia hii kadhia kama ina ukweli ni imechafua masheikh wote na taasisi kwa ujumla. Fikiria angeachwa na kashfa hiyo nini watu wangesema juu ya Taasisi na masheikh
 
Baraza la Ulamaa BAKWATA limeazimia kumsimamisha Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Walid Omar Kawambwa kutokana na mienendeo inayokiuka misingi ya kiungozi ya Kibaraza

View attachment 3629032

Uamuzi wa Baraza hilo umetolewa leo tarehe 14/07/2026, mara baada ya kukutana katika Kikao cha dharura chini ya Kaimu Mufti Sheikh Ali Khamis Ngeruko ambae pia ni Naibu Kadhi Mkuu wa Tanzania

Soma: PreGE2025 - Rais Samia ameahidi kujenga Msikiti wa Kisasa Vigwaza/Migude wenye hadhi ya Rais. Sheikh Walid ampigia debe urais 2025

Nafasi yake kwa sasa itakaimiwa na Sheikh Abbas Ramadhani ambae ni mjumbe wa Baraza la Mashekhe Mkoa wa Dar Es salaam.

View attachment 3629082

View: https://youtu.be/WcoUxbzr6AA?is=KhkliFvOhmtZgyO3
 
Kwenye Mashekhe wote at least Shekhe Alhad Mussa ndo nilikua napendezwa na haiba yake.. Japo alikua na kauchawa flani but alikua walau anajitahidi.. Ingawa mi ni mkristo lakini yule Shekhe nilikua namkubali content zake.
 
WAMEKURUPUKA KUMTOA HUYO KIONGOZI...
HATA KAMA KUNACHANGAMOTO MTU ANAPISHA UCHUNGUZI NA SIO KUWEKWA MWINGINE MUDA HUO HUO
 
Kwa nini uikataae namba moja kwani haiwezekani yeye kuteleza na kufanya dhambi??
Yote yanawezekana Allah ndio mwenye kujuwa ukweli
Hio sababu namba moja naikataa kwa sababu hio dhambi kwa wanaume rijali wa kitanzania asilimia 90 wanaifanya ndio maana idadi ya masingo maza na watoto wasio na baba ni kubwa sana. Huyo dada mkimbizi wa kirundi wamemtengeneza wakampa na pesa, na kumrekodi na kuirusha mitandaoni ili zengwe litimie wamtimue. Mamlaka ndio imeamrisha aondolewe, Siku aliposema "mwanamke hana mamlaka ya kuongoza nchi" ndio siku iliomponza.
 
Back
Top Bottom