Shekhe Ponda: Kuna nini ndani ya "MUUNGANO" zaidi ya Fitna, majungu na kudumaza Maendeleo ya Raia? Ni heri turudi kama zamani

Shekhe Ponda: Kuna nini ndani ya "MUUNGANO" zaidi ya Fitna, majungu na kudumaza Maendeleo ya Raia? Ni heri turudi kama zamani

Yupo sahihi ! chuki ni real bora uvunjwe watu watapeana heshima
 
Mimi bado nafikiria yule mzee aliwaza nini, aliona nini cha faida kule Zanzibar, alishirikisha kweli watu wazo lake hilo la muungano?
Alifikiria kweli baada ya miaka kumi ishirini baada ya huo muungano tungehesabu faida?

Au ni kwa nini basi aliona heri Tanganyika ife na Zanzibar ibaki, kwake Tanganyika ilikua sio muhimu zaidi ya muungano?

Kwa nini hakuacha hata mwanya kwa wajukuu kwamba tukiona hali imekua sivyo tujitoe?

Ninajiuliza pia kati kumi kama faida zilizopatikana kwenye muungano huu sisi kama Tanganyika tumepata ngapi?
 
Mikopo, wana uwezo wa kuilipa? Zanzibar ina deni kubwa sana kwa Tabganyika,buwa wanaamua tu kuweka siri.

Pesa yote inayokopwa na JMT, sehemu inayopelekwa Zanzibar, haijawahi kulipwa hata mara moja.
Una uhakika imepelekwa kila Senti inayostahiki kupelekwa?
 
Na hao kila siku wanatutukana sisi Watanganyika wakidai tunawanyonya. Uvunjwe huu muungano na tunawafukuza warudi kwao tuone kama watabeba haya majumba yao. Hakuna Mtanganyika mwenye mali isiyohamishika huko visiwani. Tumechoka matusi na dharau zao. Majuzi tu wamesamehewa deni la umeme bilioni 65.
Hawajakaa sawa wakapiga mnada bandari yetu.
 
Tatizo hawana adabu na ndiyo wao wanaanza chokochoko sasa bora tukate mzizi wa fitna yeshe.
🤣🤣🤣😁😁watakufa wagonjwa wengi hospital aisee tuachane nao hao wachumia tumbo kina ponda.
Tatizo ni elimu elimu elimu
 
Shekhe Ponda amesema:

Tanganyika na Zanzibar ugomvi mpaka lini? Mara nyingi tumewazindua kutoka kwenye Jinamizi la " MUUNGANO' Dawa kila Taifa lirudi kama zamani tuishi kama Kenya na Uganda, Malawi na Msumbiji

Shekhe Ponda amezungumza kupita Ukurasa wake wa twitter

My take: Shekhe Ponda badala ya Kujenga anataka Kubomoa

=========

View attachment 2656035
Yes, muungano uvunjwe haraka
 
Back
Top Bottom